Character Never Lies! Utamtambuaje Mtu Mwema au Mbaya?

Character Never Lies! Utamtambuaje Mtu Mwema au Mbaya?

Nashindwa niwekeje ila am innocent kiasi kwamba watu wanatumia kuniadhibu nao ila nikishakugundua biashara inaishia hapo sasa wanageuza kibao kwangu kwamba mm n mtu mbaya but i don't care
 
Nashindwa niwekeje ila am innocent kiasi kwamba watu wanatumia kuniadhibu nao ila nikishakugundua biashara inaishia hapo sasa wanageuza kibao kwangu kwamba mm n mtu mbaya but i don't care
Usijali sana maneno yao kwa sababu
Wewe ndio unaejua zaidi kuhusu wewe sio wao
 
Kwenye hii dunia vitu vingi vimeumbwa viwili viwili: binadamu, wanyama, wadudu

Hata kwenye tabia zipo nzuri na zipo mbaya
Watu wapo wema na wapo wabaya

Hapa sina maana ya muonekano wa mtu, I'm talking about character, kwa sababu tabia yako ndiyo itatuambia wewe ni nani, na tabia yangu ndiyo itawaambia mimi ni nani

Sasa je, tabia za nje zinatosha kumjua mtu kuwa ni mbaya au mwema?

Kwa mtazamo wangu jibu ni ndiyo, ila si mara zote tabia ya nje huonyesha kilichopo ndani

Kuna watu wanaonekana wema sana, lakini ndani wamejaa hila

Na kuna watu wanaonekana wakali au wagumu, lakini ndani wana mioyo safi sana

Lakini ukweli ni kwamba, actions speak louder than words

Mwisho wa siku tutakutambua kwa matendo yako

Sasa ni matendo gani ukiyaona kwa mtu unahitimisha kuwa huyu ni mtu mwema?

Kwangu mimi, mtu mwema nampima kwanza kwa upendo alionao kwa wengine

Mtu mwema mara nyingi habebi chuki wala roho mbaya kwa wengine

Mara nyingi watu wema huwa watulivu wanapoamua mambo, kwa sababu wanaamini wakifanya haraka wanaweza kusababisha matatizo au hasara kwa wengine

Watu wema hujali hisia za wengine Kama hawezi kukusaidia, mara nyingi hayupo tayari kukuumiza au kukupa matatizo

Mtu mwema hufurahia kuona wengine wakifanikiwa

Akiona mwenzake amepiga hatua hasemi
(Kwa nini yeye?)Badala yake anasema, Hongera🤗
Anaamini mafanikio ya mwingine hayapunguzi nafasi yake

Mtu mwema akimkosea mtu huwa yupo tayari kuomba msamaha

Na akikosolewa hasikii vibaya kila wakati, kwa sababu anajua hakuna binadamu mkamilifu

Kwa hiyo ukipata mtu wa aina hii kwenye maisha yako, usimchukulie poa

Watu wema ni wachache kuliko tunavyofikiri

Mara nyingi huwa ndiyo watu wanaokupa amani ya moyo wanakushauri kwa faida yako hata kama ukweli unauma wanakuombea mema hata ukiwa haupo nao, na wanabaki upande wako hata pale ambapo hawapati faida yoyote kutoka kwako

Ukiwa na mtu mwema karibu yako, mara nyingi unajikuta hata wewe unabadilika na kuwa mtu bora zaidi Positive people create positive lives
👇

Sasa twende kwa mtu mbaya...

Mtu mbaya mara nyingi hubeba chuki dhidi ya wengine

Moyo wake huwa kama umekufa ganzi, hana anachojali kuhusu wengine

Hata kama hana cha kukusaidia, atafanya juu chini akupe maumivu

Mtu mbaya marafiki zake ni unafiki, uchonganishi, umbeya, ubinafsi, chuki na husda

Mtu mbaya hataki kuona wenzake wakifanya vizuri

Anataka yeye ndiye awe top kwenye kila kitu

Akiona wenzie wanasifiwa, roho inamnyonga akiamini hawastahili

Hufurahia maanguko ya watu

Yule alikuwa anajidai, sasa amekuwa kama sisi kiko wapi🤣

Mtu mbaya hubeba chuki ambayo mwisho wa siku hummaliza yeye mwenyewe kidogo kidogo

Lakini pia ni hatari kua karibu yake maana chuki aliyoificha ndani akiitoa njee ni majanga

Anaweza kutabasamu mbele yako, lakini ndani anateseka kwa sababu tu huwezi kuanguka kama anavyotamani

Na kitu kingine nilichokiona, mtu mbaya huwa ni mgumu sana kufurahia mafanikio ya wengine

Kila zuri analigeuza baya kila mafanikio anaona kuna mchezo umefanyika utasikia
(hapa si bure kuna kitu)

Shida ya kuwa karibu na mtu wa aina hii ni kwamba taratibu utaanza kupoteza amani yako bila kujua

Atakuvuruga kisaikolojia, atakufanya uwaone wengine wabaya kama yeye, atakukatisha tamaa kila unapopiga hatua na wakati mwingine anaweza kuwa sababu ya wewe kuharibu mahusiano yako na watu wasiokuwa na kosa

Watu wabaya hua pia wanapenda wakikosana na watu na wewe eti ukosane nao pia hua wanapenda kurithisha uadui🤣🤣

Watu wa aina hii wakishindwa kukutumia, wanaanza kukuchafua Ndiyo maana kuna msemo unasema, show me your friends and I'll tell you who you are

Mara nyingi tabia huambukiza, hivyo ukikaa sana na mtu mwenye roho mbaya bila kuwa makini, unaweza kujikuta unaanza kufanana naye bila hata kugundua

Sasa hapo tumeona baadhi ya tabia za watu wema na watu wabaya na huo ni mtazamo wangu


Wewe ongezea...

Ni tabia gani ukiiona kwa mtu unaamini kabisa huyu ni mtu mwema?

Na ni tabia gani ukiiona unaona huyu ana roho mbaya?

Halafu ukijipima wewe mwenyewe, kwa tabia zako za ndani na nje unajiona upo upande gani?

Happy Tuesday 😊
ShesRise_1 ✋️
Moja ya mbinu zangu ni kumpa mda na kumtengenezea muhusika mazingira ya kuwa confortable ili tabia zake halisi zitoke
 
Back
Top Bottom