Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Cuf ndo chama likubwa zaidi Tanzania kikiwa na wabunge pande 2 za muungano...
Tuchukulie nadharia ya Pasco iwe kweli..basi ni out come ?
Litalotokea ni kukua kwa upinzani mara kumi.
Cuf inaweza kuungana kabisa na CDM na mitaji yao kutaipa nguvu pande zote mbili za muungano...kiuonfozi CDM itafaidika na uzoefu wa viongozi wa cuf na kuwa chama chenye nguvu pande zote 2 za muungano.
Wakitumia nafasi hio vizuri na kujenga safu yao vizuri itakuwa chama cha kitaifa kwa kuwa na viongozi kila pembe ya TZ na uwiano mkuu wa kidini ambao hata ccm haupo kwa sasa....
Naamini ccm 2020 itakua chali
 
Nilidhani CUF kina hatari ya kufutwa na Msajili wa Vyama vya siasa, lakini kumbe Msajili badala ya kukifuta CUF, amewapa kamba ya kujinyongea ili wajinyonge wenyewe kama samaki wanaojikaanga kwa mafuta yao wenyewe! .
Pasco
 
Nilidhani CUF kina hatari ya kufutwa na Msajili wa Vyama vya siasa, lakini kumbe Msajili badala ya kukifuta CUF, amewapa kamba ya kujinyongea ili wajinyonge wenyewe kama samaki wanaojikaanga kwa mafuta yao wenyewe! .
Pasco
Kweli mkuu, wangekaa meza moja na kufikia mwafaka ingekuwa nzuri... Ila kwa staili ya kutopeana mikono.... Tutawazika
 
Masheikh wangu masjid idrissa tusaidieni kwa hili la alhaj LIPUMBA mpime anachokifanya asije akajileta na usanii wake kujifanya anatupenda waislam huku akituumiza nyoyo zetu muwe wepesi wa kuhoji mambo kabla hayajaharibika
 
Pasco mtoa mada hii, looh umekoroga na mavitu mengi kiasi kwamba hapana atakayeweza kulinywa. Mimi sikuelewi hata kidogo. Hivi kweli CCM ikathibitika imefanya uhaini (uhaini ni kuisimamisha katiba ya nchi isitekelezeke) kwa nini isishitakiwe? Kwani uhaini una chama, dini ama kabila? Wewe umenishawishi nikuone kwanza mchochezi pili mbaguzi wa wazi, tatu ni mtumishi (hired cop) wa Lumumba. Nakwambia unamtumikia shetani na hakika moto wa jehenam upo kichwani kwako wakusubiri.
 
Wanabodi,

"Chama Cha Wananchi CUF, Kufutiliwa Mbali!... Iwapo Itathibitika Kinahusika/ Kitahusika na Vurugu, Ugaidi, Uvunjifu wa Amani Zanzibar na TZ!, ila ikitokea CCM ndio

Kichwa cha habari kimejieleza wazi (self explanatory) kuwa Chama cha Wananchi CUF, kitafutwa rasmi (toka kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya Siasa),only if, kama itathibitishwa pasipo shaka, with a court of competent juisdiction, tena without any reasonable doubt, kuwa kinahusika, au kitahusika na matukio yoyote ya kihalifu, ya kigaidi au ya uvunjifu wa amani, Zanzibar, Pemba au eneo lolote la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kitafutwa, kwa sababu kitakuwa kimepoteza sifa za kuitwa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992 ambayo kisheria inajulikana kama The Political Parties Act of 1992 au Chapter 258.

Sheria hiyo imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa kinachoweza kusajiliwa, lakini pia imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajiliwa, na miongoni mwa sifa za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajiliwa, ni pamoja na kipengele hiki kwenye ibara ya 8, 2-c
"it accepts or advocates the use of force or violence as a means attaining its political objectives"

Ibara hii inamaanisha kama chama kiliisha sajiliwa, lakini baadae kikagundulika kina kiuka kipengele hicho, chama hicho kinakuwa kimepoteza sifa ya kuitwa ni chama cha siasa hivyo kinastahili kufutwa kutoka kwenye daftari la msajili wa vyama, "strucked out fom the book of registerd political parties".

Viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CUF, msije kunirukia na kuniararua kuwa nawawangia au kuwachuria ili chama chenu kifutwe, bali nawapa tuu angalizo la matakwa ya kisheria, ikiwa na endapo itathibitishwa pasi shaka, "beyond reasonable doubts" kuwa CUF kama chama, kinahusika na haya yanayotokea sasa kwa kuwahamasisha wanachama na wafuasi wake kupanga, kuratibu na kutekeleza vitendo vyovyote vya kihalifu, vya kigaidi na vya kuvuruga amani na utulivu wa visiwa vya Unguja na Pemba ambazo ni sehemu za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, au eneo jingine lolote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
.


