Chama cha Wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,150
2,000
Wamiliki Wa vyombo vya usafiri nchini( mabasi, daladala, na bajaji) wamesema wataanza mgomo Wa kutosafirisha abiria kuanzia wiki ijayo Jumanne kupinga sheria kandamizi ambayo imepelekwa bungeni ili ipitishwe na kuanza kutumika.

Wakiongea kupitia taarifa ya habari ITV wamesema sheria hiyo kandamizi hawajashirikishwa kuiandaa na kuomba wabunge kutoipitisha.

Wamedai sheria hiyo haijatoa ufanunuzi Wa makosa gani yanayo muhusu dereva au mmiliki Wa Gari hivyo Kosa ambalo analoweza kufanya Dereva linaweza kumfunga mmiliki wa gari.

Kutokana na upungufu huo wameona kuna mtego Wa panya wametegewa jambo linaloweza kuwatia hatiani.
 

kiatu kipya

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
3,278
2,000
Khaaa Bajaj zangu mie itakuwa ni use..... Mkubwa sheria ipite bila kuwashirikisaha wadau kama ni kweli
 

SaaMbovu

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
5,410
2,000
Duh, kosa la dereva mmiliki wa gari anahusishwa je? Yaani dereva akafanye uhuni wake huko then mmiliki akafungwe?

Tanzania sijui tunaenda wapi?
Inafanana na ile ya kwamba Binti akipata mimba mzazi anaenda jela hahaaa
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
5,729
2,000
Hapo wamechelewa, huu wakati ambao Kisesa inaondoka Mwanza kuelekea Dar na abiria 20, ndio mnakumbuka kugoma? Acha wagome tu hakuna namna ya kuwasaidia!
 

havanna

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
1,701
2,000
Serikali inashindwa kutengeneza mazingira kwa wawekezaji hasa wa usafiri kila siku kuwalipisha makosa ya barabarani lakini hata mpango wa kutanua barabara ya dar _Moro hakuna
 

wasumu

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
1,981
2,000
Ccm hakuna wasomi wengi ni mafisi sasa hiyo sheria haina hata kichwa
 

Nena

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
2,301
2,000
Duh, kosa la dereva mmiliki wa gari anahusishwa je? Yaani dereva akafanye uhuni wake huko then mmiliki akafungwe?

Tanzania sijui tunaenda wapi?
Kama mzazi atafungwa mtoto akibeba mimba akiwa shule.
 

mkwawa complex

Senior Member
Dec 15, 2016
184
250
DAH ! INA MAANA KAMA TAJIRI ANA MABASI 12 NA MALORI 5, AJIANDAE KUFUNGWA MARA 17 KULINGANA NA IDADI YA MADEREVA ANOATAKIWA KUWA NAO.HAPO NI KAMA KILA DEREVA KAFANYA KOSA MOJA TU.WAKIFANYA MAKOSA ZAIDI,TAJIRI ATAKUFIA JELA BWAANA !
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom