NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,520
- 17,426
Binafsi napinga kauli ya makamu wa Rais kuhusu chanzo cha saratani kanda ya ziwa kuwa maji ya maiti yenye chloroform.
Ni heavy metals pekee kama mercury, lead, zinc na nyinginezo ambazo zinaweza kukaa kwa muda mrefu kwenye maji na ardhini hadi kuyeyuka kwenye maji na kudhuru watumiaji wa maji hayo.
Kuhusu formaline na chloroform hizo ni volatile in nature, haziwezi kuishi kwa muda mrefu hewani kwenye joto la kawaida hadi kumfikia mlaji. Yaani huyeyuka kutokana na joto na kuwa gesi hivyo haziwezi kuishi kwenye kiumbe kwa muda mrefu na kusababisha madhara makubwa kiasi hicho.
Kauli ya Makamu ni ya kisiasa wala siyo ya kikemia. Ni kawaida kwa wanasiasa wetu kuleta taharuki kwenye jamii kwa malengo fulani.
Najua kauli hiyo imelenga kuua uchumi wa samaki na kuwabeba wawekezaji wa migodi nchini, kama ile kamati iliyokuja na majibu ya kizembe. Eti kinyesi cha ng'ombe na mkojo ndiyo vilivyosababisha maji ya Mto Mara kuchafuka! Kamati ile na majibu yake ni muendelezo wa siasa chafu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa dhidi ya wamiliki wa migodi wa kanda ile.
Hatujui kauli ya Makamu wa Rais inaspin kitu gani hasa wakati huu wa maumivu ya Tozo, lakini sisi kama wasomi wa kemia hatuwezi kukubali taaluma yetu kudharaulika kisiasa!