gspain
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,892
- 5,946
Habari zenu wadau.
Kuna tatizo limeikuta akaunti yangu, kila ninapoapply ninapata automated answer ambayo inanionyesha siendani na academic qualification za hiyo ajira.
Ila tatizo ni kwamba niliwahi apply kwa post kama hiyo na nikaitwa hata kwenye interview ila katika post hii ndiyo napata hilo jibu.
Post ninayojaribu kuiomba ipo kwenye category ya Sociology, Political Science and Community Development. Nimehuisha taarifa via National Identification Number nimeweka kozi yangu katika category husika lakini bado napata hiyo feedback.
Nimejaribu kuwapigia kwa namba zao za help desk na malalamiko ila hazipatikani tangu Ijumaa, na nipo mbali na mkoa wa Dar so nashindwa kwenda ofisini kwao. Last resort nimeamua kuja kuomba msaada humu kwa yeyote anayeweza kunisaidia.
Natanguliza shukrani.
Sijawahi kuaccess hiyo portal ila kwa maelezo uliyotoa na kwa kuzingatia jinsi automated web based application zinavyokuwa coded, inawezekana moja kati ya haya ni sahihi;
1. System imekuwa instructed kureject yeyote aliyewahi kuomba previously on the same field na kufikia level flan ya mchakato (hapa nita assume level ya kuitwa kwenye interview) kutokana na maelezo yako hapo juu.
2. Inawezekana nafasi iko ristricted kwa watu wa kozi fulani kutoka vyuo fulani tu lakini haijawekwa wazi, mfano kuna baadhi ya matangazo wanaweza kutoa umuhimu kwa watu waliosoma kozi husika lakini kutoka vyuo fulani kulingana na units flan flan zilizo kwenye mtaala wa vyuo hivyo.
3. Network problems ambazo mara nyingi hutokana na data traffics kuuelemea mfumo husika.
4. Uzembe ama kutokuwa na uelewa wa kutosha kwa aliyekuwa anacode "error messages" hivyo kufanya system itoe the same error message kwa different problems, mfano chukulia unatuma hela kwa mobile then ukiwa huna salio la kutosha, umekosea namba, umekosea PIN nk inakupa error message moja hivyo inakufanya ushindwe kubaini tatizo husika.