SoC02 Chama Cha Walimu Tanzania Anzisheni Chuo Kikuu cha Walimu na Bodi ya Walimu Ili Kuondoa Upungufu wa Walimu na Kuthibiti Ubora wa Walimu Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

pbwmasanja

Member
Mar 20, 2013
5
7
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ni chama cha wafanyakazi chenye sifa pekee zifuatazo kulinganisha na vyama vingine vya wafanyakazi nchini Tanzania:

  • Ndiyo chama chenye wanachama wengi kuliko vyama vingine vyote vya wafanyakazi Tanzania;
  • Ndiyo chama ambacho wanachama wake wote ni wasomi Tanzania;
  • Ndiyo chama ambacho kina wanachama kila kona ta Tanzania pote vijijini na mijini;
  • Ndiyo chama chenye rasilimali na vitega uchumi vingi nchini Tanzania;
  • Ndiyo chama cha wafanyakazi imara zaidi nchini Tannzania
Kwa kuzingatia dira ya chama hiki ya ambayo ni “Kuwa shirika lenye ufanisi wa hali ya juu katika kuwaunganisha walimu na kushughulikia kero mbalimbali zinazowahusu wanachama, linalojitahidi kuwa na mazingira bora ya kazi na ustawi wa walimu na kuwa mstari wa mbele katika kutetea na kulinda hadhi na heshima ya taaluma ya ualimu. elimu kwa wote”, Chama Cha Walimu Tanzania kinao wajibu na haki ya kuendeleza, kutetea, kulinda hadhi na heshima ya taaluma ya ualimu na elimu kwa wote.

Pia kwa kuzingatia sifa pekee kama nilivyozitaja hapo juu ukikilinganisha na chama kingine chochote cha wafanyakazi Tanzania, chama hiki kikisimamiwa na kushauriwa vema kinaweza kufanya mambo na maamuzi makubwa yenye ufanisi na tija sana.

Pamoja na madudu mengi ya Chama Cha Walimu Tanzania kama ambavyo yameishawahi kutajwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) baada ya kufanya ukaguzi kwa maelekezo ya Katibu Mkuu Kiongozi mwaka 2017, ambapo naamini uongozi madhubuti wa chama ulichukua hatua thabiti kurekebisha madudu, bado naamini kuwa Chama Cha Walimu Tanzania kinayo nafasi kubwa ya kutekeleza malengo yake kwa ufanisi na tija ili mradi tu kuwepo na utawala bora, uwazi na weledi kama inavyotegemewa kulingana na asili ya chama chenyewe na wanachama wake.

KWA KUWA:

  • Chama Cha Walimu Tanzania kutokana na michango ya wanachama ya kila mwezi pekee kina uwezo wa kukusanya pesa walau kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kwa mwezi kwa uchache;
  • Chama Cha Walimu Tanzania kinamiliki majengo yake binafsi katika kila mkoa pote nchini Tanzania;
  • Wanachama wa Chama Cha Walimu wapo katika maeneo yote Tanzania vijijini na mijini;
  • Lengo kuu la Chama Cha Walimu Tanzania ni kuwa mstari wa mbele katika kutetea na kulinda hadhi na heshima ya taaluma ya ualimu na elimu kwa wote;
HIVYO BASI Chama Cha Walimu Tanzania kwa kutumia rasilimali tajwa hapo juu na nyinginezo nyingi kilizonazo kinaweza kuanzisha vyombo vifuatavyo katika kutekeleza malengo yake kwa ufanisi na tija:

  • Chuo Kikuu Cha Walimu Tanzania (Kinaweza kuwa Huria) – Chuo hiki kitakuwa na jukumu la kuzalisha walimu wapya na kuinua taaluma ya walimu wote watakaopenda kukuza na kuendeleza taaluma zao (Nikidhania kuwa sheria na taratibu za kuanzisha chuo kikuu cha aina hii zinaruhusu);
  • Taasisi au Bodi ya Kuthibiti Kiwango na Ubora wa Taaluma ya Ualimu Tanzania kwa jina lolote mfano Bodi ya Taifa ya Walimu na Wakufunzi Tanzania kama ilivyo kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania
Kwa nini Chuo Kikuu Cha Walimu Tanzania?

