Chelsea FC (The Blues) | Special Thread


hapo nimekusoma agost 8, kumbe jamaa alipata mchongo kwa conection ya mzee Grant. Nilitaka kushangaa cheo kikubwa kama hicho mwafrika akipate from nowhere.. Kumbe Grant alikua kocha kabla ya kuja darajani, sasa ikaweje tena UEFA walimpiga mkwara kwamba hana leseni ya ukocha? (kipindi alipochukua timu)
 
UEFA au FA?

 

Mkuu Rockcity native; kumbuka pia kwamba huyu bwana Avram Grant alipata shida ya kupata kibali cha kufanyia kazi nchini Uingereza alipopata kazi Portsmouth Fc na West Ham United...

Ni mambo ya kawaida ya kiutawala..hata CHELSEA FC ina mchezaji kijana mwenye uwezo tulimpeleke kwa mkopo mahala kwa sababu hangeweza kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza; mchezaji mwenyewe anaitwa Wallace anatoka Brazil ni beki wa kulia..
 

mi nasemea leseni yake ya ukocha kipindi kile walikua wamemzingua kuwa hana qualification za ukocha, sasa hapo ndo najiuliza wakati yupo kwao israel mbona alikua kocha? May be labda kuna grade alikua hajafika kufundisha champions league na premier league
 
bila shaka....



 
CHEO CHA TECHNICAL DIRECTOR{SPORTING DIRECTOR}...

Hiki ni cheo ambacho kimechangia CHELSEA FC kuwa na makocha wengi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita:

Mfano; tumekuwa na makocha wafuatao:
Jose Mourinho
Avram Grant
Guus Hiddink
Scolari
Carlo Ancelotti
AVB
Roberto Di Matteo
Rafa Benitez{interim}
Jose Mourinho-part 2


KWA NINI HAWA 'TECHNICAL DIRECTORS' NI CHANZO CHA UTATA?

Mfano 1. Avram Grant hakupenda mbinu za Mourinho; alaf kuna wachezaji ambao huyu Technical Director+ Owner {Roman} walikuwa wanamtaka Mourinho awatumie; lakini kocha hakuwahitaji{Mourinho aliona kama wanampangia kikosi}; mfano kusajiliwa kwa beki Alex Costa kulichangia mtafaruku. Na pia ile ishu ya Andry Shevchenko ilichangia sana..Jose Mourinho alimwamini Drogba..hawa watu wakamletea Shevchenko..basi ndo ikawa hakuna 'amani'...

Mfano 2; Mbali na Technical Director kunakuwa na mtu mwingine ambaye ana nguvu kuliko hata Technical director ambaye ukiwa kocha lazima uishi naye vizuri..mtu huyu anaitwa CEO..

Kwenye timu kama Chelsea..watu watatu wenye nguvu ukimtoa kocha mkuu wa timu; ni Roman Abramovich, alaf kuna CEO{ambaye kwa sasa ni Ron Gourlay aliajiriwa mwaka 2007, baada ya 'fundi' Peter Kenyon kuondoka}..alaf baada ya hapo ndo unakutana na Emenalo..

Emenalo ni kiungo kati ya Timu na Klabu..yaani kiungo kati ya timu ya mpira na uongozi wa juu...

Sasa kama huelewani na Emenalo na CEO..ujue huna kazi..
Ndo maana Mourinho mjanja sana..

alipokuja kawakuta Torres, Ba, Lukaku wachezaji ambao hakuwasajili yeye..hasa huyu Torres ambaye CHELSEA FC ilitumia hela nyingi sana kumsajili..tena kwa utashi wa tajiri..

Sasa Mourinho akaacha kila mtu ameona kwamba huyu jamaa hawezi tena kurudia makali yake ya zamani..sasa anapoomba kumpeleka kwa mkopo Milan{ na hatimaye kuachana naye} ujue ana baraka zote za uongozi wa juu; yaani akina Emenalo na CEO Roy Gourlay wanakubali..

sasa Roman si shida kwake kukubali..anategemea sana akili ya hawa mabwana wawili niliowasema:

Ron Gourlay amekuwa ndani ya Chelsea fc kwa vyeo mbalimbali tangu 2004.
Michael Emenalo kaja 2007...

unaona???:wacko:
 
Naenda kupumzika wakuu; nawatakieni jioni njema na usiku mwema..kesho pia ni siku...:sleepy:

cc: Mentor, Ntuzu, Rockcity native,viol, kunguru mjanja, Mourinho, andybird314, Khantwe, Ladyfurahia, Kituko na fans wote wa Chelsea Fc na hata majirani zetu..:grouphug:
 



Mkuu agosti 8 asante sn mkuu kwa kz nzuri hakika jukwaa linapendeza.

Na kwako pia mkuu usiku mwema.
 
Last edited by a moderator:
wao wakifunga magoli 4 sisi tutafunga 8, wakifunga 2 sisi tutafunga 4, wakifunga 3 sisi tutafunga 6..hatutaki mazoea na hizi timu za wapinzani wetu hata kidogo...

msalime Mr...kwani yuko wapi leo?

Mi yangu macho....na mkichapwa huyu ndugu yako anaingia jikoni. Zimefika shem.....yupo job atakuwa ametingwa
 
asante...

hii JF imetufanya kuwa ndugu ..hasa hapa CHELSEA FC..huyu mdogo wake Ntuzu; anaitwa Mentor sijui yuko wapi leo..:wacko:

Mi yangu macho....na mkichapwa huyu ndugu yako anaingia jikoni. Zimefika shem.....yupo job atakuwa ametingwa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…