Mtambo wa megawati 20 waletwa kuzalisha umeme Mtwara, Lindi

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Mtambo wa megawati 20 kuzalisha umeme Mtwara ma Lindi

[https://habarileo]

MIKOA ya Mtwara na Lindi imepokea mtambo mkubwa na kuzalisha umeme wa megawati 20 unaotarajiwa kuanza kazi kufanya kazi Machi 31, 2024.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mtambo huo unaenda kumaliza tatizo la umeme kwenye mikoa hiyo miwili.

Hayo yamesemwa wakati wa zoezi la ukaguzi wa mtambo huo wa kuzalisha umeme lililofanyika leo Februari 9, 2024 katika kijiji cha Hiari halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Amesema anafahamu namna ambavyo nishati hiyo ilivyokuwa kero kwa wananchi wa mikoa hiyo.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyofanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara alitoa maelekezo mahususi kwa mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko kuhusu hali ya umeme katika mikoa hii”

“Na kusema ukweli kwa maelekezo yale aliyoyatoa haikuwezekana tupate usingizi”amesema Mramba

“Mtambo huu mnaouona hapa umeletwa kwa maelekezo ya mheshimiwa Rais aliyoyatoa kwa Naibu Waziri Mkuu na yeye baada ya kupokea maelekezo hayo aliyasimamia”

Mkuu wa Mkoa Mtwara Kanali Amhed Abbas amesema upatikanaji wa mitambo hiyo inaenda kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo na ile dhana ya kuifungua mikoa hiyo inaenda kutimia.

Aidha sasa mikoa hiyo inaenda kuwa na umeme unaojitosheleza na mwingine wa ziada kwenye uwekezaji wa shughuli zingine mbalimbali za kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara, Abdallah Chikota amesema mikoa hiyo bila uwepo wa nishati ya uhakika haiwezi kufunguka.
 
Huo Utakuwa Wa Kupigia Cash Maana Bwawa Ambalo Daily Ngonjera Umeme Hakuna
 
Yaani serikali imeshindwa kuiunganisha mikoa ya kusini katika gridi ya Taifa wakati gesi ya mitambo ya Kinyerezi inatoka huko!
 
Umeme asilimia 60% wa Tanzania unatoka Lindi, sasa wabunge wa huko wanafanya nini pamoja na Majaliwa

Nchi ya hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom