Sikizeni wandugu,Nusu kijiko wa Lumumba kwenye ubora wako
Ndo nilikua namuuliza uyu mleta uzi maana kaonesha ushabiki tuKatika nchi hii ambayo ni "Police State", unategemea chama tawala "kigundulike" kuwa na makosa?
Wewe ni wa kupuuzwa na kuhurumiwa tuHakitafutwa bali kitajifuta tu kwa uamuzi wao huu.
Mgonjwa yupo ICU tunasubiri kuzima Machine ya nini kumkorogea sumu kujipatia dhambi?!
umenichekesha sanaHakitafutwa bali kitajifuta tu kwa uamuzi wao huu.
Mgonjwa yupo ICU tunasubiri kuzima Machine ya nini kumkorogea sumu kujipatia dhambi?!

Massa 48 unatupia watu lupango. Hahahaha hata kama utatumwa lkn jiji utalijua vizuriNa kifutwe ru kwani kina faida gani?
Wanabodi,
"Chama Cha Wananchi CUF, Kufutiliwa Mbali!... Iwapo Itathibitika Kinahusika/ Kitahusika na Vurugu, Ugaidi, Uvunjifu wa Amani Zanzibar na TZ!.
Nyingi ya theads humu ni threads kuhusu matukio yaliyotokea, lakini tuna threads chache sana kuhusu mambo yatakayokuja kutokea, hivyo hii ni thread ya mambo yatakakuja kutokea kutokana na kitu kinachoitwa "trend readings" na sio utabiri kama wa Sheikh Yahya (RIP) au Nostra Damas.
Trend ni inahusiana na usomaji wa historia ya kilichowahi kutokea nyuma, kulinganisha na kinachotokea sasa, ili kujua kitakachokuja kutokea huko tuendako.
Kichwa cha habai kimejieleza wazi kuwa Chama cha Wananchi CUF, kitafutwa rasmi (toka kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya Siasa), kama itathibitishwa pasipo shaka,without any reasonable doubt, kuwa kinahusika, au kitahusika na matukio yoyote ta kihalifu, ya kigaidi au ya uvunjifu wa amani, Zanzibar, Pemba au eneo lolote la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu kitakuwa kimepoteza sifa za kuitwa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992! ambayo kisheria inajulikana kama The Political Partie Act of 1992 au Chapter 258.
Sheria hiyo imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa kinachoweza kusajiliwa, lakini pia imeweka sifa mbali za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajili, na miongoni mwa sifa ambazo chama cha siasa hakiwezi kusajiliwa, ni pamoja na kipengele hiki kwenye ibara ya 8, 2-c
"it accepts or advocates the use of force or violence as a means attaining its political objectives"
Ibara hii inamaanisha kama chama kiliishasajili, lakini baadae kikagundulika kina kiuka kipengele hicho, kinakuwa kimepoteza sifa hivyo kinastahili kufutwa kutoka kwenye daftarri la msajili.
Viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CUF, msije kunirikia kuwa nawawangia au kuwachuria chama chenu kifutwe, bali nawapa tuu angalizo la matakwa ya kisheria, ikiwa na endapo itathibitishwa pasi shaka, "beyond reasonable doubts" kuwa CUF kama chama, kinahusika na kupanga, kuratibu na kutekeleza vitendo vyovyote vya kihalifu, vya kigaidi na vya kuvuruga amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar na Pemba ambazo ni sehemu za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ni kufuatia CUF kususia kushiriki uchaguzi wa marudio, hivyo kimesusia na kupanga vurigu, uhalifu na ugaidi ili uchaguzi usifanyike, kama huo ndio mpango wenu, endeleeni na mipango hiyo, lakini huku mkijiandaa kufutwa rasmi!.
Ili ikikutikana wanaofanya vitendo hivyo ni wana CUF individually bila uhusika au uatibu wowote wa CUF kama chama, CUF kama chama, kitabaki salama, na hao wanachama, watashughulikiwa kama wahalifu wengine wowote kwa sababu uhalifu ni uhalifu tuu, hauna chama, hauna dini, hauna kabila, hauna rangi wala jinsia, uhalifu ni uhalifu tuu, na wahalifu wote ni watu wa kulaaniwa na sheria ichuke mkondo wake dhidi yao!.
Sheria zipo lakini hazitekelezwi, ila kufuatia JK kuwa dhaifu, na serikali yake kuwa dhaifu, kuliwapa wahalifu mawanda ya kutamba hadi kumchea simba sharubu na hakufanya lolote, hizi nyakati sasa zimebadilika, nyie mliozoea kuchezea sharubu za simba dhaifu, msijaribu kuchezea sharubu za huyu aliyepo, huyu sii yule mtu wa kucheka cheka na ngedee na kuyavuna mabua!, sasa nyakati zimebadilika, hili ni angalizo tuu nawapa, mlipokee au mlipuuzie, yakitokea ya kutokea, msilalamike kuwa hamkuambiwa!.
Naombeni msije kunisdhutumu kuwa ninachuki na CUF, maneno kama haya ninayowaeleza leo, pia niliwahi kuwaeleza wenzenu na washiika wenu Chadema, na pia niliwahi kuyatoa kwa chama dola CCM!.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa ...
Tuhuma Hii: CHADEMA Kuendeshwa Kwa Katiba "Fake" Ikithibitishwa ...
Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio ...
Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile ...
Wasalaam.
Pasco wa jf!.
andika vizuri nyau alafu kalambe viatu kisha kachukue buku 7 zako kisha tafuta mwanamke kijana sio huyo na karibu sana mkoani.Na kifutwe ru kwani kina faida gani?