Chakula cha mama Mdigo Ubungo Kibo

Chakula cha mama Mdigo Ubungo Kibo

Kuna bibi mmoja anaitwa bibi bonge pale mbele ya manjunju (luku) aisee anauza dagaa.

Kuna msururu kama wa nmb.

Mimi siku hio niliwanunua sikuwapenda na sijarudi tena ila watu wanatoka mbali sana kujazana kwa yule bibi.

Na kuna wasambaa pale royo wanauza supu kunajaa balaa kila asubuhi.
Wachunguze aisee.
Mimi siendi tena kwa wale wasambaa manake kila siku lazima niende pale.
Nina uhakika kuna kitu
Nikija Royal/loya takucheki
 
Nilijua stori yako itaishia kwenye hayo.. eeeeh
Ila huku nasubiria kuanza kuyasoma nilikuwa najiuliza ikiwa ni enzi zako vipi haukumgundua? Au alisingiziwa? Ulikuwa hujafundishwa yale?

Mimi kwa habari za kusikia kwa watu nilikutana nao huko nje ya nchi.. na haya niliyasikia sana wao wanajua kushtuka ukiwa unajua yapo. Tupe habari ya wafanya pati kila mara au mialiko ya kula kula nao mmmmh.. kama ulishaiandika.. hiyo tena na JPM kubana ikoje siku hizi nchini?

mshana jr
Wananisingizia tu Coco ... Ishu ya party za mara kwa mara ni ibada za siri kuna mada yake unajua....
Kuhusu mzee baba kubana... No comment
 
Itakuwa kipindi hicho Bado haujaanza Uganga /Uchawi, na ndio kilichokufanya uanze mana sio kwakulishwa mavi ya Mbuzi. Pia umenikumbusha story ya Mama Beleju muuza mgahawa kule Kisaki Morogoro.
 
Itakuwa kipindi hicho Bado haujaanza Uganga /Uchawi, na ndio kilichokufanya uanze mana sio kwakulishwa mavi ya Mbuzi. Pia umenikumbusha story ya Mama Beleju muuza mgahawa kule Kisaki Morogoro.
Uchawi nilianza kujifunza rasmi mwaka 1996.. Miaka 2 baadae baada ya kisa cha mama Mdigo
 
Kibo kwa wauza mikate maarufu kina Mama Juli, Kina sherode, Manka 🙂,Mshana umenikumbusha kuna Mama hapo hapo kibo alikuwa maarufu kwa kuuza maandazi, yaani akifika tu kwenye kijiwe chao wengine wote watasubiri mpaka amalize yaani watu wapo radhi wamsubiri kama hajafika wanunue kwake, na yule mama aliyekuwa anauza pombe ambaye aliteketeza familia sababu ya tamaa, Aisee kibo ilikuwa noma kipindi kile
 
Kibo kwa wauza mikate maarufu kina Mama Juli, Kina sherode, Manka 🙂,Mshana umenikumbusha kuna Mama hapo hapo kibo alikuwa maarufu kwa kuuza maandazi, yaani akifika tu kwenye kijiwe chao wengine wote watasubiri mpaka amalize yaani watu wapo radhi wamsubiri kama hajafika wanunue kwake, na yule mama aliyekuwa anauza pombe ambaye aliteketeza familia sababu ya tamaa, Aisee kibo ilikuwa noma kipindi kile
The flashbacks na bonyokwa kwa Tina bonge na China wauza gongo never miss.. Lazima kabla ya glass upate halo halo na cheni bloku (vichwa vya kuku na utumbo)
 
Kweli muda unaenda sasa hivi imebaki historia,ila kibo jamani umekumbuka yule bibi aliyevunjiwa nyumba kipindi cha upanuzi wa barabara wakatoka paka wa kutosha
Dah yeah umenikumbusha mbali.. Ilikuwa habari kubwa sana
 
Nasubiri kwa Hamu zimeshafika mbili sasa ile ya Bondeni Dispensary maarufu kwa Dr Mgaya na hii ya Ngosha Bar, nitakuwa nakukumbusha .Mshana nitakuja PM maana utakuwa na mengi kuhusu Mtaa wetu pendwa wa Kibo😉😀
Nianze na kwa Dr Mgaya... Nilikuwa na jamaa yangu anaitwa Chacha alikuwa anafanya kazi chuo kikuu cha DSM.. Basi ikawa tulikuwa tukipata pesa kidogo tunaenda bonyokwa kunywa gongo kwa Tina bonge na China .. Jamaa alikuwa na mguu mredi mfupi halafu kibonge na usafiri wetu ilikuwa pikipiki Honda 110 ya ofisini kwao... Tumeshasalimika sana kuanguka kwenye ule mlima wa bonyokwa wakati tukirudi toka uevini
Siku moja ijumaa akataka twende ila mimi sikujisikia kwenda hivyo akaenda mwenyewe... Ilikuwa alienda na mimi, nilikuwa kama handbrake yake ya kunywa... Sasa siku ile alikuwa peke yake.. Akalitwika gongo la kutosha... Wakati anarudi akapata ajali pale Bosch... Mungu bariki kuna watu wanamfahamu hivyo wakamleta mpaka home kaumia upande wote wa kushoto wenye mguu mrefu, sikio shavu mkono mkuu vyote vilikuwa vimechubuka vibaya aliburuzika kwenye lami
Jamaa wakambwaga na kuondoka... Sasa kasheshe ikawa kumtoa hapo nyumbani, kushuka naye kile kilima kuelekea kwa Dr Mgaya kuvuka ule mto kupanda mpaka kwa Dr... Halafu mvua ilikuwa imenyesha na mguu wake mzima ulikuwa umeumia
Tukiwa mimi na mkewe ambaye hata hivyo hakuwa na msaada wowote nikahangaika na MGONJWA mlevi wangu mpaka kwa Mgaya.. Sehemu ya dk zisizo zidi kumi sisi tulitumia lisaa kasoro... Mpaka tunapokewa mapokezi ikawa sio MGONJWA mmoja tena bali wawili huku tukiwa tumechafuka kwa kuteleza na kuanguka njiani... Alishonwa bila ganzi
 
Back
Top Bottom