akashube
JF-Expert Member
- Dec 24, 2009
- 401
- 24
Tunaanza upya tu... yale yale ya akina Mabere Marando, Makani et al.. mwisho tunaanza nambari wani nambari wani....
Kwa maoni yangu hao wote wako 'kuyumbisha' matokeo ya uchaguzi unaokuja, kama vigogo nao wapo matokeo ni rahisi kutabirika....
Mwito kwa wananchi: Vyama vinavyothibitika kuwa na uwezo wa kuondoa baadhi ya manung'uniko vinaeleweka CCM, CUF, CHADEMA, etc etc na sio kwa mpangilio huu- Kabla wananchi hawajapiga kura, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya nchi hii(kuanzia mwanzoni mwa kukubalika kwa vyama vingi) na historia ya hao vigogo(chama kipya) kama kipo/wapo
Hakuna ubaya kukawa na Chama kingine kipya, vilevile hakuna ubaya kama Wananchi watakuwa wamejifanyia mazingaombwe na kuona huo mbadala.
Piga kura kwa uangalifu!
Ahsante.
Haya ndio matatizo ya kutaka kuwa katikati kama Kikwete vile. Uwe na msimamo maana mi naona hapa unazungukazunguka pale pale, ingawa ulianza vizuri tu.... Hivi CCM Kwa jinsi kilivyo kibovu ndiyo ukipange na CUF na CHADEMA, wanafanana kweli?.
CUF na CHADEMA ni vyama vyenye wanachama wa kweli kutoka moyoni. Hawaogopi kufanyiwa UBAREGU....................upo hapo? Ni vyama vya watu majasiri, makini, wenye uzalendo na uchungu wa kweli wa nchi. Wanatetea watu wasiostahili kutetewa maana watanzania ni watu wa kufuata upepo kama bendera na ndio maana tunastahili kuendelea kuibiwa MCHANA KWEUPE. TUMEKUWA KAMA MANDONDOCHA NA U-CCM WETU.
CCM ni chama cha waoga, watu waliojiunga ili kupata ulaji, madili, misheni town, wanabebwabebwa na wajomba, mafisadi, watu wasio na msimamo sikuzote wako katikati. Huwezi kuwa mwanachama mzuri CCM kama Kikwete bila kuwa na Phd ya Unafiki, Kujikombakomba, na uongo wa kizamani wa enzi za Zinjanthropus.
CCJ ni chama cha mafisadi waliokosa hisa kwenye serikali ya Kikwete na hivyo wanajifanya ni wapinga ufisadi kwa sababu za visasi. Saa hizi wanapima upepo, ni ndumilakuwili na ndio maana wanajificha, watu wa hivyo hawatufai hata kidogo, hawawezi kulitetea taifa hili dhidi ya ubabe wa ubeberu mamboleo. Wanataka kutumia mwanya uliopo ili kuhakikisha wanashika hatamu 2010. Hawataki kurudia makosa ya 2005 yaliyowafanya waishie kwenye ubunge tu na kukosa mashavu mengine. Lakini pia kinaungwa mkono na mafisadi walioburuzwa kortini na kudhalilishwa hadharani, na kwenye vyombo vya habari ili kulipa kisasi dhidi ya Kikwete mlea ufisadi.
CCJ ni kama CCM tu kwa kuwa ni watu wanaotaka kuingia madarakani kwa maslahi yao binafsi na familia zao huku wakiudanganya umma kuwa wanataka kuweka mambo sawa, na kujifanya wanataka kuiangalia jamii....bla..bla...bla.
Suala hapa ni kuwa tusikubali kudanganywa na mwanasiasa yeyote kwa vitendo avifanyavyo 2010. Tuwapime wamefanya nini 2005 mpaka 2009. kwa sababu hapa 2010 kila mmoja anakuja na danganya toto ili akubalike kwenye uchaguzi.
Walikuwa wapi kuunda chama sikuzote hizo...MPAKA WANYIMWE MKATE NDO WAJIFANYE WANATUPENDA SANA WATANZANIA? WANAFIKI WAKUBWA!!!!!!!!!!!
CCM- CHAMA CHA MAFISADI
CCJ - CHAMA CHA JANGILI
ENDELEENI KUSEMA KIDUMU UONE NINI KINADUMU NCHINI.....SHAURI YENU!!!!!!!