Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

  • Mkakati wa kuimega CCM waanza rasmi
  • Tendwa aonya hakiwezi kushiriki uchaguzi wa Oktoba
KITENDAWILI cha kuwapo kwa kundi moja la makada maarufu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuingia katika mchakato wa kuanzisha chama kipya cha siasa, kimeanza kuteguliwa baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kupokea maombi ya kusajiliwa kwa chama hicho, Tanzania Daima limebaini.

Maombi rasmi ya kutaka kusajiliwa kwa chama hicho kiitwacho Chama Cha Jamii kwa kifupi CCJ, yaliwasilishwa katika ofisi hizo Jumanne wiki hii.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka miongoni mwa makada maarufu wa CCM ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa wanachama wa siku za usoni wa chama hicho zilizothibitishwa pia na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa zinasema waliowasilisha maombi hayo ni watu ambao majina yao hayajulikani kabisa katika medani ya siasa nchini.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima jana na juzi ulibaini kuwa viongozi wa juu wawili wa chama hicho waliowasilisha maombi ya usajili huo ni Richard Kiyabo anayetajwa kuwa mwenyekiti wa muda na Katibu Mkuu, Renatus Muhabi.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Tendwa alikiri ofisi yake kupokea maombi ya usajili wa chama hicho.

Pamoja na kukiri kuhusu kupokea taarifa za kuwapo kwa maombi hayo jana, Tendwa alikataa kufahamu lolote kuhusu kuwapo kwa uhusiano kati ya chama hicho na taarifa za kuwapo kwa mpango wa kuimega CCM.

“Ofisi imepokea maombi ya usajili wa vyama vingi tu si kimoja, ni kweli hicho chama cha Jamii nimepata taarifa leo (jana) na watu wawili wamewasilisha maombi ya kusajiliwa. Siwezi kukumbuka majina yao wote ila mmoja wao namkumbuka kwa jina moja la Kiyabo. Sasa sijui kama ni mwana CCM au la,” alisema Tendwa alipoulizwa kuhusu undani wa chama hicho.

Hata hivyo akizungumzia kuhusu taratibu na sheria za usajili wa vyama, Tendwa alisema baada ya kuwasilisha ombi hilo na kupatiwa usajili wa muda, chama hicho kitatakiwa kwenda mikoani na kusaka wanachama wanaofikia 200 kwa kila mkoa na watawasilisha katika ofisi hizo.

Alisema baada ya kukamilisha kazi hiyo, baada ya miezi sita tangu kupewa usajili wa muda, waombaji watatakiwa kuwasilisha maombi ya usajili wa kudumu kabla ya kazi ya uhakiki kuanza.

Kazi ya kuanza kukisajili tangu hatua ya usajili wa muda na kisha usajili wa kudumu kama itaenda sawasawa kwa sababu ya kuwapo kwa ile miezi sita ya awali na kuwapo pia kwa kazi ya uhakiki, chama hicho kinaweza kikapatiwa usajili kamili ifikapo Septemba mwaka huu. Hakiwezi kushiriki katika uchaguzi wa mwaka huu,” alisema Tendwa.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi iwapo kuna uwezekano wa waanzilishi wa chama hicho wakafanikiwa kutimiza masharti katika kipindi kifupi kijacho na hivyo kutaka washiriki katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, pasipo kutaka kuingia kwa undani alisema; “haiwezekani wakashiriki uchaguzi mwaka huu. Hapa tuna kazi nyingi za kufanya, kuna kazi ya uhakiki na ile ya wao kuomba usajili wa kudumu baada ya miezi sita kama sheria inavyosema.”

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kiyabo ambaye ni mwenyekiti wa muda wa chama hicho, alikanusha taarifa zinazokihusisha chama hicho na kundi mojawapo la vigogo wa CCM wakiwamo wabunge.

