Ntuzu nashukuru kwa taarifa,
arsenal leo wametoa suluhu, sasa tupo kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kupanda juu, maana naona arsenal ameamua kutuachia njia kabla hajakutana na man u anayoiogopa kwa kuuziwa matta
Remember this guy???
Remember this guy???
hii mutu hatare sana,moja kati ya mabeki shupavu!hv yuko wapi huyu?
LEGENDS
3. CLAUDE MAKELELE:
Huyu mchezaji hajatokea kama yeye kabla na baada yake. Alikuwa anacheza mbele kidogo ya mabeki wa kati kama kiungo mkabaji.
Alisajiliwa kutoka Real Madrid msimu wa 2004.
Alikuwa anavaa #4.
Website ya Chelsea inasema hivi kuhusu Makelele; "The only Chelsea player to have had a position named after him."
Yaani jukumu alilokuwa nalo uwanjani hakuna mtu amewahi kuwa nalo kabla yake. Huyu jamaa alikuwa anakaba; Kushoto kwake Thiago #30, na Frank Lampard #8. Nyuma yake John Terry, Calvaho,Gallas na Paulo Ferreira.
Msimu huo tulicheza mechi zote za ligi (mechi 38) na kupata clean sheets 25.
Tulifungwa magoli 15 tu msimu mzima na tukawa mabingwa wa kihistoria kwa kufikisha points 95.
Tulifungwa magoli 6 tu msimu mzima kwenye uwanja wetu wa Stanford Bridge. Yote hayo kwa sababu huyo Jamaa Claude Makelele. Aliondoka mwaka 2008, akiwa mchezaji huru. Chelsea walimwacha aende huru kwa sababu ya heshimu aliyokuwa nayo kwenye timu.
Sitaki kusema mengi kumhusu Claude Makelele; maana nilishasema tayari; cheki hapo.
When it comes to Makelele, I wish I could turn back the time. Matic anaweza kukua na kusaidia sana Midfield yetu, nilicheck game na Stoke City alifanya vizuri sana, anaweza kuwa Makelele mdogo. Matic plays the ball before it gets to him, he is really cool
Zinedine Zidane alimwambia hivi tajiri wa Real Madrid alipomwondoa Makelele na kumleta David Beckham kwenye timu ya Madrid; "Why put another layer of gold paint on the Bentley when you are losing the entire engine?
They really lost an engine, they actually never recovered the loss. They tried with Diarra and so many more but no one got to that level, even Khedira is far from Makelele's midfield performance