Chama cha Wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo

Hio sheria itakuwa kandamizi makosa ya dereva mmliki anahusika vipiu ukiwa na madereva zaid ya kumi na wafanye makosa itakuaje hapo.
 
Kanuni hizo mpya tarajiwa ni hizi hapa. Hii ni version iliyojadiliwa siku zile pale Mwalimu Nyerere Convention centre na wadau kutoa maoni yao
 
Attachments

  • Fungo - draft regulations1.docx
    217.6 KB · Views: 40
Na makosa ambayo yanambana mmiliki ambayo awali yakimbana dereva utayaona hapo, hakuna kifungu kinachosema mmiliki atafungwa jela kwa makosa ya dereva yanayohusu uendeshaji gari. Makosa ambayo sheri hiyo inashughulikia ni makosa yanayohusu ukiukwaji wa masharti ya lesen kama vile kukatisha ruti, kupandisha nauli, watumishi kutokuwa na sare, kutembeza gari bovu, nk ambayo yote adhabu yake kwa kiasi kikubwa ni faini. Dereva anabaki na makosa yake chini ya sheria ya usalama barabarani kama vile kuovateki pasiporuhusiwa, kuzidisha mwendo, nk
 
Duh!! Ndio Hapa unamkomesha baba mwenye nyumba akiomba lifti na hakutaka kukuelewa katika kodi ya miezi iliyopita alikomaa Sana. Unamwambia panda nyumba ikupeleke unakoenda. Serekali must have to settle this down ASAP
 
Hawa TABOA mie bado sijawaelewa kwa kweli. Huu mgomo wanaotangaza kushinikiza bunge lisipitishe sheria inayowabana ni sheria gani hiyo?? Mbona ukiangalia hata website ya bunge huoni muswada wa namna hiyo? Au wanachanganya madawa hawa?
Ninachojua mimi, SUMATRA wako kwenye mchakato wa kutunga kanuni mpya za usafirishaji abiria ambazo kwa kiasi kikubwa zinambana mmiliki kuliko dereva, kwa kwa mmiliki ndiye mwajiri na ndiye aliyepewa leseni. Kwa mfano dereva akikutwa hana uniform anaadhibiwa mmiliki. Sasa hii ndio TABOA hawataki. Lakini kanuni hazipitishwi na bunge zinasainiwa na Waziri zinaanza kutumika. Sasa sijui bunge wanalihusisha vipi?? Maana kama ni uthibiti wa bunge ni kupitia kamati ya sheria ndogo ambayo tayari ilikuwa kwenye session wiki iliyopita.
Mmmh sijui ngoja tusubiri.
Hebu soma vizuri ulichokiandika halafu ulinganishe na reaction ya taboa
 
Jumatatu naenda dar natokea dar gar yangu ina nafasi 4 nauli elf 50. Njoo PM kama unasafir maana ndo fulsa hiyo sasa.
 
Asante kwa ufafanuzi umeeleweka
Na makosa ambayo yanambana mmiliki ambayo awali yakimbana dereva utayaona hapo, hakuna kifungu kinachosema mmiliki atafungwa jela kwa makosa ya dereva yanayohusu uendeshaji gari. Makosa ambayo sheri hiyo inashughulikia ni makosa yanayohusu ukiukwaji wa masharti ya lesen kama vile kukatisha ruti, kupandisha nauli, watumishi kutokuwa na sare, kutembeza gari bovu, nk ambayo yote adhabu yake kwa kiasi kikubwa ni faini. Dereva anabaki na makosa yake chini ya sheria ya usalama barabarani kama vile kuovateki pasiporuhusiwa, kuzidisha mwendo, nk
 
Na makosa ambayo yanambana mmiliki ambayo awali yakimbana dereva utayaona hapo, hakuna kifungu kinachosema mmiliki atafungwa jela kwa makosa ya dereva yanayohusu uendeshaji gari. Makosa ambayo sheri hiyo inashughulikia ni makosa yanayohusu ukiukwaji wa masharti ya lesen kama vile kukatisha ruti, kupandisha nauli, watumishi kutokuwa na sare, kutembeza gari bovu, nk ambayo yote adhabu yake kwa kiasi kikubwa ni faini. Dereva anabaki na makosa yake chini ya sheria ya usalama barabarani kama vile kuovateki pasiporuhusiwa, kuzidisha mwendo, nk
mkuu, mfano niko dodoma baada ya wizara kuhamia kule nimeliacha daladala ninapiga safari za gongo lamboto chanika, dereva hajavaa sare unakuja kunisomba ofisini na kunisweka lupango, hii itakuwa sawa? Na mfuso wa mchanga gari limepata shoti taa haziwaki dereva kaamua kwenda nalo hivyo hivyo napo uje unikamate, sawa? kuna hizi tairi za michelini hazina kashata trafik anakwambia ni kipara nazo nikamatwe? au sijakuelewa?
 
Daaaa.....wanakumbuka shuka kumekucha..??
Leo hii ndipo machozi yanaponilenga.lenga kila nikimkumbuka mpambanaji Rashid R.I.P mkuu,eti wakatwambia ulikufa kwa kula kitu kinachosadikiwa kuwa na sumu pale maeneo ya liverside ubungo.
Ila Hakika uliwapigania sana hawa jamaa ,hata mh kayanza peter na bashite wa Koromije wanakukumbuka sana.
 
Kwa hili la TABOA naona kama wamejitia kidole wao wenyewe, anaefahamu hili atakuwa shahidi kwa wengine

Mbona hawa wamiliki wa malori, ikitokea dereva yupo safarini busta ikapasuka dereva anatakiwa kulipa! Akipasua tair analipa, akivunja kioo analipa, msiba mzito upo kwa wenye tanker. Dereva akipata shoti tu ya lita kadhaa za mafuta analipishwa, madereva hawa hawa siku zote wengi wao ni vibarua tu, ni kampuni chache mno zimewaajiri.

Wamiliki hawa wao hawataki hasara wala kuwajibika kwa namna yoyote ile wakat unakuta asilimia 90 ya matatizo ya gari yanasababishwa na matajiri hawa
 
Back
Top Bottom