  • Chuo kitawapa fursa walimu wengi waliopo kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi ngazi za juu maeneo yote ya Tanzania kujiendeleza kimasomo kwa sababu kwa uwepo wa majengo ya Chama Cha Walimu kila mkoa chuo kinaweza kuwa na matawi katika kila mkoa kwa lengo la kuwasogezea huduma walimu huko huko popote walipo ili waweze kuwa karibu na maeneo yao ya kazi huku wakiendelea na masomo;
  • Kwa kuwa walimu wanavyo vipato vya kuaminika (Mshahara), suala la ada ya masomo halitakuwa tatizo kubwa kumudu;
  • Chuo kitasisitiza katka utoaji wa walimu wa kutosha na bora katika kupunguza kama siyo kuondoa kabisa tatizo la uhaba wa walimu nchini Tanzania;
  • Chuo kinaweza kuiga na kuboresha mfumo unaotumiwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika utoaji wake wa elimu na mafunzo.
Kwa nini Taasisi au Bodi ya Kuthibiti Kiwango na Ubora wa Taaluma ya Ualimu Tanzania?

  • Ni ukweli usiopingika kuwa Ualimu ni Wito lakini kadiri siku zinavyopita suala hili limeanza kuzoeleka na kuwa ualimu ni sehemu ya kimbilio la wale ambao hawakufaulu vizuri (Hii ipo hasa kwenye kiwango cha ufaulu katika shule ya msingi na sekondari);
  • Kudhibiti shughuli na mwenendo wa walimu na wakufunzi;
  • Kuanzisha maendeleo ya awali na endelevu ya kitaaluma (IPD na CPD) na mahitaji ya kimaadili;
  • Kuendesha mitihani na kutoa sifa za Bodi iliyoanzishwa kwa walimu na wakufunzi;
  • Kutunza rejista za walimu na wakufunzi;
  • Kuendesha mfumo wa mapitio ya uhakiki wa ubora na mfumo wa uchunguzi na nidhamu; na
  • Kuweka viwango vya ufundishaji.
Yote hayo hapo juu, yaani pendekezo la kuanzishwa kwa Chuo Kikuu na Bodi vikianzishwa vitakuwa na maslahi mapana kwa taifa ilikinganishwa na uanzishwaji wa Benki ya Walimu kama ambavyo Chama Cha Walimu Tanzania kiliamua kuanzisha mwaka 2015. Ukifanya mazunguzo na walimu wenyewe utasikia wakisema kuwa tangu kuanzishwa kwa benki hiyo hakuna manuufaa yoyote yamekwishaonekana kwa wanachama wake.

Kwa kuwa sheria inakataza chama cha wafanyakazi kufanya biashara ni vema sasa Chama Cha Walimu Tanzania kwa kutumia rasilimali zake nyingi kijikite zaidi katika kutoa huduma bora kwa wanachama wake.

Kama mtapendezwa na wazo hili Chama Cha Walimu Tanzania tunawakaribisha kwetu TANZANIA BUSINESS AND SELF EMPLOYMENT CONSULTANTS tukae pamoja tuone tunavyoweza kuboresha wazo hili kwa maslahi mapama ya taifa letu. TANZANIA BUSINESS AND SELF EMPLOYMENT CONSULTANTS pamoja na huduma za ushauri na mafunzo ya biashara, ujasiriamali na kujiajiri, tunasaidia pia katika masuala ya uanzishaji na usajili wa taasisi kama tulizozitaja hapo juu, makampuni, NGO na udhamini. Hivyo pamoja na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) tunawakaribisha pia wengine wote wanaohitaji huduma zetu za ushauri na mafunzo katika biashara, ujasiriamali na kujiajiri ili kujikwamua kiuchumi na maendeleo ya taifa letu.
 
Ww jamaa ni kiazi kweli tena kiazi mbatata walimu wote hao mtaani laki na 10 hawana kazi wapo wapo tuu mtaan ukiongezea na walimu wa sayansi elfu23 wasio na ajira afu unasema waanzishe tena chuo cha walimu daaa .---ety bodi ya waalimu unaropoka ww hatar🤣😅🤣🤣🤣🤣🤪🤪🤪😂😂😂
 
Back
Top Bottom