Ila ikikutikana wanaofanya vitendo hivyo ni wana CUF individually kwa ridhaa zao wenyewe bila kushawishiwa wala kuratibiwa ba chama, then, CUF kama chama, kitabaki salama, na hao wanachama, individually watashughulikiwa kama wahalifu wengine wowote kwa sababu uhalifu ni uhalifu tuu, hauna chama, hauna dini, hauna kabila, hauna rangi wala jinsia, na wahalifu wote ni watu wa kulaaniwa jamii na sheria ichuke mkondo wake dhidi wahalifu hawa mapema, wasije kujiorganise wakaunda IS, Al Shabab na Al Qaeda yetu!.

Sheria zipo lakini hazitekelezwi, ila
Naombeni wana CUF, msije kunishutumu kuwa ninachuki na CUF, maneno kama haya ninayowaeleza leo, pia niliwahi kuwaeleza wenzenu na washirika wenu Chadema, na pia niliwahi kuyatoa kwa chama dola CCM!.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa ...
Tuhuma Hii: CHADEMA Kuendeshwa Kwa Katiba "Fake" Ikithibitishwa ...

Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio ...
Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile ...

Wasalaam.

Paskali
Kiukweli CUF wana bahati sana Msajili wa Vyama ni Jaji Mutungi, hivyo sio tuu wamevumiliwa sana, hadi kudekezwa hadi pale mtu anajitoa kisha anajirudisha kwa nguvu, anafukuzwa lakini anang'ang'ania na ruzuku anapewa yeye!.

Kiongozi wa chama anapotuma ma bouncer kwenda kuvuruga mkutano!.

It's now only a matter of time.

Paskali.
 
watawala wanacheza na amani,wao michezo yote hii ni kutafutia sababu ya kukiandama chama.wanataka kuona upande wa seif watavyoreact....
 
Kwa malengo YAO ya kukifuta CUF ndo maana wanatuma Watu "wanaojitoa muhanga" wapigwe mawe, ama wachomwe moto ili kuonesha kuwa CUF ni hatare. Muradi huu sasa unasimamiwa na Lipumba na Mutungi..
 
Cuf ndo chama likubwa zaidi Tanzania kikiwa na wabunge pande 2 za muungano...
Tuchukulie nadharia ya Pasco iwe kweli..basi ni out come ?
Litalotokea ni kukua kwa upinzani mara kumi.
Cuf inaweza kuungana kabisa na CDM na mitaji yao kutaipa nguvu pande zote mbili za muungano...kiuonfozi CDM itafaidika na uzoefu wa viongozi wa cuf na kuwa chama chenye nguvu pande zote 2 za muungano.
Wakitumia nafasi hio vizuri na kujenga safu yao vizuri itakuwa chama cha kitaifa kwa kuwa na viongozi kila pembe ya TZ na uwiano mkuu wa kidini ambao hata ccm haupo kwa sasa....
Naamini ccm 2020 itakua chali
Mkuu Macos, kuna kitu ulikisema hapa 4 years ago, ndio kimetokea sasa, japo sii Chadema lakini matokeo ni yale yale. Hongera kwa utabiri huu.
P.
 
Mkuu Macos, kuna kitu ulikisema hapa 4 years ago, ndio kimetokea sasa, japo sii Chadema lakini matokeo ni yale yale. Hongera kwa utabiri huu.
P.
Bwana P Mimi naona kipindi hiki ndio upinzani umeimarika zaidi kuliko wakati wote.Kipindi cha nyuma CCM ilijaza mamluki kibao upinzani.Kina Lipumba,Mrema and Co.Yote hayo yalikuwa matango pori!
 
Vyama viko kibau mbona hamuandiki habari zao? Tabia ya kuandika habari za chama kimoja tu cha upinzani inafanya waandishi waonekane vibaraka wa ccm.

Habari za chama kimoja tu siku zote hadi inakuwa "Routine and Monotonous". Acheni ukanjanja andikeni habari ya vyama vingine pia ili pia tuvifahamu. Sasa nchi utafikiri chama ni kimoja tu. This is very silly and rather bore some. Please we're fed up.
Mkuu Nyanjomigire, pole, hatuandiki kuhusu chama kimoja tuu, na huu ni mfano hai.

P.
 
Back
Top Bottom