Baadhi ya changamoto za madereva barabarani

Kelela

Senior Member
Nov 7, 2020
186
269
Ni takribani miezi 10 sasa tangu nianze kuendesha chombo cha moto (pikipiki), Ingawa sina route ndefu kwani maximum route zangu ni kilometa 40 au chini ya hapo.

Kwa kipindi hicho cha miezi kumi nimeona baadhi ya makosa haya ambayo ni hatarishi na yanaweza kusababisha ajali:

1. Dereva wa pikipiki kutowasha taa usiku wakati pikipiki ina taa, yaani hadi ukimkaribia ndio anawasha taa.

2. Ku-overtake kwa anaye-vertake: Yaani unakuta mtu unaovertake gari muda huohuo na yeye anakuovertake wewe kwa hiyo inakuwa barabara yote mumeijaza kwa wakati mmoja.

3. Dereva wa daladala wanafunga breki za papo kwa hapo wakiona abiria bila tahadhari yoyote (sio wote ni baadhi).

4. Dereva kutotumia taa za ishara (indicators) anapotaka kupaki au kukunja kona, na wengi huwa wanawasha taa za ishara kwa kuchelewam, yaani mpaka amefika kwenye kona husika ndio anawasha taa.

5. Dereva wa pikipiki kuovertake magari bila kujua mbele kuna nini (Hii ni hatari sana hasa katika mwendo mkali).

6. Kutofuata taa za kuongozea vyombo vya moto barabarani (traffic light), hasa madereva pikipiki wengi wanaona kama taa haziwahusu wao.

NB: Nimeorodhesha makosa hayo sio kwa lengo la kumlaumu mtu yeyote bali ili tuchukue tahadhari na tuyaache makosa hayo hatarishi kwa ajili ya usalama wetu.
 
Ni ukweli unachokisema, matrafki wameamua kupambana na wenye magari na kuwaacha madereva pikipiki kwa sababu wanajua hawana pesa ya kiwi.

Ajali nyingi za boda boda zinasababishwa na kutokua na ufahamu wa sheria za barabarani pamoja na utumiaji wa "visungura".

Refer yanayotokea Arusha.
 
Back
Top Bottom