Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.
- Inaelekea vigogo wengi wakubwa hawamo hiki chama, kama niliyoyasikia ni kweli basi ni bora hawa CCJ wangejiunga na Chadema, ni ushauri wa bure tu!
- Nina wasi wasi, kuna vigogo ndani ya CCM, wanataka kukitumia hiki chama kipya kama cover ya mambo yao, ni mawazo yangu tu!
Respect.
FMEs!
Bila hofu nawaita wafuatao wainuke sasa na kutangaza waziwazi kuunga mkono CCJ na kutoka waliko ili kuleta ushindi.
Hawa ni waheshimiwa, S.Sita, Prof. Mwakyembe, Prof.Mwandosya, Dr. Silaa, Prof. Beregu, Magufuri,
Wengine ni Dr.Salim H. Salim, Prof. Lipumba, Lwakatare (Ex MP),Waryoba, Mama Mpiganaji (sote tunamfahamu), Dr. Shayo (Diaspora), Sanctus-Rais TPN, Kawawa (MP), Makongoro Nyerere, Dr. Chinuno (Ex DC), present RC Morogoro na timu yao ya wanahabari ikiwa na Jerry Muro, Michuzi, Kubenea na Mwanakijiji kama PR Officer.
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.
- Inaelekea vigogo wengi wakubwa hawamo hiki chama, kama niliyoyasikia ni kweli basi ni bora hawa CCJ wangejiunga na Chadema, ni ushauri wa bure tu!
- Nina wasi wasi, kuna vigogo ndani ya CCM, wanataka kukitumia hiki chama kipya kama cover ya mambo yao, ni mawazo yangu tu!
Respect.
FMEs!
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine!
Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine! Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine!
Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?
Na Mwandishi wetu
TAARIFA za mchakato wa kusajili chama kipya, Chama Cha Jamii (CCJ) kinachoaminika kuhusisha makada wenye majina makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikalini, zimewashtua na kuwatikisa vigogo kadhaa wa CCM, Tanzania Daima imebaini.
Tayari vigogo hao wameanza mkakati wa kukihujumu chama hicho kisipate usajili ili kisishiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Chanzo cha habari kimoja kimeliambia Tanzania Daima kuwa CCJ imeanza kuonekana kuwa tishio zaidi kwa CCM kwa kuwa kina vigogo 27 wa CCM ambao ni wabunge wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Bunge.
Baadhi ya vigogo wanaotishika ni wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kwa vile chama hicho kimetamba kwamba vita ya ufisadi ndiyo ajenda yake kuu, na hakitakuwa tayari kumpokea mwanachama yeyote mwenye tuhuma za ufisadi.
Moja ya sera kuu za CCJ ni kutetea na kulinda rasilimali za taifa ili zisitumiwe na watu wachache kwa manufaa yao.
Waanzilishi wa CCJ wanasemekana kuwa ni baadhi ya vigogo waliochoshwa na CCM, hasa kwa madai kuwa chama hicho tawala kinawafumbia macho baadhi ya makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi kiasi cha kuyumbisha nchi na chama chenyewe, huku wananchi wakiendelea kuwa masikini.
Kuna orodha ya wabunge wanaodaiwa kuwa waanzilishi wa chama hicho ambao hawajaweka wazi majina yao, na wamewatanguliza wengine kwa sababu za kiusalama na kimkakati.
Zipo taarifa pia kwamba tayari vyombo vya usalama vimeanza kuifuatilia CCJ ili kubaini majina ya vigogo waliomo.
Taarifa nyingine zinasema baadhi ya vigogo wamekuwa na hofu na mustakbali wao ndani ya CCM hasa baada ya kuelezwa uanzishwaji wa CCJ umetokana na kile kinachoonekana ni udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, anayetuhumiwa kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu dhidi ya makada wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa.
Ndugu yangu kuna baadhi ya vigogo sasa wana wasiwasi kuwa chama kinaweza kuwatosa ili kinusurike na aibu ya kumeguka ambako bila shaka kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuja kwa CCJ, kilisema chanzo kimojawapo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa hatua hiyo ya baadhi ya wanachama wa CCM kuanzisha chama chao ni kitisho au shinikizo kwa Rais Kikwete, ili achukue hatua kali dhidi ya wanachama wanaokitia doa chama hicho tawala.
Shinikizo hilo linapata nguvu kutokana na dhana kwamba asipochukua hatua kali chama kinaweza kufia mikononi mwake, jambo ambalo asingependa kuhusishwa nalo.
CCJ inaweza kuwa shinikizo la baadhi ya makada wa CCM kumshinikiza Mwenyekiti (Kikwete) kukisafisha chama kwa kuwaondoa wale wote wanaotuhumiwa katika kashfa mbalimbali, kilisema chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutambulishwa gazetini.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa chama hicho kipya, Richard Kiyabo amesema ana uhakika wa kutimiza masharti ya usajili wa kudumu ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kiyabo alisema hayo kama majibu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa ambaye juzi aliliambia Tanzania Daima kuwa chama hicho hakitaweza kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa mchakato wa kukifanya kipate usajili wa kudumu utachukua muda mrefu.
Mwenyekiti huyo alisema hadi sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kupata wanachama 200 kwa mikoa 10 kama walivyoagizwa na msajili wa vyama vya siasa na kusisitiza kuwa watashiriki uchaguzi ujao.
Kwa kujiamini, mwenyekiti huyo alisema hadi sasa kwa Dar es Salaam peke yake tayari wamepata wanachama 2,000 watakaohudhuria siku ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu kwenye ofisi za msajili.
Hili jambo kwamba hatutashiri kwenye uchaguzi ujao limewashtua sana wanachama wetu tumepokea simu za kuulizwa kila wakati, ndiyo maana nikaenda kwa mmoja wa wanasheria wa ofisi ya msajili.
Katika kufafanua jambo hilo, nimeambiwa hata kesho kama tunaweza tupeleke majina ya wanachama wetu 200 kila mkoa kwa mikoa nane ya Tanzania Bara na miwili ya Visiwani, si lazima miezi sita, alisisitiza na kuongeza kwamba idadi hiyo ikishatimia kinachofanyika ni kukamilisha baadhi ya taratibu ndani ya chama.
Alisema CCJ imejizatiti kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, na baadhi ya wanachama watagombea ubunge iwapo ofisi ya msajili itafanya bidii katika kupitia taarifa za wanachama wao.
Hata hivyo Kiyabo alikanusha taarifa za chama hicho kuasisiwa na baadhi ya vigogo wa CCM.
Chama chetu kimekuja kufanya mapinduzi kwenye siasa za upinzani. CCJ haitakubali kuwapokea majeruhi wa ufisadi kutoka vyama vingine. Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kusema upinzani wa kweli utatoka CCM. Tumejizatiti kujenga jamii yenye usawa kwa kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wote tutapigana vilivyo na ufisadi, alisema.