Wanachama wa Yanga kutibiwa kwa bei ya punguzo kwenye Hospitali za Agakhan

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Klabu ya Yanga SC, leo hii imeingia mkataba na Hospital ya Aga Khan, ambapo itawafanya wachezaji wa Yanga kupima afya zao, lakini pia wanachama na mashabiki wa Yanga SC kuweza kupata huduma nchi nzima kwenye Hospital za Aga Khan.

Wanachama wenye kadi ya uanachama wa Yanga SC wanaweza kuhudumiwa kwa punguzo la bei kwenye Hospitali za Agakhan ambazo zimeenea nchini.

Mkataba wa Yanga SC na Hospital ya Aga Khan ni wa miaka miwili.

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Klabu ya Yanga SC, leo hii imeingia mkataba na Hospital ya Aga Khan, ambapo itawafanya wachezaji wa Yanga kupima afya zao, lakini pia wanachama na mashabiki wa Yanga SC kuweza kupata huduma nchi nzima kwenye Hospital za Aga Khan.

Wanachana wenye kadi ya uanachama wa Yanga SC wanaweza kuhudumiwa kwa punguzo la bei kwenye Hospitali za Agakhan ambazo zimeenea nchini.

Mkataba wa Yanga SC na Hospital ya Aga Khan ni wa miaka miwili.
Ndugu yangu.
Hakuna mlo wa Bure kwenye dunia ya Kibepari! Nakwambia hakuna MwanaYanga anayeshindwa kulipa Kiingilio cha Elfu 3000/= leo apate punguzo la kutibiwa Aga Khan akatoboa. Hiii ni yale yale Maigizo ya kuwalipia VIPOFU VIINGILIO WAJE KUTAZAMA MECHI ZA YANGA. Tangu lini Kipofu akatazama???
Tangu lini Mlalahoi wa Yombo, Manzese nk asogelee hata geti la Aga Khan! Hebu kuweni na Akili acheni ngojera buana.
AGa Khan Panaodol inauzwa 20,000/= wakati hospital zetu ni Tsh. 2,000/= simply kila huduma imeongezwa zero "0" mbele utawezea wapi wewe kajamba nani????
 
Kwa makolo hili wangeliweka kwenye orodha ya mafanikio ya timu kama lile la kufungua WhatsApp channel.
Luc Eymael aliyewaita nyani aliona mbali sana
FB_IMG_1707213280656~3.jpg
 
Ndugu yangu.
Hakuna mlo wa Bure kwenye dunia ya Kibepari! Nakwambia hakuna MwanaYanga anayeshindwa kulipa Kiingilio cha Elfu 3000/= leo apate punguzo la kutibiwa Aga Khan akatoboa. Hiii ni yale yale Maigizo ya kuwalipia VIPOFU VIINGILIO WAJE KUTAZAMA MECHI ZA YANGA. Tangu lini Kipofu akatazama???
Tangu lini Mlalahoi wa Yombo, Manzese nk asogelee hata geti la Aga Khan! Hebu kuweni na Akili acheni ngojera buana.
AGa Khan Panaodol inauzwa 20,000/= wakati hospital zetu ni Tsh. 2,000/= simply kila huduma imeongezwa zero "0" mbele utawezea wapi wewe kajamba nani????
Kwa hio ulitaka iweje mbona unalia lia
 
Nimeisikia hii taarifa. Ila kwa upande wangu naona bado haijakaa sawa. Maana hawajaweka asilimia ya hilo punguzo.

Nadhani wangeweka wazi watapunguza kwa asilimia ngapi, ili iwe rahisi kwa wanufaika kufahamu kiwango halisi cha hilo punguzo wakati wa kupata matibabu.
Mkuu hayo ni masuala ya kimkataba hayatakiwi kwenda hewani kwa kila mtu. Ila Wahusika (Wachezaji, Wanachama na Mashabiki) watajulishwa vipengele vyote vya mkataba.
 
Wazo zuri Ila sidhani Kama wanachama wa yanga wanajua gharama halisi za matibabu aghakan, Kama wangejua wasingefurahia huo mkataba.
Kingine nawapongeza yanga kuongeza wanachama na kuwapa vivutio mbalimbali wanachama wao sisi Simba hatutaki kuongeza wanachama Ila tunang'ang'ania kuuza Kadi za mashabiki.
 
Klabu ya Yanga SC, leo hii imeingia mkataba na Hospital ya Aga Khan, ambapo itawafanya wachezaji wa Yanga kupima afya zao, lakini pia wanachama na mashabiki wa Yanga SC kuweza kupata huduma nchi nzima kwenye Hospital za Aga Khan.

Wanachama wenye kadi ya uanachama wa Yanga SC wanaweza kuhudumiwa kwa punguzo la bei kwenye Hospitali za Agakhan ambazo zimeenea nchini.

Mkataba wa Yanga SC na Hospital ya Aga Khan ni wa miaka miwili.

Written by Mjanja M1
Jikusanye na ki 50 ujifanye unaenda tibiwa A.K, unaweza pata surprise ya mwaka.
 
Itakuwa wagonjwa wamepungua aghakan. Je mashabiki wa Yanga, watapima tezi dume? Ni vizuri wapime tezi dume ili wajue afya zao.
Aliyekwambia Agakhan wanaenda wote nani? Mabalozi wote na familia zao hukimbilia pale
 
Kwa namna hii Nchi ilivyo na Ujanja janja hawachelewi kutoa punguzo la elfu 7 ama elfu 5 Kwa Kila huduma

Wakati gharama za matibabu hapo Agha Khan ni shilingi 700,000 hadi milioni kadhaa kutegemeana na ugonjwa

Anyways, Kila la kheri Mtani 🤗
 
Nawaomba Yanga watuunganishe na kwa wale vigagula wao wanaowasaidia kuroga mechi, waganga wao wakali sana...
 
Hii ni move kwa Yanga kupata wanachama wengi, yaani mtu asiye na kadi kwa sasa anaweza akavutika baada ya kuona kuna benefits kuwa mwanachama wa klabu...

Kwa namna hii Nchi ilivyo na Ujanja janja hawachelewi kutoa punguzo la elfu 7 ama elfu 5 Kwa Kila huduma

Wakati gharama za matibabu hapo Agha Khan ni shilingi 700,000 hadi milioni kadhaa kutegemeana na ugonjwa

Anyways, Kila la kheri Mtani 🤗
 
Kuliko kutafuta ujiko kuonekana mmechagua hospotali ya Hadhi sana, ingechaguliwa hospital yenye gharama wastani na ubora. Gharama za kuchangia zitakuwa chini kuliko hiyo ambayo hata NHIF hawapokei kutokana na gharama zake kuwa juu sana.
 
Hii ni move kwa Yanga kupata wanachama wengi, yaani mtu asiye na kadi kwa sasa anaweza akavutika baada ya kuona kuna benefits kuwa mwanachama wa klabu...
Absolutely

Ila wangeweza wakaboresha Kwa kutaja hizo percentage za punguzo.

Nafurahi kuona hivi Vilabu viwili vimeanza kuamka Kwa kuajiri wataalamu kwenye masuala Mtambuka, though Kuna pesa nyingi bado inapotea Kwa kushindwa kubuni vyanzo vya uhakika vya mapato
 
Back
Top Bottom