Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,661
- 119,284
Wanabodi,
"Chama Cha Wananchi CUF, Kufutiliwa Mbali!... Iwapo Itathibitika Kinahusika/ Kitahusika na Vurugu, Ugaidi, Uvunjifu wa Amani Zanzibar na TZ!, ila ikitokea CCM ndio chanzo, au kisababishi cha vurugu hizo, CCM hakiwezi kufutwa kwa sababu ni chama tawala!".
Nyingi ya theads humu ni threads kuhusu matukio yaliyotokeakwa upande wa events, au events zitakazokuja kutokea lakini tuna threads chache sana kuhusu mambo ya ideas yatakayokuja kutokea, hivyo hii ni thread ya mambo ideas yatakakuja kutokea kutokana na kitu kinachoitwa "trend readings" na sio utabiri kama wa Sheikh Yahya (RIP) au Nostra Domus.
Trend ni inahusiana na usomaji wa historia ya mwenendo wa jambo fulani, kisababishi (the motive behind) kilichosababisha hiki kinachotokea sasa kitokee, ili kujua kile kitakachokuja kutokea huko tuendako, yaani ile "so what" ya maamuzi ya kufanya au kutofanya jambo fulani!.
Kichwa cha habari kimejieleza wazi (self explanatory) kuwa Chama cha Wananchi CUF, kitafutwa rasmi (toka kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya Siasa),only if, kama itathibitishwa pasipo shaka, with a court of competent juisdiction, tena without any reasonable doubt, kuwa kinahusika, au kitahusika na matukio yoyote ya kihalifu, ya kigaidi au ya uvunjifu wa amani, Zanzibar, Pemba au eneo lolote la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kitafutwa, kwa sababu kitakuwa kimepoteza sifa za kuitwa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992 ambayo kisheria inajulikana kama The Political Parties Act of 1992 au Chapter 258.
Sheria hiyo imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa kinachoweza kusajiliwa, lakini pia imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajiliwa, na miongoni mwa sifa za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajiliwa, ni pamoja na kipengele hiki kwenye ibara ya 8, 2-c
"it accepts or advocates the use of force or violence as a means attaining its political objectives"
Ibara hii inamaanisha kama chama kiliisha sajiliwa, lakini baadae kikagundulika kina kiuka kipengele hicho, chama hicho kinakuwa kimepoteza sifa ya kuitwa ni chama cha siasa hivyo kinastahili kufutwa kutoka kwenye daftari la msajili wa vyama, "strucked out fom the book of registerd political parties".
Viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CUF, msije kunirukia na kuniararua kuwa nawawangia au kuwachuria ili chama chenu kifutwe, bali nawapa tuu angalizo la matakwa ya kisheria, ikiwa na endapo itathibitishwa pasi shaka, "beyond reasonable doubts" kuwa CUF kama chama, kinahusika na haya yanayotokea sasa kwa kuwahamasisha wanachama na wafuasi wake kupanga, kuratibu na kutekeleza vitendo vyovyote vya kihalifu, vya kigaidi na vya kuvuruga amani na utulivu wa visiwa vya Unguja na Pemba ambazo ni sehemu za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, au eneo jingine lolote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ni kufuatia CUF kususia kushiriki uchaguzi wa marudio, swali la kujiuliza ni jee ni nini "the motive behind" ya kususa huku kwa CUF?!. Kwa vile uchaguzi wa marudio umeishatangazwa na majina ya wagombea wa CUF bado yapo, lakini CUF wameshikilia msimamo wake wa kususia uchaguzi huo, jee CUF wanaendelea kususa ili iweje?!. Jee kuna uwezekano kuwa kwa vile CUF wamejielekeza kususa uchaguzi huu tangu mwanzo lakini ZEC imewalazimisha kuwepo na kuyaweka majina ya wagombea wao kwa lazima, siku ya uchaguzi kupangwa baadhi ya wananchi wacheche kuwapigia kura wagombea wa CUF, hivyo ZEC kuhalalisha udhalimu wao, kuwa uchaguzi ilikuwa huru na wa haki, na matokeo ndio hayo yatakaoonyesha CUF imeshindwa vibaya!, hivyo kuna uwezekano CUF kama chama, wameamua, kuliko kusubiri aibu na kudhalilishwa kwa kushindwa vibaya, ni bora kufanya hujuma zozote ili uchahuzi usifanyike?!, hivyo kupanga, kuatibu na kutekeleza vitendo vya vurugu, uhalifu na ugaidi ili uchaguzi usifanyike?!. Ikithibitika CUF ndio ,mhusika wa haya, hakuna jingine zaidi ya kufutwa!.
Ila ikikutikana wanaofanya vitendo hivyo ni wana CUF individually kwa ridhaa zao wenyewe bila kushawishiwa wala kuratibiwa ba chama, then, CUF kama chama, kitabaki salama, na hao wanachama, individually watashughulikiwa kama wahalifu wengine wowote kwa sababu uhalifu ni uhalifu tuu, hauna chama, hauna dini, hauna kabila, hauna rangi wala jinsia, na wahalifu wote ni watu wa kulaaniwa jamii na sheria ichuke mkondo wake dhidi wahalifu hawa mapema, wasije kujiorganise wakaunda IS, Al Shabab na Al Qaeda yetu!.
Sheria zipo lakini hazitekelezwi, ila kufuatia JK kuwa dhaifu, na serikali yake kuwa dhaifu, kuliwapa wahalifu mawanda mapana ya kutamba hadi kumchezea simba sharubu na hakufanya lolote, zaidi ya kuitisha vikao vya maridhiano na miafaka, hizi nyakati za sasa zimebadilika, nyie mliozoea kuchezea sharubu za simba dhaifu, msijaribu kuchezea sharubu za huyu simba aliyepo, huyu sii simba yule wa kucheka na ngedee na kuyavuna mabua!, sasa nyakati zimebadilika, hili ni angalizo tuu nawapa, mlipokee au mlipuuzie, yakitokea ya kutokea, msilalamike kuwa hamkuambiwa!.
Ila pia kuna uwezekano, kwa vile CUF wamesusa, then mhalifu huu unafanywa na CCM kwa mtindo wa "self inflicting pain" ili ionekane ni CUF, ambapo CCM ni maajenti wa kitu kinachoitwa "An agent provocateur ?!, ili chama dola kipate uhalali wa kuwashukia?!. Na kama ni CCM ndio magaidi, jee nao watafutwa?!.
Kama ni CCM, hawatafutwa!, jee ni kwa nini CCM hawawezi kufutwa hata wakifanya lolote?!. Kulijua hili lazima ufanye homework kidogo kwa kauli ya Msajili wa vyama aliyepita, tena
Naombeni wana CUF, msije kunishutumu kuwa ninachuki na CUF, maneno kama haya ninayowaeleza leo, pia niliwahi kuwaeleza wenzenu na washirika wenu Chadema, na pia niliwahi kuyatoa kwa chama dola CCM!.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa ...
Tuhuma Hii: CHADEMA Kuendeshwa Kwa Katiba "Fake" Ikithibitishwa ...
Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio ...
Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile ...
Wasalaam.
Pasco wa jf!.