Akikariri taarifa za magazeti mawili yanayochapishwa kila Jumatano, Kiyabo alisema chama chao ambacho kitasimamia misingi asilia ya ujamaa, kutetea rasilimali na kupambana na ufisadi, kitakapokuwa kimepata usajili kitawakaribisha Watanzania wote wazalendo kujiunga nacho.

“Hizo taarifa za magazeti hazitoki kwetu. Ndiyo kwanza tuko katika hatua za awali, hakuna kigogo yeyote wa CCM aliye nyuma yetu. Tutakaposajiliwa tutawakaribisha wote ambao wanaamini katika katiba yetu na malengo yetu kuwa wanachama,” alisema.

Kiyabo ambaye kitaaluma alieleza kuwa yeye ni mchumi na mtaalam wa masuala ya jamii (sosholojia) akiwa na Shahada ya Uzamili aliyoipata katika chuo kimoja nchini Kenya alichokataa kukitaja, alisisitiza kwamba chama chao kitakuwa na msimamo mkali dhidi ya mafisadi.

“Hatutataka kabisa kuwa na wanachama ambao ni mafisadi, na tukipata usajili tutapambana na ufisadi kwa nguvu kubwa,” alisema kiongozi huyo wa muda wa CCJ.

Alieleza pia kwamba wao walikuwa wanaamini kwa dhati kwamba Tendwa anao uwezo wa kuwawezesha wakakisajili chama mapema iwezekanavyo na hata wakaweza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

“Tuna imani kubwa na Tendwa kwamba atalishughulikia ombi letu na kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo na tutaweza kushiriki katika uchaguzi baadaye mwaka huu,” alisema Kiyabo alipotakiwa kueleza iwapo walikuwa wana uwezo wa kukabiliana na ufupi wa muda wa usajili,” alisema Kiyabo.

Chama hicho kimejiwekea malengo mbalimbali na kuamini kuwa, binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa, kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, hifadhi na ustawi wa jamii vitapatikana kwa matumizi bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali zilizopo, serikali kuwajibika kwa wananchi ambao ni msingi wa mamlaka yote katika nchi na kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote.

Mengine ni umoja ni nguvu ya pekee ya wananchi katika kujenga jamii yenye usawa na uhuru na katika kuondoa umaskini, ujinga, maradhi na kupambana na ufisadi na uongozi bora unaozingatia uzalendo, maadili ya uongozi na kuwajali wanyonge katika jamii ni sharti la msingi la kuendesha nchi.

Aidha, madhumuni ya CCJ ni kuhakikisha utajiri wa rasilimali zilizopo unatumika kwa maendeleo ya wananchi kwa kuondoa umaskini, ujinga na maradhi, kuhakikisha uwekezaji unatekelezwa kwa kumnufaisha mwananchi ambaye anazungukwa na kamwe usitoe fursa kwa wageni kuhodhi rasilimali hizo bila ushiriki wa wananchi.

Lengo jingine ni kuhakikisha shughuli za uchumi haziruhusu ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi kuwa katika mamlaka ya watu wachache binafsi.

Mengine ni kujenga umoja wa kitaifa kwa kutoa fursa sawa na za kutosha kwa wananchi wote, wake kwa waume bila kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu, kuhakikisha kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, uonevu, rushwa au ufisadi zinatokomezwa nchini, kuhifadhi na kuendeleza mazingira kwa ajili ya uhai na afya ya binadamu na viumbe vingine na kwa faida ya vizazi vijavyo, kulinda haki ya kila raia ya kujielimisha au kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote na kuhakikisha mfumo wa uchaguzi ni huru na unaotoa fursa stahili kwa wananchi.

Taarifa kuhusu kuwapo kwa mpango wa kundi moja la makada wa juu wa CCM kutaka kuanzisha chama kipya zimeanza kusikika chini chini kwa muda mrefu kabla ya wiki hii habari hizo kuripotiwa katika magazeti mawili tofauti yanayochapishwa kila Jumatano.

Vyanzo kadhaa vya habari vimekuwa vikidai kuwa mpango huo unasukumwa kwa upande mmoja na dhamira ya kundi mojawapo lenye ushawishi mkubwa ndani ya chama hicho tawala kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya CCM. Kwa mujibu wa habari hizo, kundi hilo la makada wa CCM ambao baadhi yao Tanzania Daima ina majina yao, haliridhishwi na namna CCM inavyoshughulikia matatizo kama yale yanayohusu matumizi ya rasilimali za umma na lile la kukithiri kwa vitendo vya ufisadi.
 
Kiyabo Kiyabo Kiyabo.

Hana jina la kwanza huyu Kiyabo? Hivi hatuna namna ya kutajana majina formally? Haya, ndugu imekufa, na jina lake la kwanza hamumjui na mmeshindwa kumbana Tendwa alitoe, mnashindwa hata kusema bwana Kiyabo?
 
Ati wana kazi nyingi! Umeona Chama Cha Majambazi kinavyoogopa upinzani hata ule ambao haujulikani.
 
Kiyabo Kiyabo Kiyabo.

Hana jina la kwanza huyu Kiyabo? Hivi hatuna namna ya kutajana majina formally? Haya, ndugu imekufa, na jina lake la kwanza hamumjui na mmeshindwa kumbana Tendwa alitoe, mnashindwa hata kusema bwana Kiyabo?


ni Richard Kiyabo Mwenyekiti wa muda na Renatus Muhabi Katibu Mkuu jamani kuna mwenye CV zao
 
Ati wana kazi nyingi! Umeona Chama Cha Majambazi kinavyoogopa upinzani hata ule ambao haujulikani.


Watabana sana lakini mwisho wataachia nafikiri Makamba sasa halali akifikiria yanayoendelea Zenji hadi kikao chake NEC Dom kususiwa na sasa hili la CCJ kaazi kweli kweli.

Kama kweli CCJ ni part ya CCM basi walijua mapema kuwa kutakuwa na usumbufu kwa msajili maana mbinu wanazijua zote watazungushwa hadi uchaguzi upite lakini kwetu yote ni heri tu litakuwa somo tosha kwa CCM watakaobaki au CCM masalia.

hata kama CCJ haitashiriki uchaguzi wagombee kupitia vyama vingine vya upinzani kama kweli wako serious, ninawaambia CCM si kwamba wananchi hawaipendi CCM ila hawapendi matendo yao hata CCJ wakija na staili ya CCM na matendo yale yale tutawaponda vile vile.
 
Chama kimeshapata usajili wa muda..

- Yees! kimesajiliwa rasmi jana nina-confirm kwa 100%, wamewatuma kusajili wananchi wasio na profile kabisaa wao wenyewe bado wamejificha nyuma, isipokuwa the dataz ni habari ya kwanza ya hiki chama imetolewa na gazeti la Sauti Huru na inaaminika kwamba washirki wakubwa wa hili gazeti ni kina Lowassa na Nchimbi, je ni wao walioko behind hiki chama kipya? Bado ni kitendawili!

- Pia kuna tetesi za kumhusisha mfanya biashara mmoja maarufu sana nchini ambaye ni mzawa!

- Kesho kwa mara ya kwanza katiba rasmi ya chama hii kipya itatolewa somewhere somehow, please no questions! yaani usiniulize maswali maana sina majibu!

Respect.


FMEs!
 
Tunaanza upya tu... yale yale ya akina Mabere Marando, Makani et al.. mwisho tunaanza nambari wani nambari wani....

Kwa maoni yangu hao wote wako 'kuyumbisha' matokeo ya uchaguzi unaokuja, kama vigogo nao wapo matokeo ni rahisi kutabirika....

Mwito kwa wananchi: Vyama vinavyothibitika kuwa na uwezo wa kuondoa baadhi ya manung'uniko vinaeleweka CCM, CUF, CHADEMA, etc etc na sio kwa mpangilio huu- Kabla wananchi hawajapiga kura, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya nchi hii(kuanzia mwanzoni mwa kukubalika kwa vyama vingi) na historia ya hao vigogo(chama kipya) kama kipo/wapo

Hakuna ubaya kukawa na Chama kingine kipya, vilevile hakuna ubaya kama Wananchi watakuwa wamejifanyia mazingaombwe na kuona huo mbadala.

