Chenge kujivua gamba leo?

Chenge kujivua gamba leo?

Status
Not open for further replies.
Jk nchi IMEKUSHINDA, Lowassa kasema huna maamuzi, mimi ninamuunga mkono 100% utapendwa na wangapi wewe? Au kwa vile nawe FISADI? Unatuumiza sana, ningekuwa kijana ningeamua vinginevyo, hata kukimbia nchi. Sasa tutaandamana mpaka KIELEWEKE.
 
Ubunge ndio kinga yake hivyo hawezi kuachia ngazi hata kidogo na huwezi kuwa na chama cha jinsi kama hii
 
Mh. Chenge anapokea ushauri na maoni yenu hapa Chenge John Andrew kuhusu utendaji wake wa kazi na pia kuhusu uvuaji wa GAMBA. Kazi ya TANU wananchi msimuangushe
 
Akwende zake fisadi takataka, kamata jizi, hey polisi meeni.!
 
Ufisadi wa Tanzania ni instututionalize ufisadi hivyo ni wa kitaasisi hivyo kuna ulazima wa kuoverharaul mfumo mzima wa kisiasa Tanzania na kuona unatoa tija kwa watu
 
Uongozi wa JF to be fair to all the members napendekeza W.J.Malecela apewe ban kama wanavyopewa members wengine wanapodanganya.
Badala yake naona MODS wanazidi kumfichia aibu kwa kubadilishabadilisha headings, kwanza mwenyewe aliandika
1. Chenge ajivua gamba leo CC; Mods wakabadilisha
2. Tetesi: Chenge ajivua gamba leo CC; Mods wakabadilisha tena
3. Chenge kujivua gamba leo?; Mods wakabadilisha tena
4. Tetesi: Chenge kujivua gamba leo?

Tatizo lililopo ni kuwa headings zote zinazoletwa haziendani na content ya thread yenyewe ambayo ni a declarative statement "Chenge ameachia ngazi rasmi leo ndani ya CC " In short kadanganya please Mods do a needful.

umejuwaje kama ni Mods wanaobadilisha hizo headings?!
 
Mod ndiye mwenye uwezo wa kubadili headings!!

Si Kweli hili jibu lako la haraka na rahisi kama majibu ya Mkuu wa kaya Tanzania.

Tuendelee kutafuta habari, yeye alipata hiyo sasa kama bado haijathibitishwa si vyema kumlam mtu wakati sisi hatujafanya lolote angalao yeye amejaribu kuangaika na kuleta hiyo ambayo tunasubiri kupata uhakika wake.
 
- According to the datas, Chenge ameachia ngazi rasmi leo ndani ya CC inayoendelea sasa hivi Dodoma!



Willie @ NYC, USA.
So far, hakuna kuachia ngazi wala terraces ....sijui what is this lakini majungu na hisia ndizo zilizoiua CCM
 
Kaka mimi binafsi bado sijaona ufisadi wa huyu mzee wetu malecella, nafikiri ni kati ya wana CCM waaminifu sana wa karne hii. Na sijajua hadi leo ni kipi hasa walitofautiana na baba wa taifa - huyu mzee ana misimamo na ni mtetezi wa watu ingawa jimbo lake la Mtera na mkoa wake wa dodoma umebakia nyuma sana kimaendeleo, lakini hii si sababu ya kumwondolea ushupavu katika uongozi wake.

Sitaki kusema ukiwa kiongozi basi fanya ushawishi ili upeleke maendeleo kwenu, no. ila alikuwa na nafasi kuwaendeleza watu wake - ki fikra ili waweze kujitegemea, ki elimu na ki afya. Mtera ni kati ya majimbo yaliyosahaulika ki maendeleo

Nafikiri Willie @NYC atakubaliana na mimi kwamba ndugu zao huko mtera wako hoi bin taabani.

Chanzo ilikuwa ni yeye Malecela, kushindwa kuzuia hoja ya G55 ndani ya Bunge wakati akiwa ni Waziri Mkuu (Kiongozi wa Serikali Bungeni). Ndipo baada ya hapo Mwl. Nyerere, akaandika kile kitabu cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA.
 
Good News, I like it. What about the others? like Mhe kwa babu wa Kikombeze! poa tunakusubiri upime mwenyewe sisi ni Amani tu!
 
W.J.William,

Mkuu wangu yaani haya wala hayana sababu ya kuyaandika kabisa. Unajua CCM mnachekesha sana, yaani watu walihujumu uchumi wa nchi yetu miaka 6 iliyopita, muda wote wamekuwa wakila bata mbele ya macho yenu wakati hawana madaraka yeyote ndani ya serikali, leo kujiuzuru kwao madaraka ya chama inakuaje iwe sifa ya kujivunia hadi Bungeni. Bunge limekuwa sehemu ya mtu kama Nape kwenda kama mgeni kujivunia kazi ya chama chake kuwavua magamba!....wakati Taifa lipo kizani.

Kusema kweli mimi ningependa sana kuelewa kuhusu hii kujivua magamba. Huyu Rostam au Chenge kuondoka CC au ubunge unaleta unafuu gani ktk Ufisadi wao maana nguvu wanayoitumia ktk Ufisadi haihusiani kabisa na kuwepo kwao Bungeni ama CC..Na kibaya zaidi fedha waliisha iba, tumeshindwa kuwatia hatiani na Taifa lazidi kuwa mufilis hatuna hata umeme kwa mji mkuu....Tunafaidika vipi na kuondoka kwao ktk uongozi wa chama CCM..
 
Chenge nimemuona bungeni leo akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya miundombinu kwa ustadi na mbwembwe nyingi but so far hakuna taarifa yoyote ya kutoka damu kwa kujivua.kama ni ungo au kweli tuthibitishiwe kuwa chanzo cha habari ni kipi?
 
Wacha uzushi!, sie tulioko huku hatuna habari, we umezipata wapi?
 
Naona hiyo haisaidii chama chote cha magamba kiachie ngazi wanawaonea tu na si vinginevyo makima hao.
<br />
Waanze kuachia hao wakishajitoa wataweka mengi wazi na mwisho magamba wote watasaliti amri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom