Nafatilia kwa karibu jinsi waamuzi wanavyouharibu mpira. Huwezi walaumu sana, njaa sio mchezo. Na Chelseamovic anagawa bahasha zilizotuna.
Ukiangalia rekodi za karibuni, sioni vipi Arsenal atawaweza wanamieleka wa Chelsea. Baada ya mechi na Man United Mourinho domokaya alinukuliwa akiseama plan ya Chelsea haikuwa kucheza mpira wa kushamblia, lakini ku-pack basi na kusubiri mwamuzi avae miwani ili wafanye umafia.
Wenger anataka kuheshimu mpira na kufuata sheria na haonekani kuwa ni mkali/mkemeaji kama Sir Alex, pia hana domokaya kama Mou. Sasa soft, flowing football hailingani na Rugby na mieleka na ukichanganya na umahiri wa uzamiaji(diving) na mtindo wa waamuzi kuvaa miwani kama vile imetokea solar eclipse. BAK na Mbu zake zitaishia wodini tu kwa malaria.
Sipati picha vipi Terry na Ivanovic watakavyomsulubu Ozil. Katika timu nzima ya Arsenal ni Cloroquin (Coquelin) na Flamini ndio kwa mbali wanacheza mafia style ya Chelsea.Arsenal wanaogopa physical contact wakati kwa Chelsea ndio kama mchaga na mbege.
Nafikiri ili mwamuzi kurahisishe kazi ya kuibeba Chelsea atampa Red mchezaji mmoja wa Arsenal.
Nikipata muda nitarudi na uchambuzi wa kina.