Piga kura kwa uangalifu!

Ahsante.
 
Nafikiri hakuna taabu kuanzishwa kwa chama kingine...ni haki ya kikatiba. Wasawasi wangu ni kuwa imefika wakati haya yafanyike kitaalamu zaidi, Miezi kumi kabla ya uchaguzi mkuu! Hili ni kosa kama lile walilofanya COPE kule South Africa. Hata kama sera na nia ni njema na viongozi ni wazuri ni vyema walengwa - wananchi wapate nafasi ya kuwafahamu na kujua nia ya dhati ya chama ili kuwapa nafasi. Otherwise tunaendelea kuwachanganya wananchi na wataendelea kupiga kura bila taarifa za kutosha.
 
Kiyabo Kiyabo Kiyabo.

Hana jina la kwanza huyu Kiyabo? Hivi hatuna namna ya kutajana majina formally? Haya, ndugu imekufa, na jina lake la kwanza hamumjui na mmeshindwa kumbana Tendwa alitoe, mnashindwa hata kusema bwana Kiyabo?

Ukisoma mwanzo kwenye hiyo citation ya Luteni utaona kuwa jina lake kamili ni Richard Kiyabo
 
CHAMA KIPYA KINACHOHUSISHA VIGOGO WA CCM, UPINZANI CHATINGA KWA MSAJILI WA VYMA VYA SIASA

Na Exuper Kachenje

WAKATI kukiwa na taarufa za baadhi ya vigogo wa CCM kujiengua, jana Msajili wa Vyama vya Siasa alipokea maombi ya usajili wa Chama Cha Jamii (CCJ), ambacho kinahusishwa na kumeguka kwa chama tawala.

Kuwasilishwa kwa maombi hayo kumekuja wakati hali ya hewa ndani ya CCM ikiwa imechafuka baada ya vita dhidi ya ufisadi kuonekana kuwagawanya vigogo wa chama hicho, huku hali visiwani Zanzibar ikizidi kuwagawa wanachama wa chama hicho tawala.

Wakati baadhi ya vigogo wa CCM wanaonekana kutoridhishwa na hali inayoendelea kwenye chama hicho tawala na kuhusishwa na mipango ya kuunda chama kipya, watu wawili jana walitinga ofisi za msajili wa vyama vya siasa kuwasilisha maombi ya usajili wa chama kipya.

"Ndio, leo walikuja kwangu watu wa Chama cha Jamii na nimepokea maombi yao. Kwa kifupi ni hivyo ukitaka zaidi njoo ofisini kwangu," alisema Msajili John Tendwa alipoulizwa kuhusu kuwasilishwa kwa maombi hayo na watu waliojitambulisha kuwa ni Richard Kiabo, ambaye anakuwa mwenyekiti wa muda na Renatus Muwadi, ambaye ni katibu mkuu wa muda.

Dira na lengo kuu la CCJ ni Ustawi na Hifadhi ya Jamii pamoja na demokrasia, kwa mujibu wa rasimu ya katiba ya chama hicho ambacho makao yake makuu yatakuwa jijini Dar es Salaam, huku ofisi ndogo zikiwa Zanzibar na Dodoma.

Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ya CCJ bendera ya chama hicho itakuwa na rangi nne ambazo ni bluu, dhahabu, nyeusi na kijani, rangi ambazo zinapishana kidogo na za bendera ya taifa.

Rasimu hiyo, ambayo gazeti hili tayari limeipata, inafafanua kuwa rangi ya bluu ni ishara ya maji yanayounganisha pande mbili za Muungano yaani Zanzibar na Tanganyika, dhahabu, rasilimali za Tanzania, nyeusi ni watu na kijani ni kilimo, mazingira na uoto.

