johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,897
- 141,833
Rais Mstaafu Mzee Kikwete amewaomba Watanzania waendelee kuiombea Nchi iendelee kuwa tulivu na pia Rais Samia Suluhu Hassan aweze kutafuta Majibu ya Vikwazo vinavyowakabili.
========
RAIS mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, amesema Watanzania wanatakiwa kuendelea kuiombea nchi iendelee kuwa tulivu na pia Rais Samia Suluhu Hassan aweze kutafutia majibu ya vikwazo vinavyowakabili wananchi.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu, viongozi wa serikali, watoto yatima, wajane na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Pwani katika ifutari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge.
Kunenge, aliandaa futari hiyo Ikulu ndogo mjini Kibaha kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Kikwete, alimshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka watoto yatima na wajane kwa kuwapa futari hiyo kwakuwa jamii hiyo inapaswa kutunzwa na watu wote.
Alisema, kitendo cha kuandaa futari hiyo ni kumtukuza Mungu hasa kuwasaidia yatima ambao mahitaji yao yanategemea misaada ya wahisani mbalimbali.
Nipashe
Jumaa kareem.