Cheza na Kikwete, yuko kotekote, Kijijini Msoga hapa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
xxx1.jpg

xxx3.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.

Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29, itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya mbogamboga wilayani Rufiji.

Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe. Ameahidi kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.

Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.
mso1.jpg
 
angetumia nguvu hivi kun'goa mafisdi na wezi wa mali za umma na pia kutekeleza ahadi zake wakati wa kampeni he would make a very good president
 
Msoga si ndo kwao? Mheshimiwa anataka kufungua mradi wa ng'ombe afu mnasema mafunzo ya vijana,nchi hii bana
 
Hapo ndipo uwezo wake ulipoishia... tujiulize, yeye akifanya haya:
  • Kawambwa au Mahiza wanafanya nini?
  • Nini ilikuwa content ya semina elekezi?
  • Kama wateule wake hawayafanyi haya mpaka yeye aende, atazunguka vijiji vyote Tanzania?
  • then, nani wa kushughulikia mfumuko wa bei?

Wasanii wengine bwana!!
 
Anataka kufungua mradi wa ufugaji wa kisasa kijijni kwake, na hivyo anawatumia vijana hao kama mafunzo yao kwa manufaa ya mradi wake,
 
Hayo matofali watakayofyatua yatatumika kujengea mabanda ya kuku na ng'ombe wa kisasa! Duh kaaaaaazzzzzzzziiiiii kweli kweli!............
 
Jk bana,eti mafunzo.zamani tukiwa shule ya msingi walimu walituagiza kamba za ng'ombe na mwiko kama sanaa,eti unawekewa max kumbe baadae inapelekwa sokoni.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Asante baba!
Vijana wanatengeneza vigae viko shabby nikajiuliza vitatumikaje? Of coz its a good move lakini ina impact ndogo sana kwa taifa! Hizo machine hata waziri is too big to deliver!
Kweli ngoma imepata mchezaji, sijui kwa nini sijawahi kukutana na kijana wa hii kabila niskie nyimbo zake,lol
Hapo ndipo uwezo wake ulipoishia... tujiulize, yeye akifanya haya:
  • Kawambwa au Mahiza wanafanya nini?
  • Nini ilikuwa content ya semina elekezi?
  • Kama wateule wake hawayafanyi haya mpaka yeye aende, atazunguka vijiji vyote Tanzania?
  • then, nani wa kushughulikia mfumuko wa bei?

Wasanii wengine bwana!!
 
Rais JK Nyerere alifanya haya pia Rais Kagame naye hufanya haya kila Alhamisi (nadhani) JK si wa kwanza kama ameanza nampa big up

Tuwe wakweli
 
Mkuu DC hao uliowataja hawakufanya au hawafanyi hayo na kuishia hapo. Tatizo letu na huyu baba wa kikwere ni kwamba anaishia hapo kwenye huo mchezo mchezo tu, issues kubwa na zinazowasumbua na kuwatesa watanzania kwa ujumla wao kama inflation na mengineyo anayaacha yajishughulikie yenyewe. Siku zote nasema na nitaendelea kusema, kikwete ni mmoja wa watu wenye bahati zaidi duniani. Kuna sababu 2 kuu, kwanza kwa kuwa rais wakati hata ukuu wa wilaya ukiwa serious huwezi kumpa, pili kwa kuwa rais wa Tanzania nchi ya amani (???) duniani. Nchi nyingine wangekosea wakampa urais mtu kama huyu wiki 2 asingemaliza ikulu.

Rais JK Nyerere alifanya haya pia Rais Kagame naye hufanya haya kila Alhamisi (nadhani) JK si wa kwanza kama ameanza nampa big up

Tuwe wakweli
 
Hapo ndipo uwezo wake ulipoishia... tujiulize, yeye akifanya haya:
  • Kawambwa au Mahiza wanafanya nini?
  • Nini ilikuwa content ya semina elekezi?
  • Kama wateule wake hawayafanyi haya mpaka yeye aende, atazunguka vijiji vyote Tanzania?
  • then, nani wa kushughulikia mfumuko wa bei?

Wasanii wengine bwana!!

Wakwere ni wavivu sana ...wacha Angalau awafundishe kazi za mikono waaache uvivu......maana aliwapiga marufuku kuuza mashamba bado haikusaidia sansana....wakawa majaji yanaotaa Hadi milangoni
....
 
Sio mbaya hii kitu ila I expect something bigger than tht..alafu kama vle kwenye pcha ya pili kabadil surual..
 
Rais JK Nyerere alifanya haya pia Rais Kagame naye hufanya haya kila Alhamisi (nadhani) JK si wa kwanza kama ameanza nampa big up

Tuwe wakweli

Kagame hufanya haya mambo kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, ni utaratibu uliopo Rwanda nzima na unashirikisha wananchi wote katika shughuli zote za ujenzi wa taifa. Hivi karibuni, polisi wa Rwanda walirudi toka Haiti ambako walikuwa sehemu ya vikosi mbalimbali chini ya umoja wa mataifa kusimamia amani, na kule nako waliwafundisha wananchi wa Haiti utaratibu huo wa kila mwezi.
Sikumbuki utaratibu wa mchonga ulikuwaje, lakini all in all wanasiasa wa hapa siku hizi huwa wanatafuta photo opportunities kwa manufaa yao badala ya kulitumikia taifa toka moyoni.
 
angetumia nguvu hivi kun'goa mafisdi na wezi wa mali za umma na pia kutekeleza ahadi zake wakati wa kampeni he would make a very good president

Kwani ahadi alizozitoa ni zote zinatekelezeka?
 
Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.

The guy is not short of clangers
 
Hapo ndipo uwezo wake ulipoishia... tujiulize, yeye akifanya haya:
  • Kawambwa au Mahiza wanafanya nini?
  • Nini ilikuwa content ya semina elekezi?
  • Kama wateule wake hawayafanyi haya mpaka yeye aende, atazunguka vijiji vyote Tanzania?
  • then, nani wa kushughulikia mfumuko wa bei?

Wasanii wengine bwana!!

Inaelekea mfumuko wa bei umemshinda ndo maana kajikita kwenye matofali unakotumia nguvu zaidi kuliko akili
 
Back
Top Bottom