Imebainisha kuwa itikati ya CCJ ni demokrasia ya kijamii inayozingatia umoja wa taifa, utawala wa katiba na sheria, mgawanyo wa mamlaka ya dola, haki za binadamu, uhuru na ustawi wa jamii.

Aidha, misingi ya kiitikadi na nguzo za CCJ ni utawala wa dola na miiko ya uongozi ambapo imani yake kuu ni kwamba binadamu wote ni sawa, huzaliwa huru na Waafrika ni taifa moja. Pia kinaamini umoja wa Tanzania ni nguzo kuu ya umoja wa taifa la Waafrika na ni moja ya malengo makuu ya dola la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari za uhakika ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa viongozi hao wa muda wa CCJ wametangulizwa na baadhi ya vigogo kutoka ndani ya CCM ambao wanaandaa mikakati ya kukihama chama hicho katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Habari zinasema kuwa vigogo hao wa CCM, wakiwemo viongozi wa zamani na wabunge, wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kujadili mkakati huo na mpango wao wa awali ulikuwa ni kupambana na Rais Jakaya Kikwete ndani ya chama katika uchaguzi wa Oktoba.

Hata hivyo, habari hizo zinadai, ilionekana kuwa vigumu kumshinda Kikwete katika kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais kutokana na kusaliwa na muda mfupi wa kukampeni na ndipo walipoamua kusajili chama kipya.

Inasemakana kuwa baada ya kuvuja kwa mpango wa kuanzisha chama, vigogo hao walitaka kuingia kwenye moja ya vyama vya upinzani, lakini baada ya majadiliano ilibainika kuwa mpango huo unaweza kusababisha matatizo kama ilivyokuwa kwa NCCR Mageuzi.

NCCR, ambayo ilichomoza kwa nguvu na kujipatia wanachama wengi kiasi cha kuitikisa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, nusura isambaratike baada ya wanachama kuanza kumpinga Augustine Mrema aliyepewa uenyekiti na ugombea urais baada ya kujiengua CCM.

Habari zinasema kwamba tofauti na Mrema ambaye alitoka CCM akiwa peke yake, vigogo wa CCM watakuwa na kundi kubwa la vigogo wa CCM.

"Wanaweza kuwako zaidi ya wabunge 20 wa CCM, vilevile, kuna wabunge wa upinzani nao watakuwako katika kundi hilo. Kinachosubiriwa ni muda wa kufanya maamuzi hayo," alisema mtoa habari ambaye ameshiriki kila hatua ya kuanzisha chama hicho.

Habari za ukakika zinadai kuwa CCJ kimeratibiwa kwa karibu na vigogo wa CCM kwa kushirikiana na wanasheria makini.

"Chama hiki kimeanzishwa kutokana na maombi ya wanachama wa CCM, wanachama wa vyama vya upinzani na wananchi," alisema katibu wa CCJ, Muwadi.

"Ni mawazo ya wananchi, wafanyakazi, wastaafu, baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani na chama tawala cha CCM."

Hata hivyo, viongozi hawa wa muda watarajiwa kuwaachia madaraka vigogo hao wa CCM ambao wana ushawishi mkubwa kwa jamii mara watakapotangaza hatua ya kukihama chama tawala.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanatabiri kwamba kuanzishwa kwa CCJ kunaweza kuvuta vyama vingine vya upinzani kama NCCR-Mageuzi, Chadema na hata CUF kwa upande wa Bara na kushirikiana hivyo kutoa changamoto kubwa kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Vilevile, CCJ huenda kikachukua wabunge wengi wa sasa kutoka CCM ambao wanaweza kuangushwa katika kura za maoni, hivyo kikawa na nguvu zaidi.

Ni kwa mantiki hiyo pia wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona nguvu ya vyama vya upinzani vilivyopo sasa kupungua kutokana na uwezekano wa kupoteza wapenzi na wanachama kwa chama hiki kipya.

