Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Pasco njaa itakuua kijana.
Wenzako wamesha yashinda maisha we umebaki kubwabwaja uharo tu jukwaani.

Sasa hapa ndo unaona imetabiri ya maana sana.
Unafahamu Sharti la Serikali KUFUTA CHAMA CHA UPINZANI? Au kila kinachokuja bichwani kwako unaamua kuandika tu hapa.!!

Hizi bangi za ausubuhi zina athari mbaya sana. Jaribu kuvuta baada ya Msosi wa mchana. Kuna afadhali kidogo.
 
...all that happen in #znz ni Nani anayesababisha LET FIND THE CAUSES!....
UONGOZI WA CUF ENDAPO UTATOA KAULI YA KUANZISHA FUJO HAPO UTAKUWA HATIAHANI.
BADALA YAKE KWA HEKIMA YA UONGOZI UMESEMA #HATUSHIRIKI #UCHAGUZI.
NONGWA IPO WAPI?.....
let be wise...
 
Cuf ni magaidi hata Mungu anajua, Kiongozi wa magaidi Cuf tawi lao la Uamsho ni yule Sheikh Faridi alieko jela segerea kwa fujo visiwani, tundikali kwa masheikh wasio magaidi na kwa Watalii, pia mauwaji ya Mapadri, halafu shinikizo Wazanzibari waichukie Tanzania Bara. Huyo boss wa CUF Uamsho ni mwanajeshi wa Arabuni aliepigana vita yeye pomaja na Osama Bin Muhammad Bin Laden huko Afghanistan wakiwa enzi hizo Mujahideen. Tusitaniane jamani
 
...all that happen in #znz ni Nani anayesababisha LET FIND THE CAUSES!....
UONGOZI WA CUF ENDAPO UTATOA KAULI YA KUANZISHA FUJO HAPO UTAKUWA HATIAHANI.
BADALA YAKE KWA HEKIMA YA UONGOZI UMESEMA #HATUSHIRIKI #UCHAGUZI.
NONGWA IPO WAPI?.....
let be wise...
Hekima Gani waliokuwa nayo.. wanajua fika wakitoa kauli hiyo tu ndiyo mwisho wao....Na jaribuni kufanya fujo mtavikimbia visiwa vile kwa kuogelea kwani mtahisi ngarawa, mashua na majahazi yatawacherewesha au mtaonekana haraka... angalia 2001 si zilifanyika fujo. nini kimetokea?
 
***
unatumia akili ipi?/ are happy with all stupidity? ajabu sana.
 
Na kifutwe ru kwani kina faida gani?
CCM INA faida gani???Kwa miaka hamsini bado Taifa ni Maskini wa kutupwa.Hivi Gaidi ni nani si yule aliyepeleka jeshi nankuanza kupiga watu.

Siasa hizi.Hata ukilishwa kinyesi Lazima ufurahie.
 
Wanabodi,

"Chama Cha Wananchi CUF, Kufutiliwa Mbali!... Iwapo Itathibitika Kinahusika/ Kitahusika na Vurugu, Ugaidi, Uvunjifu wa Amani Zanzibar na TZ!.

Nyingi ya theads humu ni threads kuhusu matukio yaliyotokea, lakini tuna threads chache sana kuhusu mambo yatakayokuja kutokea, hivyo hii ni thread ya mambo yatakakuja kutokea kutokana na kitu kinachoitwa "trend readings" na sio utabiri kama wa Sheikh Yahya (RIP) au Nostra Damas.

Trend ni inahusiana na usomaji wa historia ya kilichowahi kutokea nyuma, kulinganisha na kinachotokea sasa, ili kujua kitakachokuja kutokea huko tuendako.

Kichwa cha habai kimejieleza wazi kuwa Chama cha Wananchi CUF, kitafutwa rasmi (toka kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya Siasa), kama itathibitishwa pasipo shaka,without any reasonable doubt, kuwa kinahusika, au kitahusika na matukio yoyote ta kihalifu, ya kigaidi au ya uvunjifu wa amani, Zanzibar, Pemba au eneo lolote la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu kitakuwa kimepoteza sifa za kuitwa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992! ambayo kisheria inajulikana kama The Political Partie Act of 1992 au Chapter 258.

Sheria hiyo imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa kinachoweza kusajiliwa, lakini pia imeweka sifa mbali za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajili, na miongoni mwa sifa ambazo chama cha siasa hakiwezi kusajiliwa, ni pamoja na kipengele hiki kwenye ibara ya 8, 2-c
"it accepts or advocates the use of force or violence as a means attaining its political objectives"

Ibara hii inamaanisha kama chama kiliishasajili, lakini baadae kikagundulika kina kiuka kipengele hicho, kinakuwa kimepoteza sifa hivyo kinastahili kufutwa kutoka kwenye daftarri la msajili.

Viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CUF, msije kunirikia kuwa nawawangia au kuwachuria chama chenu kifutwe, bali nawapa tuu angalizo la matakwa ya kisheria, ikiwa na endapo itathibitishwa pasi shaka, "beyond reasonable doubts" kuwa CUF kama chama, kinahusika na kupanga, kuratibu na kutekeleza vitendo vyovyote vya kihalifu, vya kigaidi na vya kuvuruga amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar na Pemba ambazo ni sehemu za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni kufuatia CUF kususia kushiriki uchaguzi wa marudio, hivyo kimesusia na kupanga vurigu, uhalifu na ugaidi ili uchaguzi usifanyike, kama huo ndio mpango wenu, endeleeni na mipango hiyo, lakini huku mkijiandaa kufutwa rasmi!.

Ili ikikutikana wanaofanya vitendo hivyo ni wana CUF individually bila uhusika au uatibu wowote wa CUF kama chama, CUF kama chama, kitabaki salama, na hao wanachama, watashughulikiwa kama wahalifu wengine wowote kwa sababu uhalifu ni uhalifu tuu, hauna chama, hauna dini, hauna kabila, hauna rangi wala jinsia, uhalifu ni uhalifu tuu, na wahalifu wote ni watu wa kulaaniwa na sheria ichuke mkondo wake dhidi yao!.

Sheria zipo lakini hazitekelezwi, ila kufuatia JK kuwa dhaifu, na serikali yake kuwa dhaifu, kuliwapa wahalifu mawanda ya kutamba hadi kumchea simba sharubu na hakufanya lolote, hizi nyakati sasa zimebadilika, nyie mliozoea kuchezea sharubu za simba dhaifu, msijaribu kuchezea sharubu za huyu aliyepo, huyu sii yule mtu wa kucheka cheka na ngedee na kuyavuna mabua!, sasa nyakati zimebadilika, hili ni angalizo tuu nawapa, mlipokee au mlipuuzie, yakitokea ya kutokea, msilalamike kuwa hamkuambiwa!.

Naombeni msije kunisdhutumu kuwa ninachuki na CUF, maneno kama haya ninayowaeleza leo, pia niliwahi kuwaeleza wenzenu na washiika wenu Chadema, na pia niliwahi kuyatoa kwa chama dola CCM!.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa ...
Tuhuma Hii: CHADEMA Kuendeshwa Kwa Katiba "Fake" Ikithibitishwa ...

Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio ...
Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile ...

Wasalaam.

Pasco wa jf!.

Inajulikana wazi ni CCM je huyo Msajili aliwahi kuongeabna hao CCM?? Je aliwahi kuwasummon hata siku moja??

Huyo mlezi wa vyama ni kada wa CCM unadhani haki ipo hapo.Duh hii akili za kuambiwa changanya na zako
 
Pasco njaa itakuua kijana.
Wenzako wamesha yashinda maisha we umebaki kubwabwaja uharo tu jukwaani.

Sasa hapa ndo unaona imetabiri ya maana sana.
Unafahamu Sharti la Serikali KUFUTA CHAMA CHA UPINZANI? Au kila kinachokuja bichwani kwako unaamua kuandika tu hapa.!!

Hizi bangi za ausubuhi zina athari mbaya sana. Jaribu kuvuta baada ya Msosi wa mchana. Kuna afadhali kidogo.
Asante kwa ushauri, nitakuwa napuliza baada ya mlo.

Pasco
 
Asante kwa ushari, nitakuwa napuliza baada ya mlo.

Pasco
Labda nikuulize swali binafsi hapa.
Toka umeanza kuwepo humu JF na kuandika habari chungu mzima za chuki ni kipi cha maana umepata ktk maisha yako?
Je! ni umaarufu? Au kipato kimeongezeka?
Au basi tu huna la maana la kufanya ukaamua kupoteza pumzi zako ukisubiri siku ya kufa tu!?

Watu wenye Busara hufanya mambo yatakayo waletea Faida ktk maisha yao sasa wewe mwanawane kipi umepata mpk sasa?
 
Inajulikana wazi ni CCM je huyo Msajili aliwahi kuongeabna hao CCM?? Je aliwahi kuwasummon hata siku moja??

Huyo mlezi wa vyama ni kada wa CCM unadhani haki ipo hapo.Duh hii akili za kuambiwa changanya na zako
Mkuu Tetty posti ya msajili wa vyama inashikwa na mtu mwenye cheo cha Jaji. Majaji sio wanachama wa vyama, japo Tendwa aliegemea saba CCM, Jaji Mutungi namfahamu vizui ni mtu muadilifu na non partisan!.

Ila pia huu mtindo wa wajaji na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kujiunga CCM wanastaafu, kunatia mashaka na uwezekano walikuwa CCM kabla!, tumemuona Jaji Ramadhani japo alidhalilika ila angalau tumejua!. Harakati za Apson pia zilijulikana, hivyo ni kweli kabisa unaweza kukuta Mwamu nae ni CCM!, Othmans wote wawili ni CCM, inawezekana hata Muf.i na 'Jino' pia nao ni CCM, sasa nani atakuwa sio CCM?!. Kwa muktadha huu, CCM itatawala milele!.

Pasco
 
Mkuu Pasco ni Opportunist au mchumia tumbo kama wachumia tumbo wengine kina Mwanakijiji. Baada ya kuona nguvu ya Lowassa tangu yuko CCM na baadae kuhamia CDM alidhani kuwa angeshinda uraisi. Hivyo alijipanga kuwa upande wake Kwa kuandika mfululizo WA threads za kumsifia Lowassa na kueleza kuwa UKAWA ndo chaguo sahihi. Pitieni humu JF mtaona threads hizi. Na kweli alipata wengi wakumuunga mkono katika wapinzani na wengi wa kumponda toka CCM.
Sasa baada ya kuona upepo umebadilika na CCM ndo imeshinda amekuja na gia nyingine ya nitoke vipi kwa kuponda upinzani na kufagilia CCM na Magufuli.
Mtaona kuna complete u turn kwenye misingi ya hoja zake. Amepoteza mvuto na sio yule critical thinker tuliyemjua kabla ya uchaguzi.
Hivyo Mimi sishangai kuona watu Hawa maana anaagalia Maslahi take zaidi anaweza kuwa manipulated kirahisi tu.
Wapuuzi kama haw ndo wa kukamatwa ili kusaidia polisi.
 
Labda nikuulize swali binafsi hapa.
Toka umeanza kuwepo humu JF na kuandika habari chungu mzima za chuki ni kipi cha maana umepata ktk maisha yako?
Je! ni umaarufu? Au kipato kimeongezeka?
Au basi tu huna la maana la kufanya ukaamua kupoteza pumzi zako ukisubiri siku ya kufa tu!?

Watu wenye Busara hufanya mambo yatakayo waletea Faida ktk maisha yao sasa wewe mwanawane kipi umepata mpk sasa?
Kiukweli tunatatizo kubwa la uono na uelewa, mimi ni mwana fasihi, hivyo naelewa fika unapokuwa mkweli daima bila kuegemea upande wowote, utachukiwa na kuwa an enemy of the people, hili ni bandiko langu la 17,616 na hakuna hata bandiko langu moja ninalohubiri chuki na kikweli kabisa kusema kweli kwangu kumewahi kuniponza mara chungu nzima na kunikosesha opportunities kibao, lakini ukiwa mkweli toka ndani ya moyo wako, unakuwa gratified kwa kusema kweli, na hata ikibidi kulala njaa, unalala njaa smiling, kama kozi mwana Mandanda, kulala njaa kupenda!.

Kama Masiya alikuja kwa ajili ya Wayahudi na wakamsulubisha, nitakuwa mimi ninaowaeleza ukweli magaidi?!.

Pasco
 
huko kutakuwa ni kuishiwa kwa ccm kwani wanachama wa cuf hasa znz wanajua nini wanataka, na wavifute vyama vyote wabakishe ccm tu wazanzibari hawatowabadilisha akili zao. cuf ni jina tu muhimu malengo labda wawafute wazanzibari wote
 
Mkuu Pasco ni Opportunist au mchumia tumbo kama wachumia tumbo wengine kina Mwanakijiji. Baada ya kuona nguvu ya Lowassa tangu yuko CCM na baadae kuhamia CDM alidhani kuwa angeshinda uraisi. Hivyo alijipanga kuwa upande wake Kwa kuandika mfululizo WA threads za kumsifia Lowassa na kueleza kuwa UKAWA ndo chaguo sahihi. Pitieni humu JF mtaona threads hizi. Na kweli alipata wengi wakumuunga mkono katika wapinzani na wengi wa kumponda toka CCM.
Sasa baada ya kuona upepo umebadilika na CCM ndo imeshinda amekuja na gia nyingine ya nitoke vipi kwa kuponda upinzani na kufagilia CCM na Magufuli.
Mtaona kuna complete u turn kwenye misingi ya hoja zake. Amepoteza mvuto na sio yule critical thinker tuliyemjua kabla ya uchaguzi.
Hivyo Mimi sishangai kuona watu Hawa maana anaagalia Maslahi take zaidi anaweza kuwa manipulated kirahisi tu.

Pamoja na kuandika maneno mengi, hakuna hata sentensi moja inayojadili hoja. Hoja aliyotoa Pasco ni nzito na ya kikatiba. Soma tens halafu ujibu hoja kwa hoja.
 
Back
Top Bottom