Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

VILLAS-BOAS APPOINTED

Posted on: Wed 22 Jun 2011

Chelsea Football Club is delighted to announce that Andre Villas-Boas will be the club's new manager.

He has signed a three-year contract and will start work immediately.

Andre was the outstanding candidate for the job. He is one of the most talented young managers in football today and has already achieved much in a relatively short space of time. His ambition, drive and determination matches that of Chelsea and we are confident Andre's leadership of the team will result in greater successes in major domestic and European competitions.

Andre will bring his coaching experience back to a club he is already very familiar with, having previously worked here for three years. He has always been highly regarded at Chelsea and everyone here looks forward to welcoming him back and working with him.

Chelseafc.com
 
VILLAS-BOAS APPOINTED

Posted on: Wed 22 Jun 2011

Chelsea Football Club is delighted to announce that Andre Villas-Boas will be the club's new manager.

He has signed a three-year contract and will start work immediately.

Andre was the outstanding candidate for the job. He is one of the most talented young managers in football today and has already achieved much in a relatively short space of time. His ambition, drive and determination matches that of Chelsea and we are confident Andre's leadership of the team will result in greater successes in major domestic and European competitions.

Andre will bring his coaching experience back to a club he is already very familiar with, having previously worked here for three years. He has always been highly regarded at Chelsea and everyone here looks forward to welcoming him back and working with him.

Chelseafc.com


Welcome back Andre!
 
English powerhouse Chelsea have appointed former Porto coach Andre Villas-Boas as their new manager. The Portuguese tactician has signed a three-year deal with the London giants.

Chelsea were in the market for a new manager ever since the departure of Carlo Ancelotti in May and they have now found their man. The 33-year-old Villas-Boas resigned as Porto coach on Tuesday and now returns to the club where he previously worked at Chelsea as Jose Mourinho's assistant.

"Andre was the outstanding candidate for the job. He is one of the most talented young managers in football today and has already achieved much in a relatively short space of time," a statement on the Chelsea website reads.

"His ambition, drive and determination matches that of Chelsea and we are confident Andre's leadership of the team will result in greater successes in major domestic and European competitions.

"Andre will bring his coaching experience back to a club he is already very familiar with, having previously worked here for three years. He has always been highly regarded at Chelsea and everyone here looks forward to welcoming him back and working with him."
 
Safi sana Chelsea!! Bado tunasubiria kwa hamu Chelsea ya kubeba makombe kama ya kipindi cha Mourinho.
 
Tumeshawazoea hao,..tunampa msimu mmoja then anatimuliwa kama kawa.
 
Jamaa ajawai kucheza mpira ila aliamua kusomea maswala ya mpira tangu akiwa na umri wa miaka 17.amekuwa na kocha jose mournho tangu alipokuwa porto akaja nae chelsea then inter na tangu mwaka 2009 alijiamin na kuwa first coach timu ya academicia ya ureno akaiweka katika ali mzuri ilikuwa inasuasua kama west ham na ndipo alipoibukia porto na kwa msimu moja ameweza,chukua vikombe vitatu akiwa na porto.bila shaka wapo wachezaj watakao timuka kwa upande wa strike na kiungo ndani ya chelsea ni kocha wa kwanza mwenye umri mdogo kufundisha timu inayoshrk epl.viva chelsea viva abroamvich.
 
Tatizo la Chelsea siyo COACH is UZEE wa wachezaji! Kuanzia Drogba, Terry, Essien, e.t.c!
 
We babuu blesed leo umeyumba!!!!na hiyo ni dalili za kuweweseka na mwaka huu moto mtauona!!!!
 
Expect new, young and fresh faces in the team.. Long live chelsea f.c
 
Thubutu... sasa ndio habari zetu zimekwisha. huyo kijana ndo kiboko yenu nyote
 
Kesho utasikia Chelsea wanamtaka Moutinho, Falcao et al... Jamaa umri sawa na most Chelsea senior players wasije wakamkosea adabu tu.
 
Haya yaani huyu kocha kaja kipindi kibaya labda abramovich abadili timu kocha hana experience ya kufundisha majina makubwa as a manager.
yaani ni rahisi wenger kuchukua champions league msimu ujao kuliko chelsea kuchukua EPL.
 