Vita ndani ya CCM imeonekana kuwa ni kubwa tangu kuibuka kwa kashfa ya Richmond iliyosababisha mgawanyiko mkubwa kuanzia kwa vigogo hadi wanachama wa CCM. Vita hiyo imekuwa ikipiganwa ndani ya chama, Bunge na nje, kiasi kwamba halmashauri kuu iliunda kamati ya watu watatu kujaribu kuondoa tofauti hizo.

Hata hivyo, habari zinasema kuwa kamati hiyo inaonekana kushindwa kuibuka na mapendekezo ya maridhiano yanayoweza kuridhisha pande zote mbili, hali ambayo imesababisha kila kundi kuanza mikakati yake kwa ajili ya Uchaguzi Kuu ujao.

CCM ilikuwa iitishe vikao vyake vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, lakini ilishindikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuingiliana kwa ratiba ya vikao hivyo na vile vya Baraza la Wawakilishi.

Hata hivyo, hali si nzuri visiwani Zanzibar ambako urafiki mpya wa Rais Amani Abeid Karume na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Seif Sharrif Hamad unaendelea kukomaa kiasi cha chama hicho kupendekeza mtoto huyo wa muasisi wa taifa la Zanzibar aongezewe muda.

Pendekezo hilo la CUF limeungwa mkono na wanachama wa CCM wanaoonekana kumuunga mkono Karume, huku wapinzani wake wake wakipinga maafikiano hayo na mpango wa kumuongezea muda kiongozi huyo wa SMZ.

Tayari mwakilishi wa CUF ameshawasilisha kwa katibu wa Baraza la Wawakilishi hoja yake binafsi ya kutaka marekebisho ya katiba ili Karume aongezewe muda kuhitimisha kazi aliyoianza ya kuondoa siasa za chuki na kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi, ambao umeelezewa kuwa ndio chanzo cha machafuko visiwani humo.

utabiri wa mwanakijiji unatimia?
 
Ni wale wale tu,hakuna mpiganaji katika ufisadi................Wa tanzania tutaendelea kuliwa mpaka siku ya mwisho!!!

Alsaidy, are you ready prepared kuliwa, actually am not? Ikiwa Watanzania wataendelea kuwa na mtizamo kama huo ulio nao, Hakika wataendelea kuliwa.

Tambua kuwa mafanikio hayaji kwa siku moja, ni hii ni dalili na ni maendeleo kuelekea kule tunakopataka. Tunahitaji watu wenye mtazamo kama huu wa CCJ.
 
Alsaidy, are you ready prepared kuliwa, actually am not? Ikiwa Watanzania wataendelea kuwa na mtizamo kama huo ulio nao, Hakika wataendelea kuliwa.

Tambua kuwa mafanikio hayaji kwa siku moja, ni hii ni dalili na ni maendeleo kuelekea kule tunakopataka. Tunahitaji watu wenye mtazamo kama huu wa CCJ.

CCJ changa la macho tu. Komredi ogopa sana wanasiasa wanaojitutumua kufanya jambo 2010. It is too late. 2005 yoote mpaka 2009 walikuwa wapi? Hawa ni wanafiki wale wale tu wa siku zote, Ila mkate ni mdogo na kila mmoja anautaka na kifimbo ndo alishalala kwa hiyo hakuna kiranja.....Kumeguka kwao CCM kutaifaa nchi kama wakichukua wapinzani wa kweli...NA SIO HAWA WALIONYIMWA MKATE KWA HIYO WANAONDOKA KWA CHUKI...HUKU WAKIDANGANYA KUWA WANAPIGA VITA UFISADI.

CCJ ni matokeo ya huruma za fisi...fisi huyu amesimama kwa mbali akimwonea huruma swala anayeliwa na simba,...haimaanishi akipata nafasi atamwokoa swala yule.....itakuwa mbaya zaidi maana atakula na kubakiza nyasi zenye damu tu kama ushahidi kuwa kuna mnyama kaliwa....HAKIBAKI KITU.....ffffffuuuu!!!!!!!!!!!!!

KOMREDI AMKA....EBO!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom