Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Mimi napita tu cuf ndio chama pekee has a kwa Zanzibar kinacho kubalika na ndio kilicho shinda uchaguzi sasa mbinu tu tens zakitoto dunia mzima inajuwa ccm ndio chama cha Fujo na uvunjifu wa amani Pemba watu wametulia wanafanya shughuli zao lakini kwa makusudi ccm wamepeleka mazombi wakaanza kupiga watu na kutia moto Nyumba sasa kama uchaguzi si wamtangaze sheni kuwa rais sasa kupiga watu dah Africa kweli tumeumbwa kuwa watumwa tu kazi tunayo iweza na kuuwana na kucheza ngoma

Bibie tunapojadili haya mambo tujifunze kuweka ushabiki pembeni.

Wewe umewaona hao Mazombie tu?! Vipi hawa wanaochukua mabomu na kwenda kulipua kwenye nyumba za wakuu wa usalama? Vipi hawa wanaochoma ofisi na nyumba za wanachama wa CCM, hawa huwaoni, au ushabiki umekutia upofu?
 
Kiukweli tunatatizo kubwa la uono na uelewa, mimi ni mwana fasihi, hivyo naelewa fika unapokuwa mkweli daima bila kuegemea upande wowote, utachukiwa na kuwa an enemy of the people, hili ni bandiko langu la 17,616 na hakuna hata bandiko langu moja ninalohubiri chuki na kikweli kabisa kusema kweli kwangu kumewahi kuniponza mara chungu nzima na kunikosesha opportunities kibao, lakini ukiwa mkweli toka ndani ya moyo wako, unakuwa gratified kwa kusema kweli, na hata ikibidi kulala njaa, unalala njaa smiling, kama kozi mwana Mandanda, kulala njaa kupenda!.

Kama Masiya alikuja kwa ajili ya Wayahudi na wakamsulubisha, nitakuwa mimi ninaowaeleza ukweli magaidi?!.

Pasco

Teh teh teh.
Leo msukuma Pasco mwandisho asie na Fani anajilinganisha na Masiyah!
Duh..
Kazi ipo.

Masiyah alikuwa na LENGO na Mission aliyotumwa kuikamilisha.
Wewe pangu pakavu Mission yako nini? Zaidi ya kusambaza Unafiki tu.?

Ukweli upi unatoa hapa km Sio story za Kubumbabumba?

Kamata shahada japo moja ya maana at least tujue una kitu cha maana.
Sio kugaa gaa na upwa ovyo.
 
Hakuna mjinga mjinga yeyote anaeweza kuifuta cuf .kwanza cuf sio chama cuf ni nchi ya zanzibar

Kwa hiyo kama unaweza kuifuta nchi ya zanzibar hapo ndio unaweza .cuf sio makaratasi kama unavozani cuf ni rai wote wa zanzibar .maalim seif kafanikiwa kutawala nyoyo za wazanzibari .

Mfalme wa kweli ni yule anaetawala nyoyo za raia wake na wala sio wanaotawala raia kwa vifaru .

Wewe ni sehemu ya wale m.mungu aliowapa jina la "mufsiduna fil ardhi " ni wanaoleta ufisadi katika ardhi .hakuna aliedhani siku moja east timor ingepata uhuru wake kutokabindoneshia .

Asie na dola ana mungu .

Pauliwapo nyoka hapokosi muombezi .

Nadhani wewe ni katika wale unaodhani hayo mambo yanayoendelea znz yanaijenga zanzibar .

Wewe na ccm ni waoga na hamewezi changamoto ya upinzani wa kweli .

Ukweli nibkwamba mnasaidiwa na mambo mawili ndio mana mtu jama ww unakua na mdomo mrifu

1) katiba na sheria kandamizi za uchaguzi

2) vyombo vya dola
Mkuu wamshambulia bure,
Pasco katoa maoni yake juu ya kile kinachoendelea Znz.
 
