Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chochote ndo kombe gani mkuu🤠🤠....bwabwaja sana ila tafadhali sana j2 tunaomba sana iwe London is always blue🤠🤠...msituangushe ndugu zetu wazee wa pira singeli
Hahahaha ......... jipambanieni wenyewe jirani, hiyo london always blue tutakutana nayo huko mbele vs Arsenal.
 
wakiendelea hawa hawa Sporting Director tuseme kwamba sisi na mafanikip bye bye.

Sahiv tunaongozwa vibaya mno,Sijawah ona wajinga wanaorudia same mistake kila mda bila na wenyewe kujiangalia.

Wasipobadilika tutaendelea kutia aibu mpka basi
 
Kibarua cha Enzo Maresca kiko mashakani kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu na sintofahamu inayoendelea kati yake, bodi ya uongozi na wamiliki wa klabu. Hali hii imezua maswali makubwa kuhusu mustakabali wake ndani ya timu.

View attachment 3523327
Maresca kosa lake kubwa ni kumuendekeza garasa Caicedo. Hakuna kiungo pale ndio maana tangu asajiliwe hakuna kombe lolote la maana. Ni liability hata aje nani as long as caicedo ndio kiungo timu yenu lazima ipigwe
 
Haya akitoka Maresca unadhani nani mzuri zaidfi yake wa kumridhi
 
Enzo Maresca, ni kocha mzuri hata kama mara nyingine hufanya maamuzi ya kutatanisha kama Alejandro Garnacho. Hakuna kocha asiye na mapungufu; kila mmoja ana dosari zake. Lakini Maresca aliendana na kikosi hiki. Mchanganyiko wa wachezaji waliopo si aina ambayo kila kocha anaweza kuimudu.

Kwa upande mwingine, tatizo kubwa liko kwa wamiliki, kwa sababu hawatamleta kocha bora kuliko Maresca kama wengi wanavyodhani. ataletwa puppete wa kutekelezwa matakwa ya wamiliki tu.

Endapo Maresca ataondoka na wakaanza mchakato mwingine wa kutafuta kocha, wale mnaoshangilia aondoke mtaachwa midomo wazi—kama ilivyotokea Thomas Tuchel alipoondolewa na wakamleta Graham Potter. Sasa wakimfukuza Maresca, au Maresca mwenyewe akiamua kujiuzulu, msishangae wakileta Vítor Pereira au Ange Postecoglou.
 
Enzo Maresca ametofautiana na Behdad Egbhali.
(@alex_crook)

Enzo Maresca hampendi Behdad Eghbali, Mauricio Pochettino hakumpenda Behdad Eghbali, mashabiki hawampendi Behdad Eghbali, na hata Todd Boehly—ambaye ni mmiliki mwenza wa klabu pamoja na Eghbali—hawampendani.

 
Leo ndio siku ambayo Enzo Maresca na Chelsea wanaweza kuachana kabisa. Inabashiriwa kuwa Enzo Maresca hatakuwepo kwenye mechi ya Chelsea dhidi ya Mancity siku ya jumanne. Kuna uwezekano Chelsea wakacheza na Man City chini ya uangalizi wa Willy Cabalero Kipa wa zamani wa Man City
 
Ikiwa Maresca ataondoka Chelsea leo, atakuwa na orodha ya kuvutia ya mafanikio katika msimu wake wa kwanza:
1) Kushinda Conference league,
2) Kuinua FIFA CWC na kuifanya Chelsea kuwa timu pekee iliyoshinda mataji yote makubwa
3) Kurudisha timu kwenye Champions league baada ya kuwa nje kwa miaka 3
 
Je, Chelsea wakiamua kumuajiri Cesc Fàbregas au Roberto De Zerbi, kweli unaona hao ni upgrade ya Enzo Maresca?

 
Hiyo record yenu mtakuja kuivunja wenyewe Arse88, sisi city watupige saba tu zinatutosha. Halafu hasira zetu tunajua tutazishushia wapi.
Hivi kuna timu mmeifunga tano kuanzia misimu mitatu nyuma? Na hili swala la kocha wenu kutaka kuondoka unalionaje
 
Yani kocha yoyote atakaye waendekeza caicedo na lavia lazima atimuliwe. Hakuna wachezaji humo.
 
Maresca akiondoka Chelsea kuna timu nkubwa kubwa tu zinamsubiria huko nje.
 
Hivi kuna timu mmeifunga tano kuanzia misimu mitatu nyuma? Na hili swala la kocha wenu kutaka kuondoka unalionaje
Unazifunga timu 6 au 5 halafu msimu unatoka mikono mitupu!!, sisi hatunaga uvumilivu na matapeli, kama nyie mnavyomvumilia huyo tapeli wenu Arteta.

Maresca kaja kachukua makombe tunafukuza, atakuja mwingine atachukua,Tapeli wenu yupo tu anawadanganya na phase, hivi mpo phase ya ngapi vile?
 
Kocha wenu ni mbovu acheni kujificha kwenye kivuli cha kikombe uchwara.

Pale United Ten Hag naye alifukuzwa kwa sababu ya matokeo mbaya na sio kwa sababu ya mataji
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…