Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 222
- 529
Hili ni swali ambalo kila Mwalimu na mdau wa maendeleo anatakiwa kujiuliza kabla hajafikiria kuwa ipo siku chama hicho cha wafanyakazi kitakuja kutetea maslahi ya Walimu nchini
Binafsi kwa wiki hizi mbili nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama hiki cha Walimu Tanzania (CWT) na nimebaini kuwa Walimu wengi hawakipendi chama chao. Baadhi ya sababu ni hizi zifuatazo:-
1. Viongozi wa chama hiki ni sehemu ya "chawa" wa serikali kwa maana ya kuogopa rungu la serikali wakienda kinyume na matakwa yake
2. Walimu wengi wameshapata uelewa kuwa makato ya 2% wanayokatwa kwenye mshahara wao ni makubwa na hayana msaada wa moja kwa moja kwao (Zaidi ya Bilioni nne kwa kila mwezi)
3. Chama kina mali nyingi ambazo haziwafaidishi wanachama moja kwa moja. Mfano; Jengo la Mwalimu House, Majengo kila wilaya ambayo yamepangishwa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo ofisi na biashara nk
4. Mishahara ya wafanyakazi wa chama hata wale wa chini na posho ni kubwa kuliko ya walimu
5. Viongozi wanapata nafasi kwa "kuhonga" na "kujipendekeza" kwa viongozi (hili halina ushahidi wa moja kwa moja lakini lipo)
6. Mapato ya chama ni makubwa sana (Zaidi ya Bilioni nne kila mwezi) kuliko huduma wanazopata
7. Matumizi ya fedha za chama ni makubwa na matumizi hayo si kwa lengo la kuwanufaisha wanachama. Mfano; Tamasha linalotarajia kugharimu Bilioni saba kuadhimisha miaka 33 ya chama hicho
Ikiwa chama chenyewe peke yake kinanyooshewa vidole na wanachama wake, kitawezaje kuinyooshea kidole serikali pale inapokiuka haki za walimu??
Ni wakati sasa TUCTA kama mlezi wa vyama vyote vya wafanyakazi waingilie kati kunusuru hali hii vinginevyo Walimu watakosa mtetezi katika mambo yao au laa Walimu nchi nzima "waliamshe" kwa hash tag ya "FUTA CWT, HAINA MSAADA KWA MWALIMU" halafu waanze upya!
Au mnasemaje wajameni!