Poleni wakuu naona mmeruka mkojo khe khe kheeeeeeeeeee

kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee


carousel-villas_1331967a.jpg



Tunamtakia mafanikio walikoelekea wenzake
khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeee


 
Hongereni sana Mashabiki wa Chelsea kwa kuajiriwa Andres Villa Boas kama kocha wenu mpya akija kurithi nafasi ya muitaliano Carlo Ancelotti .
Kwa kutazama rekodi ya Andres Villas Boas mashabiki wa Chelsea wana kila sababu ya kuwa na furaha kwa sababu kuu mbili . Nazo ni rekodi ya Villas Boas ambayo ameipata kwa haraka.


Andres Villas Boas ameweza kutwaa kombe La Ligi ya UEFA Europa , kombe la chama cha soka cha Ureno, pamoja na ligi kuu ya nchini Ureno.Hayo yote ameyafanya ndani ya misimu miwili tena akiwa na bajeti ndogo sana ambayo kwa kawaida haitoshi kusaidia timu kufanikiwa katika ulimwengu wa leo . Sababu kuu ya pili ni ukweli kuwa Andres Villas Boas ni mtu ambaye kiukweli anaujua mchezo wa soka na zaidi ya hilo anaifahamu vyema Chelsea kwani aliwahi kukaa kwenye benchi la ufundi la Chelsea chini ya Jose Mourinho hivyo ujio wake hautakuwa wa taabu sana na kuna uwezekano mkubwa kuwa anaweza asihitaji muda sana kuzoea mazingira ya Stamford Bridge pamoja na falsafa na mtindo wa timu ya Chelsea .

Tukitazama upande wa pili hapo ndio kuna utata zaidi . Labda turejee nyuma zaidi na kujiuliza kwanini aliyekuwa kocha wa Chelsea kabla ya ujio wa Villas Boas alifanya nini kibaya hadi kufukuzwa kazi . Carlo Ancelotti ni kocha aliyejijengea jina na heshima kubwa ulimwenguni kote . Heshima aliyonayo Ancelotti ni kutokana na kazi kubwa aliyoifanya akiwa na timu za Juvetus na AC Milan ambapo alitwaa mataji mengi ya ndani na nje ya nchi yake Italia . Kwenye msimu wake wa kwanza nchini England Carlo Ancelotti aliweza kulirejesha taji ambalo Chelsea ililipoteza kwa misimu mitatu taji la ligi kuu ya England , pamoja na hilo alifanikiwa kutwaa taji la kombe la FA.

Kitu ambacho Chelsea ya Roman Abramovich imeona kama kosa la jinai ambalo limemgharimu Ancelotti ajira yake ni kutotwaa taji la Ligi ya mabingwa barani Ulaya ambalo Roman Abramovich analitaka kwa udi na uvumba .Swali la kujiuliza ni moja , kwanini Chelsea imeukosa Ufalme wa ulaya ??? Kunaweza kukawa na majibu mengi kutoka kwa watu wenye mitazamo tofauti lakini nadhani jibu ambalo wote tutakubaliana nalo ni ukweli kwamba Chelsea walipokutana na Manchester United walizidiwa na timu ambayo ilikuwa bora zaidi yao.

Kusema kweli huwezi kujilaumu sana unapofungwa na timu kama Manchester United tena kwa mikwaju ya penalti , na zaidi ya hapo inapokuja ligi ya mabingwa kuna timu ambazo ubora wake huwezi kuufananisha wala kuupima . Mfano mzuri ni jinsi Manchester United walivyosasambuliwa na Barcelona kwenye fainali ya ligi hiyo ya mabingwa tena kwa mara ya pili wakirejea yale waliyoyashuhudia mwaka juzi mjini Rome . Kama Roman Abramovich angekuwa mmiliki wa United ina maana Sir Alex Fergusson angekuwa hana ajira ?

Kabla ya Ancelotti alikuwepo Avram Grant ambaye kama isingelikuwa mvua kubwa iliyonyesha na kumfanya John Terry ateleze na kukosa penati ya muhimu pengine angeendelea kuwa kocha kwani Chelsea walicheza vizuri usiku ule na bahati haikuwa yao kwani United walicheza vizuri mwanzo tu na baada ya hapo Chelsea walikamata usukani na kusawazisha bao la Cristiano Ronaldo mpaka mchezo kufikia hatua ya penati .

Bado kwa Abramovich suala la bahati mbaya halina nafasi na Grant aliondolewa na kazi yake akapewa Felipe Scolari ambaye hakukaa zaidi ya miezi sita , na kabla yake Chelsea waliwahi kuwa na mtu ambaye leo hii dunia nzima inamtambua kama kocha bora kabisa kwenye mchezo wa soka na rekodi yake ni ushahidi tosha juu ya ubora wake Jose Felix Mourinho . Alichokuwa anahitaji Mourinho ni muda na kuungwa mkono kwenye soka la wachezaji na sidhani kama Mourinho angepewa misimu mitano Chelsea angeshindwa kuwafanya wawe mabingwa wa Ulaya . Mbona alifanya hivyo ndani ya misimu miwili tu akiwa Inter ?

Maelezo hayo yote yanaonyesha kuwa tatizo lililopo Chelsea si kwa makocha bali ni mmiliki mwenyewe . Tangu kabla ya mourinho alikuwepo Claudio Ranieri na mpaka leo hii Chelsea imekuwa na makocha sita na katika hao wote zimetumika fedha kiasi cha paundi million 50 kuwaajiri na kuwafukuza tu, jiulize swali moja je fedha hizi angepewa kocha mmoja kununua wachezaji Chelsea ingekuwa wapi?


Tatizo kubwa ni Roman Abramovich , mmiliki asiye mvumilivu ambaye kama angeweza kumpa Mourinho miaka mitano kuna kila ushahidi kwamba si Barcelona , si Real Madrid wala Ac Milan au Manchester United ambao wangesimama mbele ya Chelsea kunako michuano ya ulaya . Makocha wote ambao wamepita Chelsea ukiacha Claudio Ranieri pekee ni washindi na ni watu ambao uwezo wao umedhihirika kwa wapenda soka wote , ni vipi waonekane vimeo Chelsea peke yake ?Jiulize kuwa kama usiku ule uliojaa mvua pale Moscow kwenye benchi la Chelsea kwenye uwanja wa Luzhniki angekuwepo Jose Mourinho na si Avrama Grant je matokeo yangekuwa kama yalivyokuwa kwa United kutawazwa mabingwa wa Ulaya, tazama rekodi ya Mourinho alipokuwa England dhidi ya Alex Fergusson na utapata jibu.


Andres Villas Boas anakuja Chelsea akiwa na heshima kubwa aliyojijengea mapema . Lakini atambue fika kuwa Abramovich ni kinyonga anayebadilika matokeo yanapokuwa mabaya na hatosita kushusha panga kwenye shingo ya kocha pasipo kumpa muda wa kuijenga timu , zaidi ya hapo ni mtu anayependa kuingilia majukumu ya kocha hasa linapokuja suala la usajili wa wachezaji . Kama kwa vikwazo vyote hivyo Andres Villas Boas atafanikiwa kumpa Roman ndoto yake ambayo ni ubingwa wa ulaya atakuwa ameandika ukurasa mpya si tu kwake binafsi kama kocha bali hata kwa makocha wa Chelsea chini ya mrusi Roman Abramovich .
 



1:Alizaliwa tarehe 17, 1977 akiitwa Luis Andre Pina Cabral.Anaongea vizuri kabisa lugha ya kiingereza akiwa amefundishwa vizuri lugha hiyo na babu yake.





2: Ameoa na ana watoto wawili, pia Villas-Boas ametoka katika familia yenye historia ya utajiri.




