Kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa vyuo vya VETA nchini, Kamati ya Bunge ya PAC yaishauri serikalini iajiri walimu toka India na China

Shotocan

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
2,231
4,650
Kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa vyuo vya VETA nchini kamati ya bunge ya PAC yaishauri serikalini iajiri walimu toka India na China

Waliongea hilo wakiwa Singida kukagua chuo cha VETA kilichojengwa na serikali

Wakasema Vyuo vya VETA nchi nzima vina upungufu mkubwa mno wa walimu. Miundombinu yote mizurri sana yote ipo tena ya kisasa .Tatizo ukosefu wa walimu wa VETA.

Kwa hiyo wakatoa ushauri kwa serikali iajiri walimu toka India na China ambako wako wengi tu wakati nchi ikijipanga kuwa na walimu wa kutosha wa VETA

Source: ITV habari saa moja Asubuhi
 
Kweli nchi hii haina watu wenye akili yaani watanzania hakuna tunaloliweza, Kuna Walimu kibao mtaani ni kuwapa tu fursa ya kwenda ku upgrade course waingie veta tatizo wabongo akili na ubunifu ndio tatizo.
Wabunge hadi wanaongea kuwa walimu wawe imported ina maana hawapo kwa sasa hakuna cha ku upgrade wala nini
 
Vijana wajielekeze huko kusomea ualimu wa vyuo vya VETA badala ya kusomea ualimu usio na ajira au misomo isiyo na ajira na wazazi wasomesha nje ya nchi watoto India na China wasomeshe mwelekeo huo ili kuwa na uhakika wa ajira za watoto wao
 
Serikali inapaswa iwe na mpango wa muda mrefu na muda mfupi wa kuhakikisha walimu wa Veta wanapatikana hapa hapa nchini
TUnaweza kuiga utaratibu uliotumika miaka kadhaa wakati wa utawala wa Mhe. Kiwete ukaboreshwa zaidi tukapara walimu kwa kipindi kifupi sana
 
Back
Top Bottom