Mkuu Pasco ni Opportunist au mchumia tumbo kama wachumia tumbo wengine kina Mwanakijiji. Baada ya kuona nguvu ya Lowassa tangu yuko CCM na baadae kuhamia CDM alidhani kuwa angeshinda uraisi. Hivyo alijipanga kuwa upande wake Kwa kuandika mfululizo WA threads za kumsifia Lowassa na kueleza kuwa UKAWA ndo chaguo sahihi. Pitieni humu JF mtaona threads hizi. Na kweli alipata wengi wakumuunga mkono katika wapinzani na wengi wa kumponda toka CCM.
Sasa baada ya kuona upepo umebadilika na CCM ndo imeshinda amekuja na gia nyingine ya nitoke vipi kwa kuponda upinzani na kufagilia CCM na Magufuli.
Mtaona kuna complete u turn kwenye misingi ya hoja zake. Amepoteza mvuto na sio yule critical thinker tuliyemjua kabla ya uchaguzi.
Hivyo Mimi sishangai kuona watu Hawa maana anaagalia Maslahi take zaidi anaweza kuwa manipulated kirahisi tu.
Mkuu Kikwebo, kwanza asante opinion yako kwa sababu everyone has the right to his opinion.

Tangu nimejiunga jf, siku zote nimekuwa nikisema mimi sina chama ila kuna watu ninawakubali sana, na miongoni mwa watu hao ni El. Sijawahi kuwa CCM lakini nilimkubali EL akiwa CCM na nimeendelea kumkubali akiwa UKAWA lakini sijawahi kuwa Chadema wala UKAWA japo nimewaunga sana tuu mkono!. Ndani ya Chadema nimekuwa nikimkubali sana Zitto, Zitto amehamia ACT, nimeendelea kumkubali na sijawahi kuhamia ACT. CUF namkubali sana Jusa na sijawahi kuwa CUF.

Tofauti na wana jf wengi wana vyama, wana kambi na mirengo, mimi sina chama, sina kambi sina mrengo bali ni ukweli tuu!. Wapinzani wakifanya madudu sipondi bali nasema haya ni madudu na huo ndio ukweli wenyewe!. CCM wakifanya madudu sipondi bali naeleza kuwa ni madudu, tofauti na wengine, CCM wakifanya mazui nasifu, na wapinzani wakifanya mazuri pia nasifu.

Magufuli!.
Toka Magufuli hata kabla hatateuliwa na CCM, mimi ni miongoni mwa wana JF tuliosema ni Magufuli and not by chance but a pre meditated move and for a reason!. Jee wewe hapo ulipo unajua kwa nini ni Magufuli how, and why?!. Kanisome hapa angalia bandiko ni la lini!
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli...

Alipoteuliwa tuu na CCM, nilieleza msimamo wangu kuhusu Magufuli na kutoa ushauri kwa Lowassa.
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Baada ya kutangazwa mshindi, nilitoa tena ushauri.
ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote ...
Licha ya Magufuli kushika nchi, kwenye mazuri tunampongeza na kwenye madudu pia tunamwambia ukweli.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...

Hili la kuitana wachumia tumbo nimelizoea, sijawahi kula hata senti tano ya Lowassa wala sijawahi kulipwa hata senti moja kwa kuandika jf. Mimi kazi yangu ni mwandishi wa habari wa kujitegemea for the love of it, not for the gain from it. Napenda kuandika, so doing what you love makes you happy hata kama you don't make a penny or gain!. Bora kuwa masikini mwenye furaha na amani kuliko tajiri mwenye mashaka!.

Ukweli unasifa moja kubwa, husimama mpaka mwisho.

Nimesimama!.

Pasco
 
Mkuu Tetty posti ya msajili wa vyama inashikwa na mtu mwenye cheo cha Jaji. Majaji sio wanachama wa vyama, japo Tendwa aliegemea saba CCM, Jaji Mutungi namfahamu vizui ni mtu muadilifu na non partisan!.

Ila pia huu mtindo wa wajaji na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kujiunga CCM wanastaafu, kunatia mashaka na uwezekano walikuwa CCM kabla!, tumemuona Jaji Ramadhani japo alidhalilika ila angalau tumejua!. Harakati za Apson pia zilijulikana, hivyo ni kweli kabisa unaweza kukuta Mwamu nae ni CCM!, Othmans wote wawili ni CCM, inawezekana hata Muf.i na 'Jino' pia nao ni CCM, sasa nani atakuwa sio CCM?!. Kwa muktadha huu, CCM itatawala milele!.

Pasco

Shemeji hongera sana kwanza naona Wasukuma mmekuja juu kwenye Siasa,nimeona na Shemeji mdogo Dr.Vicent naye ndiyo Muongoza ligi ya Chadema hongera kwa hilo.Hope umemuandalia kasherehe kafupi kwa kumpongeza na kumfunda.

Shemeji yangu asili ya Wine haiishi kwa kuwekwa kwenye chupa ya soda au bia,bado inakuwa wine.

Majudge wote ni wanaCCM hilo hakuna wakulipinga.Hili ni pamoja na wanajeshi na Polisi,maana tumeona hata kada wa CCM akipiga filimbi ya kama ta mpinzani,apigwe tu basi mpinzani ataipata fresh,ataswekwa ndani,atapigwa au hata kuuawa na akisha uawa hakuna kesi bali aliyeua anauhakika wa kupanda cheo.

Kwahiyo Shemeji yangu tusikimbie mvua sababu inatunyeshea tunatakiwa kulikimbia jua maana likipiga sana linaleta njaa.Nakutakia siku njema.
 
Sioni tija wala mantiki ya huu uzi
Mkuu Ulokwi, mimi huwa nikikutana na uzi ambao hauna tija wala mantik, huwa naupotezea, sipotezi muda wangu kusoma vitu visivyo na tija na mantiki, hivyo nakushauri next time, save you time, kwa sababu time is money, ikipita imepita!.

Pasco
 
Kwa nini CUF na sio CCM?Kwani CCM hawawezi kuwa nyuma ya hizo fujo na matukio ya Kifaidi? Lengo ni nini kuanza kunyooshea kidole CUF na si Ccm? Kukataa Uchaguzi wa marudio ni jinai? Wamewaachia ccm na vibaraka wake waendelee na uchafuzi wao, wao wamekaa pembeni, ya nini kuwachokoza?
Kuifuta CUF gharama yake ni kubwa zaidi ya hicho mnachokifikiri. Haihitaji PhD kung'amua kuwa, MABAVU HAYASAIDII, maelewano na Maridhiano siku zote hujenga Umoja wa Kitaifa! Majeraha kwenye Kiini cha Moyo wa Utaifa yatafutiwe tiba badala ya kuyaongeza la Sivyo, hatutakuwa SALAMA KAMWE!
Ukinisoma huku umetulia utapaona nilipoizungumzia CCM kama causative agent au mtu anayefanya kitu kinachoitwa An agent provocateur (French for "inciting agent") is a person who commits, or who acts to entice another person to commit an illegal or rash act or falsely implicate ...
Pasco
 
Pascal mayalla katika ubora wake!. pasco bisha nifunguke!
Mkuu Unga Unga kama join yako jf ni 2014, then huna ugeni wowote humu kuhusu sheia zetu, endelea tuu kutaja taja majina wa members humu, Pascal Mayalla yupo, tunajuana na kushabihiana sana tuu na ni verified member wa jf, na mimi nimo ni member, kosa la name calling adhabu yake ni ban!.

Nabisha na funguka!.

Pasco
 
Mkuu wamshambulia bure,
Pasco katoa maoni yake juu ya kile kinachoendelea Znz.
Kutoa maoni ni kitu cha kawaida ktk Nchi huru km hii , tunachokataza hapa ni uropokaji wa vitu bila kujua sheria za nchi.
Huyo Pasco mara nyingi huandika Vitu vya kinafiki bila kutambua Sheria na kanuni za Nchi anayoishi.

Vipi Chama Kifutwe kwa sababu ya Vurugu za watu?
Nani ulimuona au kusikia kabla ya kuanzisha vurugu akapeleka Kitambulisho chake cha chama polisi?
Na Sheria ipi ktk Nchi hii inayosema Chama Kitakacho sababisha Vurugu KIFUTWE?

Tukiruhusu watu wasio na elimu km hawa waendelee kubwabwaja ovyo kuna hatari ya kuliingiza hili taifa ktk upotofu na kutia hofu wananchi bila sababu za msingi.
Huyu jamaa anatakiwa akajifunze japo kidogo Sheria za nchi kabla ya kuanzisha nyuzi zake za ajabu ajabu humu.
 
I do not deny that I planned sabotage. I did not plan it in a spirit of recklessness nor because I
have any love of violence. I planned it as a result of a calm and sober assessment of the political situation that had arisen after many years of tyranny, exploitation and oppression of my people. Quote Nelson Mandela.
Naunga mkono hoja kuwa the dividing line between freedom fighting na inciting violence ni very thin!, kinachofanyika ni kujusfy violence kwa kisingizia cha fighting for the right cause, na hapa ndipo wanapokuja kutengeneza wale suicide bombers kwa ahadi ya kuwa “martyrdom ”, na kwenda peponi ukijitolea kufa !. Hatutaki kufika huko ndio maana haswa ya bandiko hili, ukithibitisha tuu, futilia mbali kwa kujihadhari kabla ya hatari!.

Pasco
 
Bibie tunapojadili haya mambo tujifunze kuweka ushabiki pembeni.

Wewe umewaona hao Mazombie tu?! Vipi hawa wanaochukua mabomu na kwenda kulipua kwenye nyumba za wakuu wa usalama? Vipi hawa wanaochoma ofisi na nyumba za wanachama wa CCM, hawa huwaoni, au ushabiki umekutia upofu?
Hio nyumba tuwekee picha hapa...nakupa 2 hrs uweke picha hio ya mkuu wa polisi....ameshindwa kuongoza sasa analeta propagandaa ili afanye uovu
2 hours unazo kuleta picha ya hio nyumba
 
Pasco,
Huwezi kuijua leo yako ikiwa huijui jana yako.
CUF haina historia hiyo.

Kwa muda mrefu CUF imewekeza sana katika elimu ya vijana na kujenga
mtambo ndani ya chama ambao utaweza kushinda uchaguzi wowote dhidi
ya CCM.

Hii ndiyo iliyofikisha CUF hapa tulipo hivi sasa.

CUF imeweza kushinda kila uchaguzi Zanzibar juu ya vikwazo vyote dhidi
yake.

Historia ya ASP hadi kufikia CCM Zanzibar inafahamika na kwa kukusaidia
ili uijue vyema nakuwekea hapa chini darsa dogo:
  1. Mohamed Said: KABLA YA MAZOMBIE KULIKUWA NA AKINA KAUJORE: MWANAMAPINDUZI ALIYEUA WATU MSIKITINI
  2. Mohamed Said: AMAN THANI ANAMWELEZA MANDERA NA MATESO YA KUNG'OA KUCHA 9
  3. Mohamed Said: MASULTANI WALIPATAPO KUUA, KUWEKA JELA ZA MATESO NA KUFANYA DHULMA NYINGINEZO DHIDI YA WAZANZIBARI?
  4. Mohamed Said: PEMBA: THE FIRE NEXT TIME
Pasco,
Hiyo hapo juu ndiyo historia ya Zanzibar.
Hakuna asiyeifahamu na ningeweza kukuwekea mengi ila naogopa kukuchosha.

Nakuuliza unadhani ikiwa hali ndiyo hiyo ni nani wa kufungwa kamba asiumize jamii?
Chama kipi kinastahili kufutwa ili jamii isalimike?

Kwa kumalizia nakuomba fungua uzi makhsusi kuhusu ugaidi.
Nakuwekea hapa chini mada kuhusu ugaidi ikufikirishe:
Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT
Mkuu Maalim Mohammed Said Seyyid wangu, kwanza asante kutia mguu kwenye bandiko langu, kitendo tuu cha kupita hata ungesema neno moja tuu kuwa nimekusoma, kwangu ni faraja tosha!.

Hili la chama na possibility ya CCM kuwa causative agent na An agent provocateur (French for "inciting agent") is a person who commits, or who acts to entice another person to commit an illegal or rash act or falsely ... nimelisema, ila nikasisitiza CCM haiwezi kufutwa hata ikukutikana ni yenyewe na sababu ziko kwenye link ya kufutwa kwa Chadema.

Japo mimi natofautiana sana na wewe kwenye issues za fundamenalisim yako, lakini nakubali sana kipaji chako, ilmu yako, na uwezo wako katika maandishi hivyo nakusoma sana tuu, na hizo links zako nitazipitia.

Kwa kukusaidia tuu, kwenye ile kadhia ya Mwembechai, mimi ndiye niliyekuwa ipota wa DTV on the line of fire, nashika kamera na kuripoti, pia kwenye zile seke seke za Zanzibar, ni mimi na Ally Saleh ndio tulilazwa Mwembemadema, hivyo ninauzoefu wa kutosha na hizi political violence, tuliwaona tangu mnapanda mbegu, mkiishea mimea, sasa karibia na kipindi cha mavuno, uzi huu ni kushauri tusisubirie mavuno kamili, dalili za sharri zimeishaanza kuonekana, heri ya nusu shari kuliko shari kamili, nimesisitiza na kuandeline, ikithibitishwa ni boa kifutwe!.

Ahasanta.
Pasco
 
Umekuwa mpuuzi sana siku hizi! Kila mtu ana gharama yake, they have just reached yours.
Shame on you
 
Mkuu Maalim Mohammed Said Seyyid wangu, kwanza asante kutia mguu kwenye bandiko langu, kitendo tuu cha kupita hata ungesema neno moja tuu kuwa nimekusoma, kwangu ni faraja tosha!.

Hili la chama na possibility ya CCM kuwa causative agent na An agent provocateur (French for "inciting agent") is a person who commits, or who acts to entice another person to commit an illegal or rash act or falsely ... nimelisema, ila nikasisitiza CCM haiwezi kufutwa hata ikukutikana ni yenyewe na sababu ziko kwenye link ya kufutwa kwa Chadema.

Japo mimi natofautiana sana na wewe kwenye issues za fundamenalisim yako, lakini nakubali sana kipaji chako, ilmu yako, na uwezo wako katika maandishi hivyo nakusoma sana tuu, na hizo links zako nitazipitia.

Kwa kukusaidia tuu, kwenye ile kadhia ya Mwembechai, mimi ndiye niliyekuwa ipota wa DTV on the line of fire, nashika kamera na kuripoti, pia kwenye zile seke seke za Zanzibar, ni mimi na Ally Saleh ndio tulilazwa Mwembemadema, hivyo ninauzoefu wa kutosha na hizi political violence, tuliwaona tangu mnapanda mbegu, mkiishea mimea, sasa karibia na kipindi cha mavuno, uzi huu ni kushauri tusisubirie mavuno kamili, dalili za sharri zimeishaanza kuonekana, heri ya nusu shari kuliko shari kamili, nimesisitiza na kuandeline, ikithibitishwa ni boa kifutwe!.

Ahasanta.
Pasco

Jijengee utaratibu wa kujifikirisha kidogo kabla ya Kuandika, unajua madhara ya kufuta chama kama Cuf?
Kwanin husemi ikithibitika ni ccm kifutwe? What's your motive? Bila Kujali kama inawezekana au la, ilitakiwa ukemee kwa uzito ule ule,! Uhalifu ni Uhalifu haijalishi unafanywa na Nani!
Njaa inatoa ufahamu, akili ndogo kutawala akili kubwa. Shame
 
Mkuu Pasco mbali na kutoa tahadhari ya yaliyopangwa kuhusu mustakabali wa CUF, toa mwanga pia jinsi unavyouona mustakabali wa demokrasia nchini. Umenukuu vifungu vya sheria kwenye hoja yako.

Unaamini kweli sheria inatumika inavyostahili nchini? Yaani nchi hii inaweza kujidai kwamba inaendesha utawala unaozingatia sheria na haki? Kama sivyo, badala ya kuwa "msoma matangazo ya vifo" kwa wapinzani, toa pia mawazo nini kifanyike kurejesha demokrasia ya kweli, haki na utawala wa sheria nchini?
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa objectivity ya bandiko lako, maana jf ya sasa kuwapata watu wenye objectivity ya kiwango hiki ni nada sana!, asante.

Nchi inaendesha kwa mihimili mitatu ya kiutendaji na wa nne wa sisi wapiga kelele, wapuliza firimbi.

