Chakula cha mama Mdigo Ubungo Kibo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,441
2,000
Hili eneo kwa sasa sio maarufu kama miaka ile ya 80- 90. Hapa ilikuwa ndio kama kituo kidogo cha abiria wa mikoani. Wale wauza mikate wa stendi ya mkoa zamani walikuwa wanauzia pale Kibo. Ilikuwa ni lazima mabasi na hata magari makubwa yasimame kwa ajili ya kununua mikate.

Upande wa pili wa kituo kwa juu kidogo kulikuwa na banda maarufu sana la mama ntilie akijulikana kama mama Mdigo. Huyu mama alikuwa hakai mbali na hapo; alikuwa anakaa pale msikiti wa Kibo kwa bondeni kidogo

Wajihi wa huyu mama ulikuwa wa aina yake; Mrefu mnene kiasi mweupee, kisha mashaallah akajaaliwa nyonga na mguu. Mama Mdigo kwenye banda lake alikuwa anasaidwa na mabinti zake wawili, Mishi na Ashura. Hawa ilikuwa ni C&P toka kwa mama yao kuhusiana na swala zima la wajihi na maumbile (shape) kiuno nyonga ya nyigu nakazalika mbili. Alikuwepo pia binti mwingine wa kazi, Binti wa kizaramo.

Banda la mama Mdigo lilikuwa linafurika kuanzia asubuhi kwenye kifungua kinywa mpaka mchana lunch time. Jioni alikuwa hapiki. Madereva wa mikoani walikuwa wanapaki ili wale kwa mama Mdigo kabla ya kuendelea na safari. Watu walipasifia na kupapenda sana kwa mama Mdigo kutokana na chakula chake kitamu halafu bei poa.

Menu yake ilikuwa wali wa nazi, samaki sangara au nyama vilivyoungwa na nazi pia, mboga ya majani na maharagwe ya nazi; yalikuwa matamu mno. Utamu mpaka utosini, ladha mpaka kwenye kope...!!! Ugali wa kukoboa, usafi wa vyombo na banda bila kusahau uchangamfu wa mama na mabinti zake.

Menu yote hiyo ilikuwa shilingi za kitanzania 300 ugali na 350 wali na mboga yoyote kati ya nyama ama samaki. Maharagwe ilikuwa ni must iwe umekula ubwabwa au iwe umekula ugali.

Nikiwa naishi gheto mtaa wa Rombo kama unaenda bondeni kwa Doctor Mgaya enzi hizo. Nikajikuta nakuwa mteja mkubwa wa chakula cha mama Mdigo. Nilikuwa mteja mzuri kiasi kwamba ilifika mahali nikawa nalipa kwa wiki na ikafika mahali hata weekend nikienda kuwatembelea ndugu labda niende baada ya lunch lakini nikienda kabla ukikaribia muda wa chakula nitatoa visingizio nisile ili nikale kwa mama Mdigo.

Baada ya mwaka nilihamia Mtoni kwa Aziz Ally karibu na uwanja wa Sifa lakini huwezi kuamini ilikuwa siwezi kumaliza wiki lazima nitoke Mtoni kwa Aziz Ally mpaka Ubungo kibo kisa tu kufuata chakula cha mama Mdigo. Yani kile chakula kilikuwa na mvuto wa ajabu. Cha kushangaza tu ni kwamba kilikuwa hakinenepeshi

Miaka ile ya 93/94 ndio tulianza kuwa na vituo vya luninga, wakati huo vikiwa ni DTV na CTN na wamiliki wa TV walikuwa wachache mno. Ni kipindi hicho pia ishu za kutolewa uchawi na chumaulete zilikuwa maarufu sana.

Jioni moja tukiwa tumekusanyika bar moja inaitwa Zebra kwa mzee Mushi tunaangalia luninga (Bar yake pekee maeneo hayo ndio ilikuwa na tv). Mara kupitia DTV habari namuona mama Mdigo eti katolewa uchawi na ya kwamba alikuwa kazindika madawa ya mvuto kwenye banda lake (matunguli yakaoneshwa) halafu alikuwa anatumia mkono wa binadamu kama mwiko wake (tukaoneshwa mwiko wa kawaida). Kubwa kuliko yote ni eti maharagwe aliyokuwa anatulisha hayakuwa maharagwe halisi bali mavi ya mbuzi. Mama Mdigo alikuwa na mbuzi wengi sana pale kibo nyumbani kwake. Huu ulikuwa ndio mwisho wa mama Mdigo na mabinti zake wawili. Miezi michache baadae pale kwenye banda lake palivunjwa kupisha upanuzi wa barabara.

