Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

😁😁😁 Lile kombe liliwadanganya mkadhani mna timu nyie hamna utofauti na Eibar.
 
Acheampong amejitahidi
 
Acheampong amejitahidi
Yeah. Kwenye kuzuia kajitahidi sana ila kwenye kupenyeza pasi zile za vunja mstari alijaribu mara mbili kidogo atufungishe goli, wenzake walikuwa sharp kuzuia. Baada ya hapo akaamua kucheza kwa tahadhari sana bila kupiga mipira mbele. Ukweli ni kwamba tutahitaji CCB, Acheampong anatakiwa mechi za size yake ili akue bila presha
 
Gittens hamna kitu, afadhali aliyoingia EstΓͺvΓ£o game likaanza kuchangamka.

Palace wamecheza kibingwa sana, wangekuwa wanaingia sana kwenye goli pinzani wangeondoka na point tatu leo mapema sana.
 
Enzo hayuko fiti kabisa na nililiona hili tangu pre season
 
Mimi si huwa nawambia hapa? Nikiwambia mchezaji fulani ni takataka muwe mnaelewa, nafuatilia sana michezo na wachezaji.

Narudia tena, hawa wachezaji ni matakataka.

Nicolas Jackson
Christopher Nkunku
Liam Delap
Jamie Gittens
Romeo Lavia
Wesley Fofana
Jorrel Hato
Benoit Badiashile
Axel Disasi
Robert Sanchez
 
Yule mwenye jezi no 08 unamuogopa au umesahau
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…