Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Chama Cha Wananchi CUF Kufutiliwa mbali

Wasi wasi ni kuwa wakifutwa katika orodha ya msajili wa vyama wataenda wapi? Serkali na vyombo vyake vitakuwa na wakati mgumu zaidi maana sasa hawatakuwa na ofisi inayojulikina wala wanachama wanaofahamika. Ni afadhali wakawepo na kuthibitiwa kisiasa kuliko kuwapeleka kusikojulikana!!!
 
Sio suluhisho hilo, mahakama ndio yenye mamlaka ya kudhibitisha makosa ya kila jambo sasa sijui msajili ataenda mahakamani?
 
I do not deny that I planned sabotage. I did not plan it in a spirit of recklessness nor because I
have any love of violence. I planned it as a result of a calm and sober assessment of the political situation that had arisen after many years of tyranny, exploitation and oppression of my people. Quote Nelson Mandela.
 
Wanabodi,

"Chama Cha Wananchi CUF, Kufutiliwa Mbali!... Iwapo Itathibitika Kinahusika/ Kitahusika na Vurugu, Ugaidi, Uvunjifu wa Amani Zanzibar na TZ!.

Nyingi ya theads humu ni threads kuhusu matukio yaliyotokea, lakini tuna threads chache sana kuhusu mambo yatakayokuja kutokea, hivyo hii ni thread ya mambo yatakakuja kutokea kutokana na kitu kinachoitwa "trend readings" na sio utabiri kama wa Sheikh Yahya (RIP) au Nostra Damas.

Trend ni inahusiana na usomaji wa historia ya kilichowahi kutokea nyuma, kulinganisha na kinachotokea sasa, ili kujua kitakachokuja kutokea huko tuendako.

Kichwa cha habai kimejieleza wazi kuwa Chama cha Wananchi CUF, kitafutwa rasmi (toka kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya Siasa), kama itathibitishwa pasipo shaka,without any reasonable doubt, kuwa kinahusika, au kitahusika na matukio yoyote ta kihalifu, ya kigaidi au ya uvunjifu wa amani, Zanzibar, Pemba au eneo lolote la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu kitakuwa kimepoteza sifa za kuitwa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992! ambayo kisheria inajulikana kama The Political Partie Act of 1992 au Chapter 258.

Sheria hiyo imeweka sifa mbalimbali za chama cha siasa kinachoweza kusajiliwa, lakini pia imeweka sifa mbali za chama cha siasa ambacho hakiwezi kusajili, na miongoni mwa sifa ambazo chama cha siasa hakiwezi kusajiliwa, ni pamoja na kipengele hiki kwenye ibara ya 8, 2-c
"it accepts or advocates the use of force or violence as a means attaining its political objectives"

Ibara hii inamaanisha kama chama kiliishasajili, lakini baadae kikagundulika kina kiuka kipengele hicho, kinakuwa kimepoteza sifa hivyo kinastahili kufutwa kutoka kwenye daftarri la msajili.

Viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CUF, msije kunirikia kuwa nawawangia au kuwachuria chama chenu kifutwe, bali nawapa tuu angalizo la matakwa ya kisheria, ikiwa na endapo itathibitishwa pasi shaka, "beyond reasonable doubts" kuwa CUF kama chama, kinahusika na kupanga, kuratibu na kutekeleza vitendo vyovyote vya kihalifu, vya kigaidi na vya kuvuruga amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar na Pemba ambazo ni sehemu za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni kufuatia CUF kususia kushiriki uchaguzi wa marudio, hivyo kimesusia na kupanga vurigu, uhalifu na ugaidi ili uchaguzi usifanyike, kama huo ndio mpango wenu, endeleeni na mipango hiyo, lakini huku mkijiandaa kufutwa rasmi!.

Ili ikikutikana wanaofanya vitendo hivyo ni wana CUF individually bila uhusika au uatibu wowote wa CUF kama chama, CUF kama chama, kitabaki salama, na hao wanachama, watashughulikiwa kama wahalifu wengine wowote kwa sababu uhalifu ni uhalifu tuu, hauna chama, hauna dini, hauna kabila, hauna rangi wala jinsia, uhalifu ni uhalifu tuu, na wahalifu wote ni watu wa kulaaniwa na sheria ichuke mkondo wake dhidi yao!.

Sheria zipo lakini hazitekelezwi, ila kufuatia JK kuwa dhaifu, na serikali yake kuwa dhaifu, kuliwapa wahalifu mawanda ya kutamba hadi kumchea simba sharubu na hakufanya lolote, hizi nyakati sasa zimebadilika, nyie mliozoea kuchezea sharubu za simba dhaifu, msijaribu kuchezea sharubu za huyu aliyepo, huyu sii yule mtu wa kucheka cheka na ngedee na kuyavuna mabua!, sasa nyakati zimebadilika, hili ni angalizo tuu nawapa, mlipokee au mlipuuzie, yakitokea ya kutokea, msilalamike kuwa hamkuambiwa!.

Naombeni msije kunisdhutumu kuwa ninachuki na CUF, maneno kama haya ninayowaeleza leo, pia niliwahi kuwaeleza wenzenu na washiika wenu Chadema, na pia niliwahi kuyatoa kwa chama dola CCM!.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa ...
Tuhuma Hii: CHADEMA Kuendeshwa Kwa Katiba "Fake" Ikithibitishwa ...

Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio ...
Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile ...

Wasalaam.

Pasco wa jf!.

Kama CCM ilivyopoteza muelekeo na kuanza kufanya Ugaidi?
 
Mkuu Pasco siku hizi watanzania wamekwenda shule, hivi kwa akili za kawaida CUF inaweza kufanya vitendo ambavyo vita halalisha kufutwa kwake kutoka kwenye vitabu vya msajili wa vyama?
 
Mkuu Pasco siwezi kutumia lugha zenye ukakasi juu yako ninakuheshimu sasa kaka yangu.Labda nikuulize swali kimekusibu nini ndugu yetu? Mbona umekuwa mun'gunya unaharibikia ukubwani?
hivi pasco huyu mchumia tumbo ndio wa kumheshimu ? una ujasiri wa kutisha sana kuheshimu visivyostahili .
 
Tukio Kama la kuchinjwa Yule Mawazo kule chato tunaweza kuliitaje? Je lile lilikua sio tukio la kisiasa? Mnachinja watu Kama kuku hamuoni? Unasubiri Na unahamu sana uone Pemba watu wanachinjana ili huu utabiri wako wa kijinga ufurahi? Wewe Ni kichogo Zanzibar haikuhusu, Mbona husemi wakulima Na wafugaji Ni magaidi?

Wewe kichogo usituombee matatizo, Zanzibar ilikuwepo Kabla ya Cuf Na itabaki, Mbona majanga yakitokea kwenu Bara huandiki ujinga wako humu? Risasi zinalia asubuhi Na jioni unachekelea au kwakua Na wewe Ni jambazi mwenzako? Hatuoni ujinga wako kukemea hapa.

Nadhani vyama Ndio vinavokupa mkate unahisi kikifutwa Cuf Waznz watakufa? Usiwe mjinga nyinyi Ndio mnaotuharibia Zanzibar Yetu Kwa kuwalisha watu wakashiba huku Zanzibar Na wakawasumbua wenye njaa.
 
Back
Top Bottom