Kwenye hili jambo tangu linatokea mwanzo nimeshauri sana tuu nini cha kufanya ila ushaui wangu uliishia kuwa kelele tuu.
Chanzo cha yote ni Jecha kufuta uchaguzi kinyume cha sheria. Jambo lolote la kisheria linahitaji utatuzi wa kisheria na sio kufanya press conferences na kupiga kelele.

Hebu nisome nimesema nini, nimeshauri nini,
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua ...
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabia, Zanzibar,
Maalim ...Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? | JamiiForums ...
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima ...
Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio ...
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar!. Waziri ...
Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein ...

Kufukia sasa vurugu zimeanza, nashauri bora kifutwe!.

Pasco'
13467;o,
 
Jijengee utaratibu wa kujifikirisha kidogo kabla ya Kuandika, unajua madhara ya kufuta chama kama Cuf?
Kwanin husemi ikithibitika ni ccm kifutwe? What's your motive? Bila Kujali kama inawezekana au la, ilitakiwa ukemee kwa uzito ule ule,! Uhalifu ni Uhalifu haijalishi unafanywa na Nani!
Njaa inatoa ufahamu, akili ndogo kutawala akili kubwa. Shame
Kwenye bandiko langu nilipoizungumzia CCM hukupaona?!, na pia nikasema hata ikitokea ikawa ni CCM, haitafutwa!, na sababu nimezitaja!.

Pasco
 
Kutoa maoni ni kitu cha kawaida ktk Nchi huru km hii , tunachokataza hapa ni uropokaji wa vitu bila kujua sheria za nchi.
Huyo Pasco mara nyingi huandika Vitu vya kinafiki bila kutambua Sheria na kanuni za Nchi anayoishi.

Vipi Chama Kifutwe kwa sababu ya Vurugu za watu?
Nani ulimuona au kusikia kabla ya kuanzisha virugu akapeleka Kitambulisho chake cha chama polisi?
Na Sheria ipi ktk Nchi hii inayosema Chama Kitakacho sababisha Virugu KIFUTWE?

Tukiruhusu watu wasio na elimu km hawa waendelee kubwabwaja ovyo kuna hatari ya kuliingiza hili taifa ktk upotofu na kutia hofu wananchi bila sababu za msingi.
Huyu jamaa anatakiwa akajifunze japo kidogo Sheria za nchi kabla ya kuanzisha nyuzi zake za ajabu ajabu humu.
Mkuu Kahataan, kiukweli mimi ni msikivu sana, na inshaalah, nimeupokea ushauri wako, mwezi wa 10 panaapo majaliwa, nitajiunga na chuo kimoja kusomea certificate ya sheria.

Pasco
 
Mimi nadhani siku za mbele ccm ikiwa benchi ifutwe kabisa ili turekibishe vizuri historia ya nchi.
Kifutwe ili kiwe ni katika historia ya chama kilichotokana na Tanu na Asp.
Kwa uchache vyama hivi viliwahusu wengi hata kama hupendi watu walishiriki kuvichangia
Lumumba na dodoma chamwino kugeuzwe kuwa makumbusho ya taifa.
Mali zote zirejeshwe serikalini.
Wapenzi wake wachague vyama vingine ili kuleta ushindani wa sawa sawa.
Likifanyika hili n hi yetu itakua imefanikiwa kuwaunganisha watu wake kuwa wamoja. Muungano nao utakua wa Watanzania na sio wa ccm. Hii itaepusha kuvunjika kwa muungano siku Mfano CDM ikishika madaraka kwani hawatakua tayari kulea fikra potofu ya mapinduzi daima na ccm znz itakosa god father wao wa kulea uozo wao.
Na nchi itapiga maendeleo sana kutokana na uwajibikaji bila ya kupewa maagizo ya masiku kwani wana nchi watakua sasa wameelewa faida ya vyama vingi na faida zake hivyo ume deliver unaendelea ..umechemsha wanakuweka bench wakati wa uchaguzi.
Kwa mfumo wa sasa bila ya ccm kufutwa hatuendelei maisha ...
 
Back
Top Bottom