Hebu tuzijadili changamoto wanazopambana nazo waombaji wa ajira kupitia Recruitment Portal

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,661
18,035
Ama kwa kweli kila hatua ina changamoto zake, japo makali ya hizo changamoto yanaweza kutofautiana!!
1. Changamoto moto kwenye hatua ya application:
*Mtandao kusumbua wakati deadline ya application imekaribia
*Application kugoma kwenda kwa kigezo kuwa huna sifa, wakati sifa zako ni hizo hizo zinazotakiwa
kwa hiyo nafasi. Mfumo unakuletea meseji ifuatayo:

Job Application FAILED​

Sorry! You can not apply for the job post, kindly Check Academic Programmes Qualifications Requirements for the Job Post

Please read and understand carefuly Job post qualification requirements before applying

Thank You.
*Kusubiri kwa muda mrefu ukiwa kwenye "received" status kabla ya kuitwa kwenye written interview wakati waombaji wa nafasi zingine wakitwa mara kwa mara kwenye usaili.

2. Changamoto kwenye hatua ya written interview:
*Kuitwa kwenye written interview lakini huna pesa ya nauli, malazi na chakula za kukuwezesha kuhudhuria usaili huo! Kwa mfano uko mwanza lakini unatakiwa uhudhurie usaili Dodoma au Dar!
  • kusubiria matokeo ya written interview hadi usiku wa manane!
  • Kuitwa kwenye usaili lakini haujui uanzie wapi kujiandaa kwa maana ya eneo husika ambalo maswali yanaweza kutoka, nk

3. Changamoto kwenye hatua ya oral interview:
  • Kusubiria tarehe ya oral interview wakati pesa imekuishia lakini unatakiwa usubiri pengine siku moja zaidi baada ya writtewn interview!
  • Kutokuwa na uzoefu kabisa kwenye oral interview!

4. Changamoto kwenye hatua ya placent!!
* Kusubiri placement wakati hujui hata ulipata marks ngapi kwenye oral exam!!
*Kusubiri placement wakati hujui kama ulifaulu au ulifeli oral interview maana huwa hawatoi matokeo!
  • Kusubiri kwa muda mrefu utokaji wa pdf maana ndio njia pekee ya kujua kama ulifaulu au vinginevyo!
  • Kusubiri placement kutoka kwenye data base japo huna uhakika kama kweli jina lako liko kwenye data base maana data base hiyo haijawahi kuwekwa wazi!!

5. Changamoto baada ya kulamba asali (kuitwa kazini) na jina lako kutokea kwenye pdf
* Kuamua je uifuate barua yako dodoma au usubiri baada ya wiki moja barua itumwe kwenye anwani yako ulioweka kwenye akaunti yako ? Upande mmoja unasema niifuate lakini tatizo ni nauli!! Upande mmoja unasema watanitumia lakini ikiwa misplaced na siku 14 zikapita itakuwaje? Wengi (karibu wote) huamua kufuata barua zao dodoma hata kama itabidi wakope pesa kwa riba!!

6. Changamoto baada ya kuripoti kituo cha kazi alichopangiwa:
* Kijana anaripoti akiwa na vyeti vyote original vinaangaliwa, anajaza form za taarifa binafsi nk. Kisha anaambiwa rudi nyumbani hadi tutakapokuita kwa simu!! Hapo kijana hata pesa ya kujikimu kwa siku moja tu hana na nauli nyenyewe alikopa!!, hana mwenyeji ambapo anaweza kujibanza wakati anasubiria huo wito kwa simu!! Afisa utumishi hapo keshamalizana na wewe na kukutaka umpishe ofisini ili mtu mwingine anayetaka huduma yake aingie!! Hakuna cha posho wala baba yake na posho! Kwa vijana wa kiume, wengine wanakomaa tu na kulala stendi za mabasi nk. Kwa mabinti sitaki kuwaza wanafanyaje maana kwao ni risk kubwa sana! Kuna baadhi ya waajiriwa wapya wanasubiria hadi mwezi mpaka kuitwa, wengine wiki moja, wengine wiki mbili na hakuna formula! Mimi naona hii ni changamoto kubwa zaidi japo matumaini ya uhakika yanawabeba kiasi fulani!