Baada ya tukio lile nikaamua rasmi sasa nianze kuwachunguza mama ntilie. Nikagundua wanasingiziwa mengi Lakini pia mengi yapo yenye ukweli

1. Wengi hawana elimu hivyo kwao suala la mvuto kibiashara sio usafi na huduma bora bali ni kutafuta mvuto kwa waganga wa kienyeji
2. Wengi hawajiamini hivyo kutafuta kinga kwa waganga ili biashara itoke lakini pia wasirogwe na wenzao
3. Wengi huogopa chuma ulete na kukopwa.. Hivyo hutumia tiba mbadala kujikinga na hizo hali
4. Wengi hupenda kupika kidogo lakini auze sana na faida iwe hata mara tatu.. Kumbukeni wali au ugali wa hamira.. Sasa hii ni cha mtoto

Wanafanyaje sasa
- Kwenye mvuto ndio kama hivyo kupikia maji liyoogea
- Kuweka vipande vya nyama sehemu za siri kwa muda kisha kuchanganya na vingine wakati wa kupika
- Kuchanganya mboga na vitu kama mavi ya mbuzi nk
- Kupikia wateja nyama tofauti na ya ng'ombe mbuzi kuku nk

Kwenye kinga
- Kutumia viungo vya binadamu kupikia
- Kuchanganya chakula na kitu kama yai viza nk
- Kuchanganya kwenye chakula madawa yasiyoeleweka yametengezwa na nini nknk

Utagunduaje kama huyu mama ntilie sie
- Unaona kabisa chakula chake ni cha kawaida kabisa lakini kinagombewa
- Unaona kabisa banda lake halina hadhi na huduma za usafi haziridhishi Lakini utakuta watu wamepiga foleni
- Utakuja hata siku moja sio yeye, familia yake au watu wake wa karibu wanakula hicho chakula... Wapishi wa chapati na vitumbua wana hizi sana

Mama ntilie asiyethubutu kula chakula chake hata ukimpa ofa jitenge naye ila yule anayejumuika kula na hata na wafanyakazi wake huyo si mbaya. Mpaka leo hii sijui ukweli kuhusu mama Mdigo na chakula chake ila tu kilikuwa na jambo la ziada.. Ni lipi? siwezi jua......
 

ganja man

Member
Sep 1, 2017
19
75
Dah mkuu ni kweli n hayo mamboz yapo hapa kijiweni kuna mdada anauza kwelikweli ila muda wa kula yy anaend nunua soda n mkate ama anasong ugali wake ukut anakula kile anachotuzia si yy wala mabinti zake. Niliwai wauliza kwann awali nikajibiwa chakula ukipika kinakinaisha
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,441
2,000
Dah mkuu ni kweli n hayo mamboz yapo hapa kijiweni kuna mdada anauza kwelikweli ila muda wa kula yy anaend nunua soda n mkate ama anasong ugali wake ukut anakula kile anachotuzia si yy wala mabinti zake. Niliwai wauliza kwann awali nikajibiwa chakula ukipika kinakinaisha
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
6,691
2,000
Kuna bi farashuu kino pale mtaa wa mafere ,miaka hiyo anauza chipsi mayai tu, mishkaki kuku njoo nayo mwenyewe.
Ilo foleni sasa, huyu bibi Ali mmario ben kinyaiya mda mrefu sana kipindi hiyo dogo anasoma jitegemee.
Pia ma kishori pale A, akimaliza kupika kitumbua cha mwisho kimenunuliwa.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,441
2,000
Kuna bi farashuu kino pale mtaa wa mafere ,miaka hiyo anauza chipsi mayai tu, mishkaki kuku njoo nayo mwenyewe.
Ilo foleni sasa, huyu bibi Ali mmario ben kinyaiya mda mrefu sana kipindi hiyo dogo anasoma jitegemee.
Pia ma kishori pale A, akimaliza kupika kitumbua cha mwisho kimenunuliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom