Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Wengi wa wanaoichukulia poa Chelsea ni walioanza kushabikia miaka ya 2015. Hawajaiona Chelsea ya asali na maziwa
 
THE BLUES ya sasa hivi imexpire
Wewe ni mfano wa mashabiki waliojichokea, hakuna matumaini tena
Hata hivyo vitani sio lazima wote wawe na imani
Tunasonga mbele, bado viraka vichahce sana ili timu ile ya MOU irudi
Wewe unadhani hawa wamiliki kila siku wapo uwanjani wanapenda Chelsea kufungwa fungwa?
Kuna mambo yanayoendelea nyuma ya pazia kwa ukimya sisi hatujui
 
Hiki ndicho tunachokiita sasa akili ya mpira. Huwezi kuipata kutoka kwa kocha, wala kwenye mazoezi uwanjani. Inatoka moja kwa moja kwenye ubongo — hasa kwenye Prefrontal Cortex. Ndiyo sababu Lionel Messi anacheza kwenye kiwango ambacho wengine hawawezi kufikia. Messi ni genius halisi wa soka.

Hawa wachezaji sasa hivi hawapo
Ingekuwani Pedro Neto hapo angesema asante Mungu na kuutumbukiza wavuni kwenye offside position.

Your browser is not able to display this video.
 
James hayupo bado

Chelsea vs Leeds United

4-2-3-1

--Joao Pedro--

Estevao --- Enzo (C) --- Palmer

Santos --- Caicedo

Cucurella — Chalobah — Acheampong — Gusto

--Sánchez--

Bench
  1. Sharman‑Lowe
  2. Fofana
  3. Badiashile
  4. Sarr
  5. Hato
  6. Garnacho
  7. Neto
  8. Delap
  9. Guiu
 
Sub anayejitambua kisoka ni Pedro neto tuu, Hao wengine n wachovu wengine n wala mishahara ya bure.
 
Sub anayejitambua kisoka ni Pedro neto tuu, Hao wengine n wachovu wengine n wala mishahara ya bure.
Hapo ndio utajua kuwa Chelsea bado inatakiwa kuingia sokon baada ya kutumia zaidi ya 2bn
Ila Sarr na Fofana bado ni sub nzuri
 
Kwamba sababu ya cucurela kutoka n ipi?
Ila huyu kocha kuna namna afundishwe namna ya kupanga kikosi
 
Kwa ufupi n kwamba Leeds amenufaika Na Sisi Kwa 100%

Amepata points 4, Huku Sisi tukipata point 1 😂
 
Ile tap in aliyokosa Palmer angekuwa ni Jackson kamati ya lugha chafu ingekaa kikao cha dharula
 
Chelsea inaongoza kwenye ligi kwa kufungwa magoli ya kijinga sana
 
Angalia kabisa jinsi Chelsea wanavyokaba — ni vurugu tupu. Ukiwaona makocha wakimuweka Acheampong benchi, hii aina ya ukabaji wa kitoto ndiyo sababu. Gusto ni beki wa hovyo sana; wamgeuze tu awe winga. Halafu Caicedo, Chalobah, Santos… hakuna anayesaidia kukaba.
Ningekuwa hapo uwanjani ningewachapa wote viboko
Your browser is not able to display this video.
 
Palmer na Caicedo leo wametuangusha sana kwenye kuondoka na point tatu
Caocedo katoa penalti ya kijinga sana
Palmer kakosa goli ambalo hakupaswa kukosa
 
Kama mafala vile, wanarukaruka tuu
 
Mpira ni mchezo wa makosa lakini huyu dogo anastahili kwenda kwa mkopo timu zisizo na pressure akapunguze makosa ya kitoto
otherwise ili kosa linaweza mgharimu future yake ndani ya club
 

Attachments

  • 20260211_151436.jpg
    24.4 KB · Views: 30

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…