7. Changamoto baada ya kupigiwa simu na kutakiwa kuripoti kuanza utumishi wao!
  • Wengi hawajui hata haki na stahiki zao!!​
  • Changamoto ya kupata mahali pa kuishi (kwa baadhi ya sehemu), hapo watalazimika kuingia kwenye 18 za madalali. Baadaye kero ya mama mwenye nyumba na kero ya wapangaji wenzao!!​
  • Mwisho wa siku ni changamoto ya kuona mshahara hautoshi, ni mdogo sana hasa baada ya makato ya bodi ya mikopo kuanza!!​

Inabidi watu wajue tu kuwa, changamoto katika maisha huwa haziishi japo makali ya changamoto hutofautiana. Je wewe uko kwenye changamoto ya hatua ipi?. Changamoto ni sehemu ya maisha ya kila mwanadamu. Usikatishwe tamaa na changamoto ulizo nazo, bali changamoto hizo zikusaidie kutafuta namna ya kukabiliana nazo!! Historia ya binadamu inaonesha kwamba maendeleo makubwa yaliyopo duniani leo, ni matokeo ya majibu ya changamoto ambazo mwanadamu alikabiliana nazo.

Yawezekana kuna watu wanaosaka asali kwa udi na uvumba leo hawatapata kabisa placement! Na watajiona kama watu wenye bahati mbaya sana, na pengine kuona kama vile walipoteza tu muda kusoma hadi chuo!! Lakini baadhi ya watu hao hao ambao watakubali jukumu lao la kupambana na changamoto zao zilizopo leo, miaka kumi hadi ishirini ijayo WATASHUKURU SANA kwa kutokupata placement!! Maana hiyo ilipelekea watoboe sehemu nyingine ambayo asali yake si ya kulamba tu bali ya kunywa kwa kujimiminia, na kulambisha wengine(watakuwa waajiri)!! Wngine watakuwa wafanya biashara wakubwa, wengine watakuwa wakulima wakubwa, wengine watamiliki viwanda nk. Cha msingi usikate tamaa na ulikubali jukumu la kupambana na changamoto zako!! USIKUBALI KULAUMU WENGINE KWA CHANGAMOTO UNAZOKUTANA NAZO, HATA KAMA KUNA KILA DALILI YA KUHUSIKA KWAO KWENYE CHANGAMOTO ZAKO. KULAUMU WENGINE HULEMAZA UWEZO WAKO WA KUJIPAMBANIA.

Mungu ni mwenye haki, watakaolamba asali wamshukuru Mungu, na watakaokosa kwa sasa wamshukuru Mungu pia maana kwa hakika watakuwa wameandaliwa yamkini mahali pazuri zaidi.


Lakini kitu kibaya zaidi ni kwamba yawezekana kuna watu pia ambao hawatapata asali wanayoisubiria kwa hamu, na mbaya zaidi ni kwamba, badala ya kukubali kupambana na changamoto zao, watabaki wakilaumu wengine. Hata kama wale wengine wanastahili kabisa kulaumiwa, lakini kulaumu hakujawahi kuwa na mchango wowote katika kutatua changomoto zinazomkabili mtu!. Kijana wa kiume pambana, NINAKUAMINIA!!, kijana wa kike PAMBANA, acha kulia lia NINAKUAMINIA pia, wala usijirahisishe!! Amini kwa moyo wako wote kuwa KUTOBOA NI LAZIMA, NI SUALA LA MUDA TU!!​
NAWATAKIA MAFANIKIO WOTE

 
Vyeti viwe verified.

Majina ya vyeti yasiwe na dosari.

Before interview soma kweli kweli, omba even material from friends.

Siku ya oral vaa vizuri
Tuwe wakweli!! inahitaji mwezi mzima kuverify vyeti vya mtu? Kwa nini vyeti visiwe verified kwa waombaji wote wa ajira kabla ya kuwaita kwenye usaili?? Kwa nini umfanyie usaili mtu ambaye bado una cwasi wasi na uhalali wa vyeti vyake? Mbona kati ya application na call for interview hupita hadi miezi kadhaa, kwa nini wasitumie muda huo kuverify vyeti? Watanzania wanapenda sana kusumbua wenzao kwa kisingizio cha vitu visivyokuwa na sababu ya msingi!! Huu ushauri mwingine uliotoa ni SAFI SANA!!
 
Kijana usiende kwenye usaili na mindevu lukuki, watu watakuogopa kwa kufanana na desturi za magaidi!! Usivalie chochote kinachotabulisha dini au kabila lako!
 
Back
Top Bottom