Chenge aongezewa shitaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge aongezewa shitaka

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mpita Njia, Apr 30, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mods, mukiona inafaa muiunganishe na thread ile kuu.

  waendesha mashitaka leo wameongeza shitaka la kuendesha gari lisilokuwa na bima katika mashitaka yanayomkabili Chenge kwenye ile kesi yake ya kuua watu wawili aliowagonga katika Bajaj.
  Pia, Majid Gharib, yule mmiliki wa bajaj ambaye alikimbia, naye ameongezwa kwenye kesi hiyo
   
 2. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #2
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Majid Gharib, yule mmiliki wa bajaj anakosa gani huyu?
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ameshitakiwa kwa kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva wake
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukiangalia unaweza kubuni kuwa Chenge huenda akakwepeshwa na mauaji na kuhukumiwa kwa hili la kuendesha gari bila ya bima na yule mmiliki wa Bajaji kutolewa kafara.
   
 5. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #5
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Du kumbe nalo ni kosa????
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehe
  yule dereva anashtakiwa kwa kuokoa maisha yake kwa kuruka kutoka kwenye chombo alipoona hana njia ya kukwepa mbogo aliyecharuka.
  ina maana angefariki kwenye ajali pasingekuwa na tuhuma dhidi yake. unajua ajali kama ile mtu unapagawa na inabidi kujihami sana kwani kama angepatikana nadhan mheshimiwa asingekuwa na kesi kubwa sana maana dereva wa bajaji angesulubika kirahisi mno.
   
 7. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Mwiba, Huo ndio muelekeo wa kesi, wewe sheria za bongo huzifahamu?????
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kosa pia!

  BWT....Hiyo avatar yako......? & Location......?....Du mkuu umeamua kabisa?
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,675
  Likes Received: 21,907
  Trophy Points: 280
  Mimi naona kuliko kuzugana kila siku, Chenge wamwachie tuu ili aendelee na majukumu yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama kitukufu na kama kuna uwezekano arudishiwe ule wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali maana toka aondoke ofisi ile Michongo imepungua na visenti havipatikani kwa wingi.
  Sh..xyz taip...
   
 10. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Tehe tehe tehe....
   
 11. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwa asiye fuatilia mwenendo wa siasa za jamuhuri ya Danganyika atashtushwa na hili. Sisi wengine tuliisha acha lipite kama mengine mengi (mazito zaidi) yalivyopita. Sioni umuhimu wa kupoteza muda wa mahakimu kwa huyu mhe. vijicenti (wakati mwisho wa hili unajulikana), nawasihi mahakimu waendelee kusikiliza na kuhukumu kesi za walalahoi kuibiana vijisimu kariakoo na mbagala!

  Huyu ndiye mwenyekiti kamati ya maadili wa CCM, vioja vitupu!!

  CCM nambari one
   
 12. b

  babalynn Member

  #12
  Apr 30, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du, Bongo ni nchi nzuri sana.... hivi kesi kama hii ingemkuta mshkaji tu wa street angekuwa wapi saa hizi? Haya mambo kuna haja ya kutoyafuatilia kabisa maana saa zingine roho inauma mno inatamani ipasuke! Hapa tayari mchongo unachorwa na mzee atahukumiwa kulipa fine kwa kuendesha gari bila bima na kufungiwa leseni miezi miwili, kwisha kazi! Kwa sasa habari kuwa alikuwa amelewa hazisemwi tena, any way tunamuachia Mungu maana nae ana majibu yake, kesi ya Dito iligeuzwa ikawa bila kukusudia ili hukumu iwe kifungo cha nje lakini Mungu nadhani alichoka na ujinga huu.......
   
 13. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  haha, nafikiri anakimbia kujibu shitaka la kwanini aliweza kumuajiri mtu ambaye hana leseni na ndio maana dereva aliamua kutoweka baada ya tukio (mawazo yangu tuu)
   
 14. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Mungu atamhukumu, Ditopile yuko wapi?? RIP Ditopile
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Chenge amrudie Mungu wake maana nina uhakika hawa mafisadi 10 yrs back hawakuwa hata na 2mil bank wamekwapua miaka hii hii...watubu,warudise pesa zote,watubu na washitakiwe mimi jamani inaniuma sana sana nashangaa hv usalama na jeshi hawapo??
   
 16. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  SWALI LA MUHIMU: Kwanini awali shitaka hili halikuwepo, na wakati lilijulikana wazi. Na nini kimewafanya waliongeze sasa shitaka hilo licha ya kuwa lilipigiwa kelele na ndugu?
  Hapa ndipo siri ya kesi imejificha tukibaini kilichowaogopesha kilikuwa nini tunaweza kubashiri pia kesi itaisha vipi/
   
  Last edited: May 1, 2009
 17. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mdogo wangu alikaa keko wiki 2,mwendesha pikipiki alimgonga ubavuni mwa gari na kuumia vibaya,kesho yake mahakamani wakadai hali ya mwenye pikipiki ni mbaya kwahiyo asipewe dhamana.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mjadala huu wote wa nini?
  Hamjui kwamba viongozi mliowachagua si Chenge pekee bali nina maanisha wote mliowachagua kama viongozi wenu( hapana nina maana watawala wenu) at the same time mmewapa tiketi ya kuwaueni, tena kuua yeyote kwa namna yeyote bila kesi?
  Hadi pale wadanganyika tutakapokuwa tumejua kuwa tuko katika utawala mbovu sana tangu uhuru yaani utawala usiokuwa wa sheria kwa wakubwa lakini ni washeria kwa wadogo, hapo tutakapokuwa tumeamka katika usingizi huo, hapatatokea uvunjifu wa sheria wa viongozi wetu kwa dharau kubwa kama ninayoiona sasa hivi.
  Lakini wasubiri tu iko siku watu wanachoka na mbaya inakuwa mbaya.
   
 19. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Sawa lakini wanapaswa kuelewa kuna nchi wanapaswa kuiongoza na watu wa kuwatumikia, ile ole wao siku isiyo na jina inakuja, wala haiko mbali!
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Siku akijaribu kuua ndugu yangu sikubali mambo ya kusafirisha maiti wala pesa ila nami namvaa mbaya iwe mbaya. Tena sintajali ni nani na ana wadhifa gani. Lazima nimuwinde nijilipize kisasiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii wamezoea sana sasa. Tena wameifanya fashion
   
Loading...