SoC02 Changamoto ni fursa; Uchafu ni fursa kwa kuzalisha umeme, gesi ya kupikia, vilainishi pamoja na mbolea yenye virutubisho

Stories of Change - 2022 Competition

LAETUS

Member
Jul 24, 2022
43
73
Uchafu ni kitu chochote ambacho hakina matumizi kwenye mazingira; mfano chupa zilizoishiwa matumizi, karatasi, makapi ya mazao mbalimbali,majani ya matunda, mabaki ya vyakula na vinginevyo. Kwa hiyo kutokana na uchafu, mazingira yanakua sio safi na salama kwa viumbe hai ndani yake.

Asilimia 37% ya watanzania hawajafikiwa na nishati ya umeme ,hasa wale wanaoishi vijijini ,lakini pia ,asilimia zaidi ya 61% ya watanzania wanatumia kuni na mkaa ,kama vyanzo vyao vya nishati ya kupikia.

Tanzania na Afrika kwa ujumla ,inapitia tatizo la ongezeko la bei ya petroli,na vilainishi hasa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri ,na mashine kama jenereta za kuzalisha umeme na za kutumia kwenye shughuli za kilimo na uzalishaji hasa kwa watu waishio sehemu za vijijini.

Shirika la Afya duniani (WHO) ,limetangaza kuwa zaidi ya Watu milioni 1.4 wanafariki dunia ,kila mwaka kutokana na matumizi ya kuni na mkaa kama vyanzo vya nishati ya kupikia ambalo linaonekana kuwa janga la kidunia hasa kwa nchi za uchumi wa chini .

Tanzania ,nchi yetu ina watu zaidi ya milioni tisa wanaotegemea kilimo na ufugaji kama chanzo chao cha mapato na chakula ,wawekezaji pia wanajitokeza kwa wingi katika sekta hili,Licha ya kuwa na faida nyingi ,sekta ya kilimo inapaataa changamoto ya mbolea hasa kwa wakulima wadogowadogo ambao hupanda mazao bila ya kutumia mbolea ,ambayo hupelekea uvunaji wa kiasi kidogo cha mazao.

Je wajua?
Tanzania inazalisha uchafu unaoweza kuoza (uchafu wa asili) zaidi ya Tani 10,000 kwa siku kwa kila manispaa; kwahiyo kwa nchi nzima ,kuna kiasi kikubwa sana cha uchafu unaozalishwa,Uchafu huu ni fursa na una matumizi mengi badala ya kutupwa au kurundikwa kwenye dampo.Basi kama hukujua ,litumie andiko hili kujua hilo,na ningependa kukwambia kuwa ,uchafu huu unaozalishwa ni fursa !!!.

CHANGAMOTO tajwa hapo juu ,zote kwa pamoja zinazweza kutatuliwa kwa kutumia uchafu ambao unatusumbua hasa kwenye mazingira yetu ,na hivyo kubadilisha changamoto iliyo kwenye mazingira (uchafu) kuwa fursa.

Kwa kuanza na changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme hasa vijijini;uchafu unaweza kutumika kutengeneza umeme ,ambapo uchafu baada ya kuoza ndani ya kifaa maalum unatumika kuzalisha gesi asilia ,ambapo hiyo gesi inayozalishwa kwa mda mfupi kutokana na uchafu,inachujwa ili kuondoa mchanganyiko na kupitisha gesi tu, ambayo inatumika kuendeshea injini mbalimbali, ambazo zinatoa na kuzalisha umeme wa kutosha kuendeshea maisha ya nyumbani kama kuwasha taa,kuwasha pasi ,televisheni ,redio na vifaa vingine vinavyohitaji umeme kuendeshwa; hivyo changamoto inabadilishwa kuwa fursa kwa namna hiyo.

