Graduate gani wewe unakosa hata hoja za msingi ivi Nida number zingekuwa zinawekwa tu bila kuverify kuwa huyu ni mhusika unadhani ni namba ngapi zingetumika ovyo? Unapokuwa na kichwa kibovu cha kushindwa walau kujua details ulizo jaza nida wakati unajiandikisha uko kazini unataka ukafanye nini? Kwangu mfumo wa Ajira portal una ufanisi wa zaidi ya 90% sote tunajua hapo awali kwenye taasisi nyingi kama huna mtu wa kukushika mkono ilikuwa mbinde kupata ila kwa sasa ni bidii zako nawafahamu zaidi ya watu 5 wanufaika na huu mfumo bila kuwa na uncle wala baba mdogo na wamelamba ajira sehemu sensitive
Wewe kama ulikuwa unacheza chuo kwa kutegemea ukimaliza ushikwe mkono na mjomba na upate ajira ndio imekula kwako sasa pambana na wenzako
 
Bora huo mfumo wa ajira portal uendelee tu, muhimu ni kuboresha changamoto zilizopo katika mfumo huo, tukirudi kwenye mfumo wa zamani ni mbaya sana hasa; Ukanda wa kuajiri utaendelea kwa kanda husika, Undugu utaendelea kuwepo kwenye ajira. Tushukuru uwepo wa huu mfumo.
 
Mfumo wa ajira portal ni mzuri sanaa, kwa kweli umesaidia wengi kupata ajira,ilaa kwa ajira za vyuo naona bado usaili unafanyikia chuoni huku kuna ukiritimba mwingi sanaa ,hasa chuo kimoja kipo mkoa wa kati ajira zake ni za kujuana sanaa
 
Dah yani mfumo umekua mbovu sometimes uko apply inadai haujaqualify

Hii kitu wangeondoa, dogo kashindwa kuapply na alikuwa na the same qualification ila akitaka kuapply inamkatalia inamwambia haja-qualify!

Simu hazipatikani na zinazopatikana hawapokei, katuma email kulalamika hakuna aliyejibu basi majanga tupu huu mfumo wangeondoa tu! Ni kero tupu
 
Mimi nauluza, ajira portal inataka uweke namba ya NIDA na kama inavyofahamika si wote wenye hizo namba kwa nini hawajaweka alternative ya hiyo namba mfano barua kutoka serikali za mtaa nk
 
Mkuu ..wanafanya hivyo kwa faida yako mwenyewe ili kuzibiti ujanja ujanja wa kutumia vitambulisho vya watu
 
Ipo category inayosema OTHERS so nime pick iyo others nikaweka driving licence nikaatach na chet changu cha mtaani .

Swali langu ni kuwa je kwa kuchagua iyo driving licence natakiwa niweke licence au cheti?

Pili je hii profesional si itanitambulisha kama driver? wakat mm profesional yangu ni transport officer
Watu wa VETA na NIT wanapewa kipaumbele zaidi na waajiri (sio wote lakini asilimia kubwa) kuliko wa vyuo vingine. Kwa serikali, hiyo ni sawa na mama na baba.

Mfano mzuri ni pale unaumwa unampelekea mwajiri medical certificate ambayo imetoka hospital ambayo ye haitambui. So ni ngumu.
 
Mnaturudisha Zama za zamani. Ulimwengu upo Kwenye Mapinduzi ya Viwanda Awamu ya 4 (Fourth Industrial Revolution-4IR) nyie mmeng'ang'ana na Makaratasi na P. O Box tu
Tanzania digital world bado hatujafikia uwezo wa kui run...wee chunguza sehemu nyingi hata tra unaenda lipa kodi unaambiwa huduma hakuna myandaonupo chini!...haya hao nida hadi leo wameshindwa kukamilisha zoezi la vitambulisho!..mwendo kasi dar ilikua mwanzo una punch ticket ktk mageti yale,kulikua na ku swaap carf vyote vimefeli....ni kwamba tunaipenda modern digital tech lkn nchi bado hatujafika huko
 
  • Thanks
Reactions: amu
Ukisema Tassisi ziajiri Kama zamani,
Kama Huna Ndugu kwenye Tasisi inayoajiri,kilio chake ni Mara 1000 ya unayodhani ni mapungufu ya system
Bora vile kwa maana hata kama hela ya chai utatoa lkn kitaeleweka,ni afadhali mbona humu mabarabarani tunawapatia wajomba hela kidogo ya chai wanakuacha unaenda zako?
 
Graduate gani wewe unakosa hata hoja za msingi ivi Nida number zingekuwa zinawekwa tu bila kuverify kuwa huyu ni mhusika unadhani ni namba ngapi zingetumika ovyo? Unapokuwa na kichwa kibovu cha kushindwa walau kujua details ulizo jaza nida wakati unajiandikisha uko kazini unataka ukafanye nini? Kwangu mfumo wa Ajira portal una ufanisi wa zaidi ya 90% sote tunajua hapo awali kwenye taasisi nyingi kama huna mtu wa kukushika mkono ilikuwa mbinde kupata ila kwa sasa ni bidii zako nawafahamu zaidi ya watu 5 wanufaika na huu mfumo bila kuwa na uncle wala baba mdogo na wamelamba ajira sehemu sensitive
Wewe kama ulikuwa unacheza chuo kwa kutegemea ukimaliza ushikwe mkono na mjomba na upate ajira ndio imekula kwako sasa pambana na wenzako
Verification mara ngapi?serikali umenihakiki na kuridhika ukanipatia card kama kithibitisho kupitia taasisi maalum ya Nida leo hii naombabajira sehemu serikali hiyo hiyo kupitia taasisi nyingine wanashindwa kuamini uraia wangu!mambo ya ajabu sana
 
Back
Top Bottom