Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea will never die nor will drop performance. Atakayekuja anaweza akawa mnyama kuliko Abramovich akakiwasha zaidi namkapoteana humu. Hakuna mtu anayekubali kuwekeza more than 4bn pound halafu akafanya maksihara kwenye usajili na kumaitain quality performing team. No on this planet. Huu ni uwekezaji mkubwa kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa michezo yote - all sports combined duniani. Kwa hiyo wana Chelsea tukae mkao wa karamu kila msimu na kwa kila mechi
 
Ukirusha ndoano lazima kambare litanasa. Napenda mnavyotetea mada kama vile tuko mahakamani.
 
Tukiwaambia watu Chelsea ni BIG team hawakubali. Hii bei ya paundi bil 3 sijui ni timu gani EPL ingeweza kufikia kama leo ikiwekwa sokoni
Mkuu kuna tim zina bei kuliko hata chelsea unategemea leo hii liverpool akipigwa mnada, itazidi bei hiyo, hata man utd japo kuwa ni wabovu lakini kwenye mnada pesa yake itakuwa juu, huoni hata commercial wanamikataba ya pesa ndefu japo hawafanyi vizuri.
 
Hayo ni mawazo yenu mliojitengenezea nyinyi alafu mnatusingizia sisi hata Chelsea ikipata mmiliki mpya still itaendelea kufanya vizuri kutokana na kuwa na structure nzuri ya utendaji wa management tukiongozwa na raisi wetu Bruce buck na mwanamama mwenye akili kubwa marina akisaidiana na Peter Cech labda kama hawa wangeondoka but habari zinasema hawa wataendelea kwenye nafasi zao kama kawaida wamiliki walioingia kwenye top 4 wote wamecomfirm hivyo.Lakini pia kuna vipengele Chelsea wameweka kwa mmiliki yoyote atayekuwa mmiliki wa team kwanza nikuifanya Chelsea kuendelea kuwa shindani kwa kuwekeza kwenye kikosi, kupanua uwanja wa stamford bridge lakini pia kuwekeza kwenye soka la vijana na soka la wanawake
 
Wamiliki wa Chelsea wanamiliki Assets zipi? Na wamiliki wa Liverkuku wanamiliki assets zipi?
 
Yani £3B ni hela ya mboga mboga? hauko serious mkuu matajiri wenyewe wa ulaya hawafikii utajiri huo halafu kumbuka chelsea inapigwa mnada na serikali ya UK sio kwamba inajiuza yenyewe kitu ambacho ingezidi thamani ya hiyo hela
 
Yani £3B ni hela ya mboga mboga? hauko serious mkuu matajiri wenyewe wa ulaya hawafikii utajiri huo halafu kumbuka chelsea inapigwa mnada na serikali ya UK sio kwamba inajiuza yenyewe kitu ambacho ingezidi thamani ya hiyo hela
Naongezea wamejitokeza almost matajiri 30 walionyesha kuitaka Chelsea na sasa hiv wamechujwa wamefika watu wa 4 muulize ingewekwa sasa hivi liverpool sokoni wangepata idadi kama wa Chelsea?
 
Naongezea wamejitokeza almost matajiri 30 walionyesha kuitaka Chelsea na sasa hiv wamechujwa wamefika watu wa 4 muulize ingewekwa sasa hivi liverpool sokoni wangepata idadi kama wa Chelsea?
Pia ukiangalia hao waliotoa ofa utajiri wao ni kikundi sio mtu mmoja kama Roman mwenyewe alivyomiliki halafu mtu anakwambia £3B ni hela ya mboga mboga
 
Hivi "Ko" ni kituko cha wapi au mimi ndiye napitwa na wakati wadau?

Nitoeni ushamba nijue maana ya hili neno "Ko" wakuu [emoji87]
Ko wanalazimisha ya kiswahili badala ya ile ya english ya Co ikiwa na maana ya The company of, au umoja wa.. nk.
ikiwekwa Ko maana yake ni Knockout. sasa watu wanazichanganya bila kujua
 
Wapi umetoa hiyo, sisi tunaongelea uhalsiia, mnada bado unaendelea. Asset zipi Liverpool anayo ya kufikisha bn 5 hata hiyo ya bn 2.5 kama mliacha basi mlizingua hamtapata tena
 
Najua zipo timu ila kuna watu napenda wanavyojigonga kwenye mada kama hizi, Manu bado wako juu yetu ila ikiwekwa mnadani inaweza isizidi b3, liver ndio sidhani kama hata watakaribia, labda 5 yeras to come wakiednelea kufanya vizuri na Salah bado anaichezea Liverpool
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…