Chama cha Wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,548
2,000
Chama cha wamiliki wa mabasi kimetangaza mgomo kuanzia jumatatu kupinga sheria kandamizi ya usafirishaji inayoyotarajiwa kupitishwa bungeni hivi karibuni.

source: itv habari.
 

riro23

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
702
1,000
~~>>>Huyu Enea Mrutu ni diwani Kata ya Shighatini Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro kupitia CCM...

~~~>>>Huyu ni kada mtiifu ndani ya CCM.... Aendelee kuisoma namba..

Wasalimie hapo ugweno
 

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
411
195
Chama cha wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo.

Chama cha wamiliki wa mabasi -TABOA,kwa kushirikiana na wamiliki wa malori na chama cha wasafirishaji mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchinzima kuanzia siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitishwa siku ya jumanne wiki ijayo.

Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutao mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi,Malori,Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Bwana. Eneo Mrutu amesema sheria inaloyolenga kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva linasababisha mmiliki kufungwa jela.

Aidha amewaomba wabunge bila kujali itiokadi za vyama vyao kutopisha sheria hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.

Chanzo: ITV
Hawa TABOA mie bado sijawaelewa kwa kweli. Huu mgomo wanaotangaza kushinikiza bunge lisipitishe sheria inayowabana ni sheria gani hiyo?? Mbona ukiangalia hata website ya bunge huoni muswada wa namna hiyo? Au wanachanganya madawa hawa?
Ninachojua mimi, SUMATRA wako kwenye mchakato wa kutunga kanuni mpya za usafirishaji abiria ambazo kwa kiasi kikubwa zinambana mmiliki kuliko dereva, kwa kwa mmiliki ndiye mwajiri na ndiye aliyepewa leseni. Kwa mfano dereva akikutwa hana uniform anaadhibiwa mmiliki. Sasa hii ndio TABOA hawataki. Lakini kanuni hazipitishwi na bunge zinasainiwa na Waziri zinaanza kutumika. Sasa sijui bunge wanalihusisha vipi?? Maana kama ni uthibiti wa bunge ni kupitia kamati ya sheria ndogo ambayo tayari ilikuwa kwenye session wiki iliyopita.
Mmmh sijui ngoja tusubiri.
 

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,813
2,000
Kinachoshangaza wabunge wetu hawa hawa (ndiyoooooo) watapitisha hii sheria. Jamaa yangu ni mbunge na ana magari ya kusafirisha mizigo na abiria lkn nae atashiriki kupitisha sheria hiyo
 

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,603
2,000
nakuunga mkono Sugu dereva wake aliua mtoto Sugu akamatwe afungwe
Kama wakiupitisha muswada huo kuwa sheria, kwa nini na yeye asiwajibike?
Hapa siyo siasa, ni haki.
Ila kwa wabunge wa CCM lazima watapitisha maana Mwenyekiti wao alishawatishia kuvunja bunge wakileta za kuleta.
 

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,548
2,000
Kinachoshangaza wabunge wetu hawa hawa (ndiyoooooo) watapitisha hii sheria. Jamaa yangu ni mbunge na ana magari ya kusafirisha mizigo na abiria lkn nae atashiriki kupitisha sheria hiyo
Cha ajabu hawahawa wabunge ndio walpitisha sheria ya HESLB 15% halafu wengi wao ni wanufaika wa bodi na ni wahanga wa 15%,so sioni ajabu wakipitisha hiyo sheria....shame on them...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom