Aweka nyingine kabatini.
N'Golo Kante amepigiwa kura nyingi za kuwa mchezaji bora wa mwaka wa EPL kutoka kwa chama cha waandishi wa habari wa Uingereza.
Kante amejikusanyia kura nyingi kutoka kwa wanachama 340 wa waandishi wa habari wa nchini Uingereza akiwazidi Eden Hazard namba mbili na Dele Alli namba tatu.
Kante ni mchezaji wa tano katika misimu sita kukamilisha tuzo mbili kubwa kwa msimu mmoja baada ya hapo awali kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa kupigiwa kura na wachezaji wenzake.
Kante usajili wa majira ya kiangazi kutoka Leicester atakuwa mchezaji wa kwanza wa ndani ( Sio eneo la Golikipa ) kutwaa mataji mara mbili mfululizo akiwa na vilabu viwili tofauti kama Chelsea wakifanikiwa msimu huu.
Alisema," ni heshima kubwa sana kutwaa tuzo hii. Kukiwa na wachezaji wengi wazuri sana kwenye kikosi cha Chelsea na ligi kwa ujumla kwa chama cha waandishi wa habari kunichagua mimi ni swala la kujivunia sana."
Orodha kamili ya wachezaji waliokuwa wanashindania hii tuzo:-
Sergio Aguero (Man City), Toby Alderweireld (Tottenham), Dele Alli (Tottenham), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Diego Costa (Chelsea),
Philippe Coutinho (Liverpool), Jermain Defoe (Sunderland), Ben Foster (West Brom), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United),
Harry Kane (Tottenham), N'Golo Kante (Chelsea), Anthony Knockaert (Brighton),
David Luiz (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Alexis Sanchez (Arsenal), Gylfi Sigurdsson (Swansea).