Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Delusion?

who thinks CCM will split so easily like that? they learned from Mrema!

Opposition parties; many people are excited by CCJ because 'you are not alive'!! no one would ever think to form CCJ if the existing opposition parties were 'full of life'!

sijamuona yeyote CCM mwenye uwezo wa kuchomoka!
 
Dr Benson Bana of the UDSM Political Science Department said experience had shown that "no influential politician can survive politically outside the ruling party".
.
Huyu Bana nae haishi viroja sasa kwa experience gani mbona vyama vyenyewe vimeanzishwa 1992 na vingine bado vinaanzishwa! na influential politician gani ashakwenda upinzani? Mrema peke yake anatosha kuleta conclusion hii..??
 
Wandugu, tunaomba CV za waanzilishi wa CCJ huyo Mr. Kiyabo na mwenzie, wametokea wapi, shughuli zao nje ya siasa nini, n.k

Maana tukiwafahamu kwa undani, ndio majadiliano yatanoga kujua kama wana ubavu au wamewekwa kama boya tu.
 
Wakati ule Rais Mwinyi alimfukuza Mrema kutoka CCM,halafu Mrema akaingia NCCR,halafu CCM ikapata msukosuko. Sasa hivi,Ali Hassan Mwinyi anajitayarisha kufukuza watu wengine kutoka kwenye Chama. Who is to say History will not repeat itself?
Lakini certainly CCJ ni distraction,kwa sababu badala ya viongozi wake kujitokeza,wanajificha,na kusababisha mental speculation,ambayo ni polluting the atmosphere.

Mkuu ganesh, Mrema hakufukuzwa CCM alijiengua mwenyewe kwa hiyari yake baada ya kufukuzwa kazi ya Uwaziri na Bosi wake(Rais Mwinyi) wakati huo. Ila kilichotokea 1995 hakitaweza tokea tena kwani Strategist wameshapata muda wa kupanga mbinu za kuiba kura. 1996. Ilikuwa hatari sana kwa CCM kwani ilikuja ghafla yaani ni kama "Kuku kampiga Nyau" vile.
Under free and fair election vyama vya upinzani bado ni tishio. Hivi unajua hivi sasa mojawapo ya kazi za TISS ni kuhakikisha CCM haishindwi?, hasa upande wa Rais?.
 
Hawa waanzilishi wa CCJ (wadhamini/viongozi wa muda) Mr Richard Kiyabo (chairman) and Mr Renatus Mubhi (secretary-general) CV zao izingeletwa hapa ktk forum.

Maana nia na madhumuni yao ni kuchukua nchi kwa njia za kidemokrasia, yaani kwa kifupi kuwashinda CCM, CHADEMA, CUF na kuongoza Tanzania yetu.

Nimesoma magazeti yote kama The Guardian, Tanzania Daima, HabariLeo n.k hakuna wasifu wa hawa jamaa waliochochea gumzo jipya kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Nimeona picha zao, lakini wametokea wapi, wame-'achieve' nini mpaka sasa hivi nje ya siasa n.k Maana nchi nyingine ukiibuka kutaka kuchukua dola lazima wasifu wako uchambuliwe kwa kina.


Naomba kuwakilisha hoja.
 
Utaomba vipi CV za watu ambao bado hawajayaweka majina yao wazi?
 
Utaomba vipi CV za watu ambao bado hawajayaweka majina yao wazi?

Kama ni mwenyekiti na katibu majina yao yapo wazi! Mwenyekiti ni Bw Richard Kiyabo na Katibu ni Bw Renatus Muabhi. Tunaambiwa hawa ni wa muda. Hope chama kikipata usajili wa kudumu watachagua mwenyekiti na viongozi wengine kwa mujibu wa katiba yao.

Binafsi sikuwahi kuyasikia majina haya kabla katika nyanja yoyote ile!
 
Hawa waanzilishi wa CCJ (wadhamini) CV yao ingeletwa hapa ktk forum.

Maana nia na madhumuni yao ni kuchukua nchi kwa njia za kidemokrasia, yaani kwa kifupi kuwashinda CCM, CHADEMA, CUF na kuongoza Tanzania yetu.

Nimesoma magazeti yote kama The Guardian, Tanzania Daima, HabariLeo n.k hakuna wasifu wa hawa jamaa waliochochea gumzo jipya kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Nimeona picha zao, lakini wametokea wapi, wame-'achieve' nini mpaka sasa hivi nje ya siasa n.k Maana nchi nyingine ukiibuka kutaka kuchukua dola lazima wasifu wako uchambuliwe kwa kina.


Naomba kuwakilisha hoja.

ili iweje
 
Wandugu, tunaomba CV za waanzilishi wa CCJ huyo Mr. Kiyabo na mwenzie, wametokea wapi, shughuli zao nje ya siasa nini, n.k

Maana tukiwafahamu kwa undani, ndio majadiliano yatanoga kujua kama wana ubavu au wamewekwa kama boya tu.
Ili nini mkuu?
 
Kuna mawazo na propaganda kuwa eti CCJ ni chama ambacho kimesheheni Vigogo wa CCM.
Huu si ukweli.
Ukweli ni kwamba CCM iko pale pale na vigogo wake bado wako ngangari ndani ya CCM.

CCJ ni chama kilichoanzishwa ili kuwachanganya wapinzani wadhani kuwa CCM imekuwa dhaifu.

Wapinzani wakawaza kuwa CCJ ni mgawanyiko wa CCM, basi watashindwa kirahisi na CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Wapinzani unganisheni nguvu zenu badala ya kupumbazwa na CCJ kisha mkalala usingizi.

Natoa hoja.

Unachosema kina ukweli kwasababu ebu angalia;Hiki chama kina usajili wa muda,na inasemekana kinaweza kisiwe na usajili wa kudumu coming election day,lakini tizama kinavyopoteza muda wa watu tayari,eye already off the ball...
 
ili iweje

Nia na madhumuni ya kuwafahamu kwa undani ili kuona kama ni watu wanaofaa au ni watu wa dhihaka, utani n.k sije tukapoteza muda na wakati kushabikia kitu ambacho ni serious ktk kuchukua dola kwa njia za kidemokrasia. Forum hii iwe kichocheo cha 'vetting' ya potential presidential candidates, tusisubiri wengine, maana mpaka sasa magazeti kazi hiyo imewashinda

Sarah Palin wa republican alijadiliwa kwa mapana na marefu, Barack Obama nae alijadiliwa kwa mapana na marefu. Sarah Palin alikuwa gavana wa jimbo la Alaska na ni graduate akaulizwa swali la chemsha bongo: Unafahamu kazi za Federal Reserve : akajibu ni Jeshi la Akiba : wakati Federal Reserve ni Benki Kuu ya Marekani na kazi zake ni kusimamia masuala ya mabenki na fedha.

Hivyo hiyo ndio nia kuu ya tread kuwafahamu mwenyekiti wa muda na katibu wa muda waanzilishi wa CCJ.
 
Mkuu wanatumika tu. Na kwakua ni viongozi wa muda na ukizingatia haihitaji mtu kuwa na CV ndeeefu ili aweze kufungua chama cha siasa wala haihitaji sana kuwajua hawa.Maana soon watatoweka na hutakaa uwasikie tena kwenye medeni za siasa. Hawa ndo kama waleee akina Wiliam Francis wa Kagoda so ni mtindo ule ule wa kifisadi walotumia CCM ndo wameuingiza hapa kufungua chama.

Nyuma wapo wenye chama chao ambao ndio wanaoendesha na kusimamia zoezi hili. muda ukifika hawa kina sijui Kanyaboya hutawasikia. watakuja wenyewe watachukua chama na mambo yatasongeshwa.

Sasa sijui ni woga wa hao walio nyuma yao kujitokeza, au ndo tabia ya ufisadi na kupandikiza mamluki ikishakuingia huwezi kuacha.

Yetu macho
 
Kitu kilichokuwa kikinisumbua siku zote, ni kujua majina ya hawa waanzilishi wa CCJ. Niko na butwaa............

Warioba aacha ‘maswali’ CCJ

Chanzo: HabariLeo


TUHUMA za kuwepo kwa wanasiasa waandamizi na wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga kujitoa katika chama hicho tawala na kujiunga na chama kipya wanachodaiwa wamekiandaa kinachoitwa Chama Cha Jamii, zimeendelea kutoa sura tofauti miongozi mwa wanasiasa hao.

Wakati juzi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Mtera, John Malecela alikanusha vikali kuhusika na uasisi wa chama hicho, jana Habari Leo liliwapata viongozi wengine waandamizi wanaotuhumiwa kuazisha chama hicho ambao hawakuthibitisha kuwa miongoni mwa waasisi wa chama hicho wala kukana tuhuma hizo.


Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba alizungumza na Habari Leo kuhusu tuhuma kwamba yeye ni mmoja wa mawaziri wakuu watatu wanaotuhumiwa kuunda CCJ, alisema hawezi kuzungumzia chochote kuhusiana na madai kuwa yeye ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho.


“Siwezi kusema chochote kuhusiana na taarifa zinazosambazwa na mtu asiyejulikana,” alisema.


Aidha Waziri Mkuu huyo wa zamani alishauri mwandishi wa habari hizi kuwasiliana na uongozi wa CCJ kuhusiana na shauri hilo.


Habari Leo lilimpata mwanasiasa mwingine mkongwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na kumuuliza iwapo anahusika na uanzishwaji wa chama hicho, kama ilivyo katika waraka wenye tuhuma hizo na yeye alisema hajaona nyaraka zinazomuhusisha yeye na CCJ.


“Sijaona nyaraka hizo,” alisema Butiku na kukataa kuendelea na mahojiano na mwandishi wa habari hii hata baada ya kuhakikishiwa kuwa waraka huo upo.


Mwandishi wa habari alitaka kujua kama mwanasiasa huyo alikuwa ameona nyaraka za chama hicho na kama ana maoni yoyote kuhusiana na madai kwamba anahusika katika kuiasisi CCJ.


Kuomba usajili kwa chama hicho kipya cha siasa kumezua maswali mengi miongoni mwa watu kadhaa wakiwemo wanasiasa kutokana na madai kuwa viongozi wakubwa wa CCM wamekiandaa na wanapanga kujiunga nacho kwa nia ya kuiangusha CCM katika uchaguzi mkuu ujao.


Tayari Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba ametoa kauli kuwa CCJ hakiwatishi huku Katibu wa Uenezi wa Kamati Kuu ya CCM (NEC), John Chilighati akisema kuwa watakaotoka CCM, watakuwa wamejimaliza wenyewe.


Licha ya viongozi hao waliokwisha zungumzia CCJ, viongozi wengine wanaodaiwa kuhusika nacho ni pamoja na kundi la wabunge wanaojipambanua kuwa makamanda wanaopiga vita rushwa.


Kutokana na misimamo ya vigogo hao wanaotuhumiwa kutaka kujiunga na chama hicho, ilidaiwa pia kuwa vigogo hao wameandaa kongamano la kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere, litalaotumika kama uwanja wa kukitangaza chama hicho.


Kongamano hilo limedaiwa kuwa lingefanyika kwa mgongo wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Aford ambayo haijapata usajili lakini lengo lake likiwa kutoa ishara za awali za chama hicho cha CCJ.


Habari Leo lilifanikiwa kumpata kiongozi wa taasisi hiyo ya Aford, Julius Miselya ambaye alianza kuvishutumu vyombo vya habari kwa kutumia vibaya jina la taasisi yake kuisakama serikali ya Rais Jakaya Kikwete.


“Ni nyie waandishi wa habari mnaosambaza taarifa hii inayotoka kwa mtu asiyejulikana na kuleta mtafaruku nchini,” alisema.


“Mimi sifungamani na chama chochote, nimewatambua watu wanaojihusisha na CCJ kwa kusoma magazeti asubuhi hii,” alisema Miselya.


Amesema kongamano hilo ambalo bado lipo katika maandalizi limeibuliwa kwa waandishi wa habari kwa lengo la kupotosha ukweli.


“Muulize Waziri Mkuu kama amethibitisha kushiriki, sitazungumzia kitu hicho,” alisema. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ametajwa katika waraka huo kuwa ndiye atakayefungua kongamano hilo.


Alipohojiwa kama kongamano hilo litaendelea kama lilivyopangwa, alisema kwamba hatasema chochote kwa vyombo vya habari.


Baadhi ya viongozi wa CCM waliounganishwa na uanzaji wa chama kipya cha siasa nchini walipoulizwa walisema kwamba ndio kwanza wanajua kuwa kuna chama kipya.


Mwanasiasa mwingine aliyehusishwa na chama hicho kipya na kukanusha ni mbunge wa Maswa, Magale Shibuda.


Juhudi za gazeti hili kupata maoni ya wahusika wengine zilishindikana jana na bado zinaendelea.


Juzi Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, aliliambia Habari Leo kuwa chama hicho kipya kina safari ndefu kwa kuwa taratibu za kusajili chama huchukua muda.


Alisema licha ya chama hicho, tayari kuna vyama vingine vingi ambavyo vinasubiri kupewa usajili na kuongeza kuwa huenda CCJ kikapata usajili wa muda kabla ya Machi mwaka huu.
 
Wakimbilie CCJ ama wabaki CCM watu kibao watapigwa chini mwaka huu!
 
.Hapa kuna harufu ya usalama wa taifa kupitia vyombo vyake vya ndio mzee kama TBC1, habari leo nk, kujaribu kudodosa ni nani wako nyuma ya ccj. Hoja wanazotoa kwa wale wanaodhaniwa kuwa nyuma ya chama hazina mashiko, ni dhana tu, hawa waandishi wanaowasaili watuhumiwa hawasemi ni nani anatuhumu na wapi alifanya hizo tuhuma. Ama kweli ccj japo haijatoa kichwa chake lakini kiwiliwili chake kimekuwa tishio na jinamizi lililouondoa usingizi wa ccm.
 
.Hapa kuna harufu ya usalama wa taifa kupitia vyombo vyake vya ndio mzee kama TBC1, habari leo nk, kujaribu kudodosa ni nani wako nyuma ya ccj. Hoja wanazotoa kwa wale wanaodhaniwa kuwa nyuma ya chama hazina mashiko, ni dhana tu, hawa waandishi wanaowasaili watuhumiwa hawasemi ni nani anatuhumu na wapi alifanya hizo tuhuma. Ama kweli ccj japo haijatoa kichwa chake lakini kiwiliwili chake kimekuwa tishio na jinamizi lililouondoa usingizi wa ccm.


Nadhani wanahisi. Kila mtu kwako wanaona yuko nyuma ya CCJ. Nahisi itafika mahali hata mawaziri watachomekewa.
 
Yawezekana kuwa hizi ni blah blah za mtu aliyetaka kuwapa watanzania cha kujadili na kusahau masuala ya msingi zaidi?

Tafadhali angalia hata Mheshimiwa Tendwa mwenyewe kasema Ni Hoax tu:

01_10_nt0rqj.jpg
 
ABDULWAKIL SAIBOKO,
25th January 2010


THE much-publicized new political party, Chama Cha Jamii (CCJ), is nothing but a mere hoax, the Registrar of Political Parties, Mr John Tendwa, said in Dar es Salaam yesterday.

"It is disgusting to see news in the media about a party which does not exist at all. Some people have gone to the extent of claiming that the party has been given temporary registration.
This is not true. It is a hoax," he said.

Mr Tendwa said that
the whole issue was being blown out of proportion by some politicians, for reasons better known to them.

"I am tired of talking about this ghost party. In fact,
even if it existed, there is nothing special that could make it unique or different from all the other registered parties. Why should it merit such publicity? Who are the party (CCJ) members anyway?

"
We are drawing too much attention for nothing. Nothing at all," he said. There has been a series of news on the local media about the party, which has been claimed to have been backed by veteran politicians from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM).

The suspected veteran politicians, however, have distanced themselves from it.


Unconfirmed reports had it that the party was registered early last week. The reports drew mixed reactions from a cross-section of people, including politicians.


CCM leaders said the new party did not pose any threat to the ruling party's existence. One tabloid went further to claim that the party (CCJ), would parade a presidential candidate to challenge President Jakaya Kikwete in the coming October general elections.


The man who identified himself as the
chairman of CCJ, Mr Richard Kiyabo, was quoted as saying that the major target was to have a presidential candidate in this year's general elections and that the party had 2,000 members in Dar es Salaam so far.

However, Mr Tendwa said that even if the party had applied for registration, it still did not deserve such publicity. The Registrar said that normally registration of a new political party takes time before it can be allowed to operate.


"There are many applications for registration of new political parties, but these are still pending. They could be accorded provisional registration by March," he said. He fell short of saying whether legal action could be taken against the new party leaders.


Meanwhile, Mr Tendwa announced the revocation of the provisional registration of People's Democratic Movement (PDM), an opposition political party, for failure to meet legal obligations.


He said that the party, led by Mr Joseph Minja, has been revoked for failure to abide by Political Party's Act no. 5 of 1992, which demands that a party should have more than 200 members for each region from 20 regions.


Meanwhile, another political party, the Democratic National Congress (DNC), has been denied extension of provisional registration.


The same law states that provisional registration of a political party should not exceed 180 days. DNC was seeking extension for the third time which exceeds the deadline. The party was registered in 2008.

Source: Daily Newshttp://www.dailynews.co.tz/home/?n=6984&cat=home
 
CCM itapasukia ZANZIBAR sio huku Bara. CCJ ni porojo tu za ku-divert attention yetu toka kwenye mambo muhimu ya kitaifa.
 
Sawa sawa mkuu, ila uana mapinduzi wa kweli sometimes ni risk taking are we together on this?

Ninakubaliana na wewe lakini inatakiwa risk analysis iwepo inayoonesha bayana kila jambo na faida na athari zake kabla ya kujitosa.
Mambo ya kwenda kichwa-kichwa kwa karne hizi hayana nafasi, kila mtu atawajibika zaidi kwa maamuzi na matendo yake.
 
Back
Top Bottom