Changamoto ya pili kama ilivyotajwa hapo juu ,ni ya kutumia kuni na mkaa kama vyanzo vya nishati ya kupikia; changamoto hii ,inatatuliwa pia kwa kutumia uchafu ,ambapo uchafu ukiwa umechanganywa na kiasi kidogo cha maji ndani ya kifaa maalum,au tenki maalum, hutumika kuzalisha gesi asilia.Gesi hiyo inatumika kupikia ,ambapo gesi hiyo ina kiasi kikubwa cha nishati kulinganisha na vyanzo vingine vya nishati, na kulinganisha na gesi nyingine. Kutumia gesi kama chanzo cha nishati badala ya kuni na mkaa hupunguza kwa kiasi kikubwa hewa ya ukaa,na gesi chafu; lakini pia mazingira yanatunzwa na kulindwa ,na misitu pia hulindwa.Hivyo basi tunaona kuwa uchafu ni fursa tuitumie fursa hii ,kujiendeleza na kuendeleza nchi yetu.

Kuhusu bei ya petroli na vilainishi kuongezeka ,Je wajua kuwa unaweza kutumia gesi badala ya petroli kuendeshea vifaa mbalimbali ???,basi leo ningependa ufahamu kuwa gesi asilia inatumika kuendeshea mashine mbalimbali badala ya Petroli (Mbadala wa petroli ni gesi izalishwayo kutokana na uchafu asilia) ,na gesi hiyo huchujwa ili kuepuka kuharibu sehemu za ndani za injini inayoendeshwa; jenereta mbalimbali huweza kuendeshwa kwa gesi hii, na hivyo kutatua tatizo la kuongezeka kwa bei za Petroli na vilainishi kwa sasa.Injini za mashine mbalimbali pia zinaweza kuendeshwa kwa kutumia gesi inayozalishwa kutoka kwenye uchafu.

Baada ya kuzaliasha gesi,uchafu unaobaki unaweza kutumika kutengeneza vilainishi; Hili linaweza kuwezekana kupitia hatua mbalimbali na kwa kutumia kemikali mbalimbali zinazoongezwa kisaidia utengenezwaji na ubora wa vilainishi . vilainishi kama dizeli vinavyotumika kwenye magari na vyombo mbalimbali vya moto bila kusahau mashine mbalimbali, vyote vinaweza kutengenezwa kwa njia hii. Hii pia inatuonesha kuwa Uchafu kwenye maazingira yetu ni fursa hivyo yatupasa kuitumia ipasavyo kwa maendeleo kiujumla.

Kimiminika kinaobaki baada ya kuzalisha gesi ,pia kinaweza kusindikwa ili kutumika kutengeneza mbolea asili. Mbolea hii inayozalishwa kwa njia hii inakuwa na virutubisho mbalimbali na inaweza kuwekwa kwenye mifuko,maana inakuwa ishasindikwa kwa ajili ya kuweza kupelekwa sehemu mbalimbali za uzalishaji hasa mashambani,na sehemu nyingine za kibiashara kulingana na mzalishaji.Kupitia hili pia tunaona fursa kwenye uchafu uliopo kwenye mazingira yanayotuzunguka.

Hivyo basi ,ewe baba, ewe mama ,ewe kaka ,ewe dada, enyi ndugu , ni muda sasa wa kutumia changamoto ya Uchafu uliopo katika maeneo mbalimbali kwenye mazingira yanayotuzunguka ;mfano kwenye masoko na sehemu mbalimbali za kukusanya uchafu(dampo), kama fursa ya kujiendeleza kiuchumi ;maana ni ajira tosha kwa watu wa rika zote.Upande mwingine ,nguvu inahitajika kuwekezwa katika kuunga mkono bunifu mbalimbali ambazo zinaletwa mbele na wabunifu katika sekta mbalimbali; maana kupitia bunifu hizi fursa huweza kuonekana na hivo kuwa tiba kwa tatizo la ajira lililopo sehemu mbalimbali nchini.Vyombo vya habari pia ni nguzo mojawapo ,katika suala zima la kuhakikisha fursa mbalimbali zinawafikia watu kwa mda ,na pia mkono wa serikali ni muhimu sana katika kuhakikisha mazingira ni safi na salama .Na mwisho itoshe kusema “CHANGAMOTO NI FURSA ,UCHAFU NI FURSA

(Andiko hili limeandaliwa na Mr Laetus Buberwa )
 
Back
Top Bottom