Mason Mount

Taarifa zinasema Mount hakupoata majeraha mabaya kwenye ankle yake kwa hiyo asipocheza mechi na Liverpool hiyo nyingine atakuwepo
Jumatano alikuwepo kwenye mazoezi na wachezaji wengine akifanya mazoezi nyepesi nyepesi
nilitembelea page ya coquelin watu wamemtukana balaa 🤣 🤣
 
Tupaki basi kwa nyinyi vibogoyo , hayo ni masikhara aise
 

Acha utani wewe Klopp ni kama Pep hawana Falsafa za kupaki Basi hata kama mchezo utakuwa Mgumi kiasi gani.

Halafu tena apaki basi kwa Kajitimu cha Abraham na Tomori wakati hakupaki basi wakati wa Hazard na Diego Costa?

Tena unathubutu kusema ni Anfield source????
 

Yani Liverpool ya 2014 ndiyo unaifananisha na hii ya Leo?
Unaishi kwenye Sayari gani wewe bro?

Unadhani Liverpool ya 2014 VVD angeiwacha Man City na Chelsea zilizokuwa zikimtaka na kuja Liverpool??

Liverpool ya 2014 unadhani Alisson angelikuja kujiunga??

Hiyo Liverpool uliyokuwa ukitupokonya wachezaji usidhani kama ndiyo hii ya sasa.

Sasahivi nasisi tupo very powerful kwenye Soko.

Kwa hapo uengereza linapokuja suala la kugombania Mchezaji kwasasa hakuna Timu ya kutuzidi! Labda Timu iweke Mshahara Mkubwa kuliko tutakaomuekea sisi huyu Mchezaji.

Nakushauri uhame kutoka mwaka 2014 na uishi katika mwaka 2019 huu tuliopo.

Mwaka 2014 ilikuwa hata wachezaji average tunapowataka walikuwa hawatutaki wanatukimbia!

Lakini sasahivi ni sisi ndiyo tunaowakataa wachezaji, Sio sisi tena tunaokataliwa.

Mfano:

1) Tulimtaka Fekir baadae akakataliwa kwenye vipimo vya Afya

2) Tulimtaka Pulisic mwisho tukafika £15m, Dortmund walipotaka £55m Klopp akaachananae na kumpotezea kabisa

3) Tulimtaka Joginho kabla ya Man City na Chelsea, Klopp alipoona Napoli wanafanya Mbwembwe kumpandisha dau kila siku! Kaamua kumpotezea kaenda kwa Fabinho.

Hao niliowataja wote walikuwa wanalia na kutamani usiku na Mchana lakini Klopp kaamua kuondosha interest kwao.

Kwahiyo kwasasa usijigambe huna Chelsea haina uwezo wa kupambana na Liverpool kwenye soko la kugombania Mchezaji.

Sio VVD tu, hata Chamberlain kumbuka mulimtaka nyinyi Chelsea mwanzo akawakatalia akaichagua Liverpool hii ikionesha kuwa Tumeshafanya Mapinduzi kwenye Soko la usajili.

Hatupo tena kwenye mwaka 2014 Ndugu be realistic
 
Wakati wa uhamisho wa kuja Chelsea alihisi kuface a massive competition ktk namba anayocheza
 
Wewe unajikanyaga mwenyewe ngoja nikuache
 
Wewe unajikanyaga mwenyewe ngoja nikuache

Ni mashabiki wachache wa Chelsea wanaoweza kuaccept challenge kwa ustaarabu hata kama watakosa points/reasons za kubackup their claims

Wengi wenu munajisemea tu mambo bila ya facts zozote then tukiwachallenge munaishia kusema maneno kama hayo dhidi yetu.

Wengine wanapokosa Facts hujijengea defensive mechanism kwa kutuita kwa sifa mbaya! Mara 'Hatujui lolote' 'Mara hatuna kitu' 'Mara Wapumbavu' and so on.

Sasa nawewe nimekutoa katika Giza la kuishi mwaka 2014 na kukukaribisha mwaka 2019 umeanza kusema nakinyaga! Serious?

Mulimchukua Torres tukiwa tunamuhitaji! Man City walimchukua Sterling tukiwa tunamuhitaji! Sasa kama bado unaishi mwaka 2014 na next Window mukimaliza Ban yenu Njoni Mumtake Mane au Mchezaji yeyote wa Liverpool muone kama mutaweza kumbeba Tena.
Au Man City waje kumtaka Mchezaji yeyote kutoka Liverpool waone kama watafanikiwa tena.

Hii ya sasa sio Liverpool ya 2014 Ndugu usipinge kitu ambacho kipo wazi kiuhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…