3:Alianza kucheza soka kama kiungo lakini akagundua kuwa hakuwa na uwezo ulijitosheleza kuwa mchezaji wa kucheza mechi za ushindani, Villas-Boas akaamua kujiunga na uhandishi wa habari za michezo lakini akasitisha mpango huo na kuamua kujiunga na mafunzo ya ukocha kupitia Hayati Sir Bobby Robson, rafiki wa bibi yake.Anelezea: "Kipindi Mr.Robson alipokuja Porto kuwa kocha mwaka 1994 alihamia katika jengo letu. Nilikuwa mdogo lakini kwa sababu nilikuwa napenda soka nilienda kwake kumwelezea matamanio yangu.Alipenda jinsi nilivyokuwa na mapenzi na mchezo wa soka hivyo akanisaidia kuweza kuingia katika mafunzo ya ukocha ndani ya chuo cha Lilleshall, kiukweli nisingeruhusiwa kujiunga pale kwa kuwa sheria zilikuwa haziruhusu vijana wadogo kujiunga na mafunzo. Nilikuwa kocha mdogo kuliko wote pale lakini nilikuwa na nia ya dhati ya kufanikiwa kuwa kocha mzuri."


4: Villas-Boas alikuwa na miaka 21 alipokuwa mkurugenzi wa ufundi wa visiwa vya Virgin nchini Uingereza mwaka 2000, lakini FA walikuwa hawajui.Anasimulia: "Nilikuwa mdogo, lakini hawakutambua.Niliwaambia ukweli kuhusu umri wangu siku ambayo nilikuwa naacha kazi."




5: Kocha Villas-Boas alikuja kuwa kocha msaidizi wa Porto chini ya Jose Mourinho mwaka 2002.Alikuwa ndiye kiongozi wa kitengo cha kuwasoma wapinzani, na baadae wote kwa pamoja na Mourinho wakaamia Chelsea. Mourinho alikuwa akiwaita wasaidizi wake "macho na masikio yake".Alipokuwa Chelsea alipewa jukumu la kuwapa wachezaji DVDs za kuonyesha mchezo wa wapinzani wao kwa kila mechi, akiewalezea wachezaji udhaifu na uimara wa wapinzani wao.

6: Villas-Boas anatajwa kuwa moja ya wasaidizi wa Mourinho waliohusika na ugomvi na Frank Rijkaard mwaka 2005.Andre anasema kuwa alimuona Rijkaard akiongea na refa Frisk kwa mara 3 kipindi cha mapumziko katika mchezo wa kwanza UEFA Champions League february 2005.Mourinho nae alirudia kutoa shutuma hizo za Rijkaard kumshawishi refa kuipendelea Barca hivyo kupelekea kufungiwa kwa Special One katika mechi ya pili dhidi ya Barcelona.





7:Villas-Boas pia alifanya kazi na Mourinho ndani ya Inter Milan, ingawa kwa sasa watu hawa wawili hawaongei kwa sababu ambazo Villas-Boas anazificha lakini anasema: "Tuna itikadi na maono tofauti kuhusu mchezo wa soka.Namuheshimu Mourinho lakini sitaki kufuata mitazamo yake.Nataka kuwa na uhuru wa kufanya kazi nitakavyo bila kujizuia wala kuwa wasiwasi kama anavyofikiria."




8:Villas-Boas aliacha kazi Inter mwezi wa 10, 2009 ili aweze kupata nafasi ya kuwa kocha mkuu kwenye timu ya Academia De Coimbra, iliyokuwa chini ya mkia wa msimamo wa ligi, ikiwa haijashinda mechi yoyote kati ya michezo saba lakini alifanikiwa kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 11 kati ya timu 16 na pia kuingoza kucheza nusu fainali ya kombe la Ureno.Mafanikio haya ndani ya miezi miwili yaliwavutia Sporting Lisbon na wakata kumpa nafasi ya kuwa kocha wao lakini Andre aliamua kurudi Porto.



9: Villas-Boas aliweka rekodi msimu uliopita akiwa Porto, baada ya kuwa ndiyo timu ya kwanza ya bara la ulaya kushinda mara mbili makombe matatu ya kombe la ligi kuu, kombe la FA, na kombe la UEFA cup.Ushindi wa kombe la UEFA cup umemfanya awe kocha umri wa mdogo kuweza kushinda kombe kubwa la barani ulaya.



10: Villas-Boas anapenda kutumia mchezo wa mashambulizi katika mfumo 4-3-3.

KARIBU STAMFORD BRIDGE SPECIAL ONE NO.2
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom