Chaguzi za CCM: Undugunisation au majina kufanana tuu?

Hapo kwenye Sofia Simba HAKUNA UHUSIANO WOWOTE wa wawili hao, Sofia Simba ni mtu wa Morogoro na huyo Iddi Simba nadhani ni mtu wa Kigoma, namjua Sofia Simba Ndani nje ! hawana uhusiano wowote na Idi Simba, hao wengine sina uhakika kabisa !
 
Hapana, Sofia Simba aliwahi kuwa mke wa Kigogo mmoja alietamba sana enzi za miaka ya 80 mpaka 90 na alijaaliwa kuwa nae mtoto mmoja. Sidhani kama jina lake limefanya awe hivo chunguza zaidi Kigoli wangu.
 
Shida kubwa ya huu undugunisation hauishii kwenye kupeana vyeo tu. Wanapeana tenda kubwakubwa za serikali; wanapeana AJIRA nzuri serikalini na kwenye taasisi za UMMA; wanapeana ELIMU bora kabisa;...., ili mradi ionekane kuwa mbwa wa mtemi naye ni mtemi wa mbwa wote! Kama hali ni hii, tuendako sio salama sana.
 
Ila walipita bila kuulizwa wala kuhojiwa kwenye VITI MAALUM. CHADEMA walikosea kwenye hili kwa kigezo chochote walichotumia. Haikuwa bahati mbaya.
 


Salma Rashidi KIKWETE

Ridhiwani Jakaya KIKWETE

Hawa ni ndugu na Jakaya Kikwete (M/Kiti wa CCM taifa) au ni majina tuu?
Good Observation Mwali..ila hayo majina yasikutishe, yamefanana tu hawana uhusiano kabisa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Huyo Salma Kikwete alikuwa na Mwalimu wa Shule fulani hivi ya msingi ila nasikia siku hizi ana NGO yake, pia angekuwa na uhusiano wowote na Mkuu ungemuona ona kwenye misafara yake katika siku za hivi karibuni.
Ridhiwani Kikwete hata mimi mara ya kwanza nilikuwa ninadhani ni mtoto wa rais mpaka ile siku alipokanusha kumiliki mali na hela nyingi na kudai yeye anaishi kimjini mjini yaani kimesheni town.
 
hapa zinatakiwa data watu wasianze tena matusi kwa lengo la kupoteza mwelekeo wa thread
 
Good Observation Mwali..ila hayo majina yasikutishe, yamefanana tu hawana uhusiano kabisa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Huyo Salma Kikwete alikuwa na Mwalimu wa Shule fulani hivi ya msingi ila nasikia siku hizi ana NGO yake, pia angekuwa na uhusiano wowote na Mkuu ungemuona ona kwenye misafara yake katika siku za hivi karibuni.
Ridhiwani Kikwete hata mimi mara ya kwanza nilikuwa ninadhani ni mtoto wa rais mpaka ile siku alipokanusha kumiliki mali na hela nyingi na kudai yeye anaishi kimjini mjini yaani kimesheni town.
Sema tu kukaa sana IKULU au kupitapita mle kunakufanya uwe mwanaSIASA na KIONGOZI mzuri sana! Akili zinaongezeka, unapendwa na watu, unachagulika au unapita bila kupingwa, unakuwa na vipaji hata ambavyo haukuzaliwa navyo!
 
Namuomba msajili akibidili hichi cha kiitwe "CHAMA CHA NDUNGU"

kumbe ndio maana wengine waliona waachane na siasa uchwara!
 
Iliyobaki sasa ni KATIBA MPYA ijayo itambue uwepo wa MKE na WATOTO wa Rais au Mwenyekiti wa CHAMA. Kokote watakakojitokeza kugombea wapite bila kupingwa.
 
Hizo hasira sasa sijui utaenda chama gani Chadema nako utakutana Tundu Lissu, Christian Lissu, Philemon Ndesamburo, Owenya Ndesamburo, Mke mkubwa wa Dr Slaa, Rose Kamili Slaa.

Vipi hawa sio ndugu zako Josephat Manyerere, Vicent Nyerere, Leticia Nyerere.

shindwa na ulegee .usithubutu kuhusisha uchafu unaoendelea ndani ya nchi hii .chini ya uongozi wa kikwete ,na Baba wa taifa JK NYERERE .mmepatia mnakula sasa usifikie kutaka kunya kwenye sahani ya chakula ,
 
Nifuatilie wapi ebu tuambie kwa faida ya JF Mbowe aligombea na nani cheo cha uenyekiti wa taifa...usilete mapenzi kaka.
Point is, hakurithishwa kama unavyotaka kutuaminisha. Kulikuwepo na wenyekiti wangapi tangu Mzee Mtei aachie uongozi?
 
Kama ulimsikiliza vizuri Mkuu wa Kaya Dr,Mh,Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake kwa wanachama wake wanaogombea nafasi mbalimbali katika chama chetu aliwatakia kila la kheri wale wooote wenye kutaka kuondoka kwa sababu ya majina yao kuondolewa katika uchaguzi huu na hasa wale (WAZEE) akasema zamu hii anataka kundi la kuleta ushindi nalo ni la VIJANA zaidi, ambao kimtazamo ni vijana wasomi wa viongozi wenzake ndani ya chama chetu Watoto wetu ambao wataweza kulinda maslahi ya chama chetu CCM na ulaji wetu pasipo kuingiliwa na mtu pembeni ambaye hajui ngoma inayopigwa hujui tunavyoicheza ndio maana mkuu unaona Majina yanayofanana. Huo ni Ukoo wa Chama Cha Mapinduzi utakaoleta ushindi,Mshikamano,katika chama.ukiona jina lako halipo hapo haraka tafuta ukoo wako uko wapi katika Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania usingoje wakati ni huuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Pole yako, muda mwingi hawa huwa na raslimali za kuwafikisha huko na vigogo wa kuwakingia kifua ikibidi
 
Mke wa Rais (Mwenyekiti wa Chama) kuchaguliwa kwenye Chama si tatizo! Maana anaweza kuwa na sifa zinazotakiwa na huwezi kumnyima haki yake ya kugombea kwa sababu tu eti ni mke wa Rais/Mwenyekiti. Tatizo ni mfumo wa kuchaguana ndani ya Chama - je mifumo iko tayari kuhakikisha kuwa huyu hachaguliwi kwa kuwa tu ni mke wa Rais/Mwenyekiti. Kwa sababu hazuiwi kugombea kwa sababu tu ni mke wa Rais/Mwenyekiti lakini pia hachaguliwi kwa kuwa tu ni mke wa Rais/Mwenyekiti. Undugunization unakuja pale tu ambapo kuwa na uhusiano na kiongozi fulani ni sifa pekee ya kuchaguliwa! Ndio falme zilivivyo. Unazaliwa mtoto wa mfalme basi hiyo ni sifa tosha kukufanya uwe mfalme - huhitaji kingine chochote.

Sasa kwa Lindi mjini na Bagamoyo, ndio sehemu pekee wagombea wanasimama bila kupingwa na wote wawili wana sifa moja inayofanana - wana uhusiano na Rais/Mwenyekiti. Hiyo peke yake haitoshi kuhalalisha undugunization. Swali je mfumo wa uchaguzi ulikuwa tayari kuhakikisha kuwa hawapendelewi. Tufanye uchunguzi mdogo tu. Je wapo wana CCM waliojitokeza wakashinikizwa wasigombee? Katika chaguzi zetu inwezekana mtu akataka kugombea lkn akapigwa mkwala asithubutu? Na wangegombea wengine, katika mfumo huu, nafasi zao kushinda zingekuwaje? Maana wengine wanaweza kusema 'ah unagombea na mke wa Mwenyekiti, utapata kweli?'.
 
CCM NA cdm vyote vimeoza ... ni walewale hawana jipya!!
Sitaki kusikia siasa zao za kipuuzi tena!!

Pole Kobelo,
wakati wenzako tunajiandaa kuufikia ukombozi wa hizo koo za kisultani wewe unakata tamaa! ole sana.
CDM ni wasakaji wa ukombozi ni lazima waende kama watu wa kundi moja lililo imara kwa ajili ya kupambana na adui maonevu, wezi, mafisadi, walafi, waroho, na wauaji, CDM wanahitaji nguvu hiyo ya pamoja. Ndio waliokutana kwanza na kuwa na mawazo mamoja na waliomiminiana, na wakajiamani, sasa wametoka nje na sisi tumewaamini tunawaunga mkono na wao wametukubali wametupokea sasa wanatoa nafasi kwa yeyote aliye kati yao na aende aombe kukubalika kwa wananchi achaguliwe, ndipo sasa tunawaona akina Silinde, safari, n.k. na wewe Kobelo nafasi yako ipo wazi kabisa, labda hujajitambua tuu.
mleta mada anasema jina lake limekatwa anadhani labda kwa kuwa jina lake la ukoo halifanani na hao waliopo na waliokuwepo, sasa haamini kwamba chama hicho kipo kwa wananchi tena ingawa chama hicho kimeanzaniashwa na watanzania wote 2007.
Kwa kweli CDM ni chama kinachokupa nafasi wewe na jirani yako kagombee na utashinda hayo hutayaona wala hutakatwa bwana kobelo..................Peoplesssssssssssssss Power.
 
Vipi hawa sio ndugu zako Josephat Manyerere, Vicent Nyerere, Leticia Nyerere.
Hilo jina la Vicent Nyerere hatulijui na wala sio ndugu wa baba wa Taifa- B. W. Mkapa
 
Back
Top Bottom