juan david
JF-Expert Member
- Jan 23, 2013
- 3,976
- 5,463
Mkuu issue ya kutaifishwa tim sio issue ndogo, halaf Roman ameikopesha chelsea almost 2BLN unahisi ukitaka kutaifisha mali zake vipi huo mkopo wake?Na wewe kweli kweli unaamini watakuwa fooled!! Waingereza. Hata wabongo huwezi kuwafool kihivyo. Roman mwenyewe anajua. Hii case ni sensitive na tusiilinganishe na ushabiki wetu. Waingereza wako inch away kutaifisha mali za Abramovich ikiwemo Chelsea. Maombi yetu iangukie mikononi salama. Uingereza ni rafiki mkubwa wa Ukraine na adui mkubwa wa Urusi, isije kwua walikuwa wanaiosubiri tu hii siku waweze kujustfy utaifishaji wa mali za tycoons wa kirusi ili kuwapunguza nguvu. Vita bado vinaendelea, Urusi wameshaanza vita vya ardhini na wako wanaelekea mji mkuu wa Kyiv. Ukraine inashambuliwa kutokea kila upande. Putin mwenyewe katishia kutumia silaha za neacleaur kwa watakapinga uvamizi wake. Ukijumlisha yote hayo unadhani hasira ya Serikali ya Uingereza inapoa au inaongezeka, unadhani kuwa wanasiasa wataach kuongea au ndi wataishinikiza Serikali kuchukua hatua zaidi. Mimi binafsi simuoni Roman Abramovicha akiokoka kwa hili. Sipendi iwe hivyo ila huu ndio ukweli
Ndio maana wanaongea hivyo ni hao wanasiasa ila Boris mwenyewe last time ameulizwa akakosa majibu
Unakumbuka issue ya matajir wa newcastle hawa wasaudia, baadhi ya wanasiasa siwalikuwa wanataka premier league izue newcastle kuuza kisa tu matajiri wake walihusika kwenye kifo cha Jamal Khashog