Kama umeomba na una vigezo unachaguliwa kwenda kwenye written interview. Kutoka hapo waliofaulu watakwenda oral interview.
 
Habari,

Ningependa kujuwa majibu ya Maswali yafuatayo ambayo yatakuwa msaada kwangu na watu wengine wenye kujiuliza.

1. Kama tangazo la kazi na maelezo yake yameandikwa kiswahili mfano AFISA MTENDAJI na sifa zake ni lazima niandike Cover letter na CV kwa kiswahili?

2. Je Barua yangu namuandikia nani? Mwajiri au Mwajiri kupitia UTUMISHI.

3. Je kuna masharti mengine madogo yanwaweza kuni COST nisiitwe kwenye INTERVIEW?

Mbarikiwe sana.
 
Sio lazima CV, ibadilike. Katika matangazo ya kiswahili mi huandika barua ya kiswahili basi. Ila CV inabaki vile vile. Pia zingatia utumishi unapoomba kazi unaattach tu barua cuz vingine unakuwa ushaviambatanisha ulipokuwa unajisajili.

Kazi kama za Afisa Mtendaji mara nyingi maombi yake yanatumwa moja kwa moja kwa wakurugenzi wa eneo/wilaya/mkoa husika tena kwa njia ya posta. So sioni kama kuna sababu ya kuweka anwani ya Karibu, utumishi wa umma. Zingatia sana address ya tangazo husika na namna ya kutuma.

Masharti sasa hapo, inategemeana na wao wanaonaje. Ila angalia sana Job specifications onesha kwenye barua yako namna ambavyo unaweza au ulivyofit kwenye job specifications na ukidokeza dokeza utakavyofit kwenye job descriptions. Usisahau kuonesha tangazo umelitoa wapi, mfano ukamwekea link ya tangazo. Atakuona kijana uko updated sana. Panga vizuri huo mtiririko. CV yako iendane na wanavyotaka. Sidhani kama kutakuwa na kipingamizi.

Sent from my Infinix Zero 4 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sio lazima CV, ibadilike. Katika matangazo ya kiswahili mi huandika barua ya kiswahili basi. Ila CV inabaki vile vile. Pia zingatia utumishi unapoomba kazi unaattach tu barua cuz vingine unakuwa ushaviambatanisha ulipokuwa unajisajili.

Kazi kama za Afisa Mtendaji mara nyingi maombi yake yanatumwa moja kwa moja kwa wakurugenzi wa eneo/wilaya/mkoa husika tena kwa njia ya posta. So sioni kama kuna sababu ya kuweka anwani ya Karibu, utumishi wa umma. Zingatia sana address ya tangazo husika na namna ya kutuma.

Sent from my Infinix Zero 4 Plus using JamiiForums mobile app
Ahsante sana mkubwa.
 
Jamani kila nikieka namba ya nida naletewa ivo shida nini?

Screenshot_20200718-171002.jpg
 
Hicho unachokifanya hakiwezekani mkuu kwa mtazamo wangu umeshafungua acc na uki fill up ma qualifications yako mpaka labda degree uka test kufuta baadhi ya academic qualifications imegoma ivo uka create acc ingine hapo huwezi ku verify kwa nida tena
 
Moja ya vitu kiukwel vinaniumiza sana n mfumo mbovu wa kutuma maombi ya kazi unaotumiwa na taasisi nyingi kwa sasa unaoitwa @ajiraportal yani una mambo mengi halafu ambayo hayana msingi

Binafsi naomba wamiliki waangalie jinsi ya kuboresha huu mfumo maana ni mbovu sana na unachukua muda mwingi sana
 
Mimi mbona naona ndio wameturahisishia wengine sio kama zamani lazima uende posta kila Mara na kutafuta mwanasheria, saiv ukishaattach vinakuwa pale miaka na miaka we unakuwa unaupload barua tu kulingana na kazi iliyotangazwa
 
Mimi nilikosea kwny ku_upload cheti cha chuo nika upload mara tatu so nimejaribu kudelete vyeti viwili ili kibaki kimoja nmeshindwa, please msaada!
 
