Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Ehee najiuliza wanaoenda kuunda CCJ ni viongozi wa sasa waliomo CCM? Sawa. Lakini kwa asili yao ni watu wanaopenda madaraka. Je wako tayari kuongozwa na wengine?

Fedha za kuendesha kampeni yao na kuendesha cCJ wataipata kutoka wapi. Je ni zile ambazo vyanzo vyake ni vya kifisadi. Kama ni za akina RA na wenzie je watakubali kuwalipa wengine?

Muda umeenda na tumebakia na miezi kama 9. Muda huo uliobakia unatosha kuitangaza CCJ na wao kukubalika kwa wananchi na kuweza kugombea ubunge, udiwani na Urais?

Hiyo bendera yao ni ile iliyokuwa ya TANU. Lugha iliyotumika ni ya akina wazee wetu wa MNF (Mwalimu Nyerere Foundation.
Umri wa hao waasisi wa CCJ ni upi. Kama ni wale wazee wetu wa MNF na wengineo hawana stamina ya kuzunguka nchi nzima na kukinadi CCJ.

Ninasema chama hiki ni non starter
 
Chama cha jamii gani/ipi? Hizi CC ambazo zilikuwa kule kwenye nCCr huwa wazipendea nini?
Tusubiri mkuu,hata hao kina Invisible wakiamuwa kujitokeza tutawasapoti kwa nguvu zetu zote....Hivyo ondoa shaka mkuu,hayo mambo ya cc yasikupe shida sana,this time inaelekea itakuwa kati ya ccJamii na ccMafisadi...Kaazi.
 
Muda umeenda na tumebakia na miezi kama 9. Muda huo uliobakia unatosha kuitangaza CCJ na wao kukubalika kwa wananchi na kuweza kugombea ubunge, udiwani na Urais?

Kwa watanzania niaowajua mimi kwao muda si tatizo kwanza hawana haja ya sera wanachotaka kujua ni nani waliomo CCJ na mgombea urais basi kama ni RA au EL au 6 au .... mengine sijui ya ilani wao hawana habari kabisa ni wewe tu, si ulishaambiwa 70% hufuata upepo au umesahau kwa hiyo hata uchaguzi ungekuwa wiki ijayo sawa tu.

go.. go......... CCJF
 
...Hakuna jipya.....hawa wametofautiana kwenye maslahi.....wakiingia madarakani hawatakuwa na jipya zaidi ya kuendeleza ulaji....
 
Eee mola tusaidie ili hili lisiwe tetesi tu, waachwe waanzishe hicho chama lakini na wao wasijekuwa na hila kama za hawa wa sasa, labda ndiyo watatukomboa watanzania kutoka kwenye huu ufedhuli wa walio madarakani sasa, haki ya nani.. kwa hili naona ile ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania itaweza kutimia...Mungu sikia kilio chetu, CCM ndiyo imetufanya bado tunadharaulika miaka 48 baada ya uhuru.
 
Tunahitaji hili dude kubwa linalochosha na hata kusahau malengo ya kuanzishwa kwake lenyewe limeguke ndipo tunaweza kuona mbele, kwani kwa sasa limeziba njia. Binafsi naamini ukombozi wa mtanzania utakuwa umeanza bila kuzingatia kama chama kitakuwa kizuri au kibaya.

Tunachohitaji kwa sasa ni hii nguvu kubwa ya kikandamizaji igawanyike na ni hapo vyama vya upinzani vya kweli vitaweza kuchanua, kwani ni wakati huu tutafahamu mbinu chafu ambazo hutumika nyakati za uchaguzi na kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na fair play.

Sijavutiwa sana na chochote kilichoelezwa kama malengo ya chama kwani vyama vyetu vinaweza kuwa na katiba nzuri kuliko hata ya uingereza au marekani ambao kwa kweli kwa kiasi kikubwa huwa wana ifanyia kazi na watchdog huwa wapo. Tatizo la sisi kuandika tunajua tatizo huwa kutekeleza na ni hapo u dikteta ndio unapoanzia na baadaye kilio cha sasa ufisadi unaposhamiri.

Kilichonifurahisha ni ku split kwa sisiem nasali hiyo itokee sasa hivi! Na hii itakuwa sababu ya kuwa hata ikibidi mwanachama miongoni wa mwanzo kabisa kama namna ya kupongeza safari ya ukombozi wa tanzania huru utakaokuwa umeanza. Wakiboa kama alivyosema baba wa taifa chama sio mama yake chama ni sera ikishindikana waenda kokote.
 
Tuna chama wadau, kwa mujibu wa redio mbao. Wanabodi wote wenye post zaidi ya 10,000 wana candidacy ya ubunge sehemu wanapotaka, wakigongana mwenye posts zenye thanks nyingi anashinda.
Mkuu hii yako mie sijaielewa naona imekaa ki comedy kidogo.Hatuwezi kuwa makini kidogo nyakati hizi tukielekea uchaguzi hasa tunapochangia mada muhimu kama hii, au wewe ni Mkenya hivyo hu feel?
 
Ingawa inawezekana maana ni haki ya kikatiba watu kuanzisha au kujiunga au kuhama kutoka chama chochote si tu CCM bali hata vya Upinzani, bado habari hii ninai rate kama uvumi, hisia, ndoto au kauli ya utafiti fulani kuliko tukio ambalo limeshatokea!

Hivyo sita fanya uchambuzi wowote juu ya 'CCJ' sasa mpaka nitakapojiridhisha kuwa huku si kupima uelekeo na kasi ya upepo wa uchaguzi!
 
Mmesahau aliyosema baba wa taifa kuwa upinzani wa kweli utatoka ccm? so, inawezekana ndoto ya mwl ndo inatimia. Yetu macho. tusubiri tuone.
 
Tusubiri mkuu,hata hao kina Invisible wakiamuwa kujitokeza tutawasapoti kwa nguvu zetu zote....Hivyo ondoa shaka mkuu,hayo mambo ya cc yasikupe shida sana,this time inaelekea itakuwa kati ya ccJamii na ccMafisadi...Kaazi.

Isije kawa Rev. wetu kafanya mambo tayari? ngoja niitafute ile thread........!
 
tanzania akuna upinzani,. upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm alisema nyerere
 
tanzania akuna upinzani,. upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm alisema nyerere

Wakati mwingine tunapaswa tumia japo sehemu ndogo ya muda wako kujifikirisha zaidi ya yale yaliotoka kinywani mwa mtu mwingine. Upinzani, unapinga nini na kwanini unapinga? Alichomaanisha nyerere sio unachokisema hapa! Mbona wengi wa viongozi wa upinzani waliwahi kuwepo cmm? Alichomaanisha nyerere ni kuwa upinzani utashamiri pale dola itakapoachana na ccm, jiulize ni lini na ni kwa vipi, na wewe unaweza kushiriki vipi?

Jiulize maswali mepesi, mwaka 1995 Nyerere aliacha ghafla kampeni ya Mkapa mkoani kilimanjaro akakimbilia Zanzibar kwenda kumtangaza Komandoo rais, na hapohapo wiki chache wakafuta matokeo ya majimbo mbalimbali ya uchaguzi ikiwemo karibia Dar es salaam yote. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu ya wapinzani ndani ya ccm?
 
Wakuu zangu Kikwete hana wakati mgumu ktk uchaguzi huu...Atapita kiulainiiiiii....Hilo la kumtakjia kushindwa ondoeni kabisa akilini, isipokuwa kuna viongozi wengi sana wameshajua kwamba hawatarudi ktk Uongozi na nafasi yao ya Ubunge imekwisha ota magugu kutokana na uwakilishi wao huko wanakogombea miaka yote.

Hawa watu hawawezi kupita uchaguzi wa ndani wa chama ambao ni mgumu sana kwao. Kwa kuelewa hivyo na sii kwa uzalendo wao kwa nchi hii wamejipanga kujitoa wakijua fika hawana nafasi ndani ya CCM.

Hawa watu ni wanafiki tu, hakuna kigogo hata mmoja ndani ya CCM ambaye ni mzalendo wa kweli kwani asingeweza kuwa kigogo pasipo kuiba na kujiweka ktk nafasi ya kuitwa kigogo...FEDHA ndio msingi wa mafanikio yao na sasa ngoma nzito hawana pa kutokea isipokuwa kujiunga na chama kingine ama kubahatisha ktk vyama vya Upinzani.

Ni muhimu sana mfahamu kwamba malengo yao sii mapungufu ya Utawala uliopo kwani wao ndaio hasa sababu ya mapungufu haya, hivyo kuja kwao na chama kipya ama hadithi mpya haina maana wanalo JIPYA na la maana. Wanakuja kwa sababu wanaangushwa ndani ya CCM, hatima yao imefika hivyo kabla hawatupwa nje wanatafuta mbinu mpya kulinda maslahi yao. JK kawapa mtihani mgumu sana kupita uchaguzi wa ndani kuchaguliwa na wananchi wanachama wa CCM na sio tena jina la mgombea kupitishwa na kamati ya chama.

Tuwe wepesi kusoma alama za wakati...
 
wamejipanga kujitoa wakijua fika hawana nafasi ndani ya CCM.

Hawa watu ni wanafiki tu, hakuna kigogo hata mmoja ndani ya CCM ambaye ni mzalendo wa kweli kwani asingeweza kuwa kigogo pasipo kuiba na kujiweka ktk nafasi ya kuitwa kigogo...FEDHA ndio msingi wa mafanikio yao na sasa ngoma nzito hawana pa kutokea isipokuwa kujiunga na chama kingine ama kubahatisha ktk vyama vya Upinzani.

Ni muhimu sana mfahamu kwamba malengo yao sii mapungufu ya Utawala uliopo kwani wao ndaio hasa sababu ya mapungufu haya, hivyo kuja kwao na chama kipya ama hadithi mpya haina maana wanalo JIPYA na la maana. Wanakuja kwa sababu wanaangushwa ndani ya CCM

Whatever the reason ya kujitoa sisi tunachotaka ni CCM kumeguka tu kwanza hatujajua ni kundi lipi ndio litatoka lile la mafisadi au wapinga mafisadi au la mtandao watakapojitenga ndipo tutajua wanafiki ni wapi.
 
hiii ni nzuuuri tena saaana lakini nyie wenye mawazo yenye utindio wa ubongo tunawaomba msitulee habari za kukatishana tamaa chama ndo hilo kiujumla tanzania nzima ni majangili watupu ushahidi ninao kama mnataka nipelekeni mahakani na kesi nashinda anapotokea mwenye afadhari wengine wanaanza oooo propaganda tu sijui nini mala heee ondokeni zenu na magonjwa yenu ya kukariri hayo sisi hatuko kule kwa samaki mmoja akioza wote wameoza, no tupo kwenye ukisikia harufu mbaya mahali ulipo hamia pengine nyie bakini hivyo hivyo tu, haiwezekani unapiga kelele tu houondoki huo ni uhuni
 
Wakati mwingine tunapaswa tumia japo sehemu ndogo ya muda wako kujifikirisha zaidi ya yale yaliotoka kinywani mwa mtu mwingine. Upinzani, unapinga nini na kwanini unapinga? Alichomaanisha nyerere sio unachokisema hapa! Mbona wengi wa viongozi wa upinzani waliwahi kuwepo cmm? Alichomaanisha nyerere ni kuwa upinzani utashamiri pale dola itakapoachana na ccm, jiulize ni lini na ni kwa vipi, na wewe unaweza kushiriki vipi?

Jiulize maswali mepesi, mwaka 1995 Nyerere aliacha ghafla kampeni ya Mkapa mkoani kilimanjaro akakimbilia Zanzibar kwenda kumtangaza Komandoo rais, na hapohapo wiki chache wakafuta matokeo ya majimbo mbalimbali ya uchaguzi ikiwemo karibia Dar es salaam yote. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu ya wapinzani ndani ya ccm?

Pamoja.
 
Back
Top Bottom