Changamoto za barabarani usiku mkubwa

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Hii picha inasambaa kwenye magroup ya madereva. Kuna dereva mmoja kakutana na hii kitu akiwa safarini.

Mimi kuna siku natoka Tunduma kuja Mbeya nipo kwenye costa siti ya mbele SAA sita mchana jua Kali ghafla kwenye pori kaibuka mtoto miaka 5-7 kakatisha barabara dereva akamkwepa tukayumba sana ila hatukupinduka. Swali la abiria yale maeneo hakuna nyumba hata ya nyasi mtoto anatokea wapi?

Kila mtu akaanza kuomba dua yake.

FB_IMG_16208017420302513.jpg
 
Muda mwingine ni walevi tuu au vichaa wanakuwa wanaranda randa wamekosa uelekeo..hiyo picha naona kuna mataa kwa mbali na huyo dada ni albino ndo imetisha sana inaezekana ni mkazi wa huko amepotea kwa sababu za ulevi..ingawa usiku kweli mambo ya ajabu hutokea.

Mimi nilishapita sehemu usiku wa mbalamwezi nikaona watu wanalima wako uchi kabisa na ni wengi.

Ule upepo wao ukanipata niliugua karibu mwezi.
 
Watanzania wengi mnaamini Sana ushirikina. Ukiangalia comments hapa utajua tulivyo na upeo mdogo.

Tutambue Tanzania tunaruhusiwa kutembea muda wowote usiku na mchana, hivyo kumkuta mtu usiku njiani Wala sio kitu Cha ajabu kukufanya umgonge.

Pili Tanzania sera yetu ya kutunza wagonjwa wa akili ni mbovu Sana. Kuna kichaa anatembea eneo la hifadhi ya mikumi Sasa ukikutana nae utasema ni msukule, kumbe kichaa tu. Hivyo hivyo na vichaa sehemu zingine za nchi.

Tatu Kuna watu wanafukuzwa kwa Ndugu zao usiku wanaamua kufanya maamuzi magumu kwenda kwa Ndugu zao kwengineko tukiwakuta tunataka kuwagonga eti wanga.

Mwisho Kuna walevi ambao wkaiwa wanatembea usiku kwenye Giza linapotokea gari ule Mwanga unawasumbua na kuwafanya waweweseke, tunataka kuwagonga eti ni wanga.

By the way wanga huwezi waona, wakitaka kukumaliza watakuja Kama punda, fisi, Ngombe etc ukiwagonga shida, ukiwakwepa shida
 
unaweza kufukia kumbe ni raia mwema tuu ukalichafua gari kwa mafi
Dar Bagamoyo saa 8 usiku unakutana na mwanamke kavaa baibui jeusi peke yake katikati ya barabara unamfanyaje huyo? kadri unavyokaribia anasogea kurudi nyuma, sisimami.
Ndg yangu alikutana na hiyo kadhia, alichofanya akazima taa na kuwasha huku akiwa speed 110 hakuna kitu, uliza madereva wanasafirisha magazeti wakupe hadithi zao, hasimami mtu iwe mbuzi au mtu, mwisho wake unakuta hujagonga chochote ni vibweka vya njiani
 
Watanzania wengi mnaamini Sana ushirikina. Ukiangalia comments hapa utajua tulivyo na upeo mdogo.

Tutambue Tanzania tunaruhusiwa kutembea muda wowote usiku na mchana, hivyo kumkuta mtu usiku njiani Wala sio kitu Cha ajabu kukufanya umgonge.

Pili Tanzania sera yetu ya kutunza wagonjwa wa akili ni mbovu Sana. Kuna kichaa anatembea eneo la hifadhi ya mikumi Sasa ukikutana nae utasema ni msukule, kumbe kichaa tu. Hivyo hivyo na vichaa sehemu zingine za nchi.

Tatu Kuna watu wanafukuzwa kwa Ndugu zao usiku wanaamua kufanya maamuzi magumu kwenda kwa Ndugu zao kwengineko tukiwakuta tunataka kuwagonga eti wanga.

Mwisho Kuna walevi ambao wkaiwa wanatembea usiku kwenye Giza linapotokea gari ule Mwanga unawasumbua na kuwafanya waweweseke, tunataka kuwagonga eti ni wanga.

By the way wanga huwezi waona, wakitaka kukumaliza watakuja Kama punda, fisi, Ngombe etc ukiwagonga shida, ukiwakwepa shida
Kichaa anavaa baibui usiku au shuka nyeupe? tembea uone au uliza wa wasafirishaji wa magazeti
 
Kichaa anavaa baibui usiku au shuka nyeupe? tembea uone au uliza wa wasafirishaji wa magazeti
Mimi nimetembea nchi nzima usiku nafahamu ninayoongea, sio story za kusadikika Kama unachotaka kusema.

Lakini pia tambua tamaduni za watu na makabila mbalimbali. Mfano ukipita kondoa, babati, Singida yote igunga. Unategemea kukuta watu wenye mavazi gani? Iwe usiku au mchana.

Macho yako usiku unaweza kuyaaminisha yaone like ambacho sio sahihi kwa hisia tu.

Naendesha gari usiku Mara nyingi zaidi ya mchana nafahamu. Kama sio muoga ukiona unachohisi umeona simama, ongea nae badala ya kugonga.

Kwa taarifa yako usizoee kugonga chochote uwapo safari I, hata Kama ni paka, sungura, nyoka etc.
 
Kuna jamaa yangu ilimkuta hii akielekea Mikumi kutokea Iringa,alitokea mtu mbele akiwa kwenye speed kama 150kph usiku mkubwa,akihama upande wake na yule mtu anahama upande alikoendea,akili ya haraka ilikuwa ni kumgonga,anasema alisikia mshindo na akapita juu kwenye kioo cha mbele,hakusimama mpaka alipofika Mikumi akachukua Lodge,asubuhi akakagua gari yake hakukuta alama ya kugongwa wala damu,alipofika Dar aliuza ile gari maana alijua hayuko salama tena...
 
Back
Top Bottom