Mimi nilikosea kwny ku_upload cheti cha chuo nika upload mara tatu so nimejaribu kudelete vyeti viwili ili kibaki kimoja nmeshindwa, please msaada!
Yaani hili tatizo ni la wengi aiseee kiukweli hii system inawaumiza weng aisee
 
Anazungumzia kwa mtu aliyepitia diploma anaweza kuondoa cheti cha degree akaacha cha diploma.

Sent using Jamii Forums mobile app
mfumo wa sasa haukubali kudelete cheti ,kama uliweka cheti hautakuta option ya kudelete utakuta option ya kuedit tu hivyo hauezi kukiondoa.

Cha kushangaza transcript unaweza kudelete,najiuliza endapo mtu akakosea na kuweka cheti mara mbili kimakosa hataweza kukidelete kimoja sababu mfumo hauruhusu kudelete,sasa nini maana kua na mfumo
 
waungwana habari za asubui, natumai wazima wa afya. Ninaitaji kujaza cheti cha basic driving course kwenye system ya ajira portal sasa sehemu ya educational level nikiweka cerficate na institutional name najaza other alafu sehemu ya kuattach cheti naattach kama kawaida sasa kimbembe kinakuja kwenye kujaza programme category hakuna option ya kuchagua upande wa basic driving certificate mana nimejaribu kujaza transport and logistics hainipi option yoyote yakuendana na mambo ya udereva.

Pia niliwapigia utumishi wakaniambia niattach cheti cha awali cha mafunzo ya udereva yaani basic certificate kwenye academic qualifications hili neno la failed lisitokee kwa maana kabla nikiapply kazi ya udereva ilikuwa inaandika failed. basi wadau kama kuna mtu yeyote mwenye uelewa wa hii inshu anisaidie hili nijaze nitume mana mwisho ni kesho.
 
Attach kwanza cheti chako cha form four. Kama tayari nenda kwenye "Professional Qualification s" Add pale. Kuna board mbali mbali zinahusika na professions kama ERB, kama we ni dereva manake utatafuta NIT au VETA zipo pale.

Na ukija kwenye course name utachagua driving license au professional driving kulingana na cheti chako. Utaweka mwaka wako ulioanza na mwaka uliomaliza, utaambatanisha cheti chako. Then utasave. Utakuwa umemaliza.

NOTE : Database au Kanzidata ni habari nyingine, so kwenye title yako nahisi umeitumia kimakosa (Kwa maoni yangu).
 
Attach kwanza cheti chako cha form four. Kama tayari nenda kwenye "Professional Qualification s" Add pale. Kuna board mbali mbali zinahusika na professions kama ERB, kama we ni dereva manake utatafuta NIT au VETA zipo pale...
Ok mkuu nimekupata, ila kuna mtu alimjazia kimakosa mara ya kwanza nadhani alikosea mana muhusika sio mimi ni jirani yangu alinifata niweze kumsaidia sasa nilijaribu kujaza kwenye academic qualifications option za kuweka hicho cheti cha awali hakuna sasa mkuu sijui itakuwaje na kesho ni mwisho wa kutuma maombi
 
ok mkuu nimekupata, ila kuna mtu alimjazia kimakosa mara ya kwanza nadhani alikosea mana muhusika sio mimi ni jirani yangu alinifata niweze kumsaidia sasa nilijaribu kujaza kwenye academic qualifications option za kuweka hicho cheti cha awali hakuna sasa mkuu sijui itakuwaje na kesho ni mwisho wa kutuma maombi
Kuna 1. Academic qualifications, 2. Professional qualifications, 3. Working and Training Experience. Hapo ni vitu kama vinaendana ila ni tofauti.

Kwenye udereva sehemu yake ni hiyo Professional qualifications. Hapo ndo utakuta maelezo na ukiweka gamba linakubali mkuu.
 
Back
Top Bottom