Hebu soma vizuri ulichokiandika halafu ulinganishe na reaction ya taboaHawa TABOA mie bado sijawaelewa kwa kweli. Huu mgomo wanaotangaza kushinikiza bunge lisipitishe sheria inayowabana ni sheria gani hiyo?? Mbona ukiangalia hata website ya bunge huoni muswada wa namna hiyo? Au wanachanganya madawa hawa?
Ninachojua mimi, SUMATRA wako kwenye mchakato wa kutunga kanuni mpya za usafirishaji abiria ambazo kwa kiasi kikubwa zinambana mmiliki kuliko dereva, kwa kwa mmiliki ndiye mwajiri na ndiye aliyepewa leseni. Kwa mfano dereva akikutwa hana uniform anaadhibiwa mmiliki. Sasa hii ndio TABOA hawataki. Lakini kanuni hazipitishwi na bunge zinasainiwa na Waziri zinaanza kutumika. Sasa sijui bunge wanalihusisha vipi?? Maana kama ni uthibiti wa bunge ni kupitia kamati ya sheria ndogo ambayo tayari ilikuwa kwenye session wiki iliyopita.
Mmmh sijui ngoja tusubiri.
magari ya jeshi yapo..yatasafirisha abiria
tuwekee hiyo sheria tuisome nasisi, yaani dereva akiwahepa trafik anakamatwa tajiri, au?
Ungejua navyoichukia SISIEM,ungeniomba radhiSema ndio wabunge wenu wa ccm sampuli za kina lusinde, ndipo walipofikia.
Na makosa ambayo yanambana mmiliki ambayo awali yakimbana dereva utayaona hapo, hakuna kifungu kinachosema mmiliki atafungwa jela kwa makosa ya dereva yanayohusu uendeshaji gari. Makosa ambayo sheri hiyo inashughulikia ni makosa yanayohusu ukiukwaji wa masharti ya lesen kama vile kukatisha ruti, kupandisha nauli, watumishi kutokuwa na sare, kutembeza gari bovu, nk ambayo yote adhabu yake kwa kiasi kikubwa ni faini. Dereva anabaki na makosa yake chini ya sheria ya usalama barabarani kama vile kuovateki pasiporuhusiwa, kuzidisha mwendo, nk
~~~>>>Mimi nipo zangu hapa Usangi Kijiweni.....Wasalimie hapo ugweno
mkuu, mfano niko dodoma baada ya wizara kuhamia kule nimeliacha daladala ninapiga safari za gongo lamboto chanika, dereva hajavaa sare unakuja kunisomba ofisini na kunisweka lupango, hii itakuwa sawa? Na mfuso wa mchanga gari limepata shoti taa haziwaki dereva kaamua kwenda nalo hivyo hivyo napo uje unikamate, sawa? kuna hizi tairi za michelini hazina kashata trafik anakwambia ni kipara nazo nikamatwe? au sijakuelewa?Na makosa ambayo yanambana mmiliki ambayo awali yakimbana dereva utayaona hapo, hakuna kifungu kinachosema mmiliki atafungwa jela kwa makosa ya dereva yanayohusu uendeshaji gari. Makosa ambayo sheri hiyo inashughulikia ni makosa yanayohusu ukiukwaji wa masharti ya lesen kama vile kukatisha ruti, kupandisha nauli, watumishi kutokuwa na sare, kutembeza gari bovu, nk ambayo yote adhabu yake kwa kiasi kikubwa ni faini. Dereva anabaki na makosa yake chini ya sheria ya usalama barabarani kama vile kuovateki pasiporuhusiwa, kuzidisha mwendo, nk
Ndio akili yako imeishia hapo?! Ok!! Vizurimagari ya jeshi yapo..yatasafirisha abiria