CHADEMA yatangaza kutomtambua John Tendwa

CHADEMA yatangaza kutomtambua John Tendwa

Hebu tumfuatilieni Adrian Stepp kwanza. Atakuwa anahoji mtu sahizi na naamini ambao bado wana maswali, majawabu yake yatapatikana hapo.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni kwamba Dr Slaa ajitambui? au ni hurka tu ndio zinamfanya afanye hayo maamuzi?

Kwa hali tu ya kawaida, huwezi kusema unaitambua ofisi pasipo kumtambua mwenye mamlaka na ofisi husika.

Mbona sheria ipo wazi na imesema kutakuwapo na msajili wa vyama vya siasa, na hili liko wazi kwa sasa ni jaji Tendwa.

Dr Slaa usinifanye niamini kuwa ni ubabu ndio unakupereka puta!

Umevurugwa wewe sio bure. Go Dr. Wa Ukweli Go never give up magamba wamelekea kibra. VIVA CDM
 
Kwasababu Chadema hawamshiriki tena Tendwa katika mambo mengi yanayohusiana na ofisi yake badala yake wanafanya mawasiliano au hata kutuma barua,kupata go-ahead kupitia maofisa ya ofisi ya msajili na sio Tendwa tena.CHADEMA haihitaji tena baraka za Tendwa kufanya mambo yao ikiwemo suala la Red Brigade ila ofisi yake ina taarifa nayo na ilishatoa baraka.Swali lingine?




kaka umeelewa vibaya sana, John kama John chadema haimtambui, lakini Ofisi ya msajili inayoongozwa na sheria au na katiba ya jamuhuri ya muungano , inatambuliwa. Ofisi ya msajili huwa hailopoki hata siku moja inafanya kazi kutokana na sheria zilizopo.
 
CHADEMA ni intrinsic ndani ya mioyo ya watu iko kwenye damu za watu hata ikifutwa kwa msajili pale ofisini DSM lakini itaendelea kuwepo Kigoma, Mwanza, Arusha, Kagera na Kilimanjaro regardless chuki dhidi ya chama hiki. CHADEMA ni invisible wall mahara popote ipo na hata viongozi wa serikali wanaihisi popote wawapo. Tendwa anajidanganya tu sawa sawa na kulazimishwa baba wakati mwenyewe rohoni na pengine DNA zimeshathibitisha hivyo
 
Safi sana upara bila elimu ni sawa na kovu tu...tendwa ni janga na ni mchochezi namba moja!!
Mnakumbuka wakati wa ubunge Arumeru alisema katumwa na wazee wa Meru juwa amuambie Lema asiruke kwao? Kilichotokea mnakijua Lema alikewnda kufanya kampeni na wazee walimkaribisha! Hivi huyu mzee mwanya wake kama kigoli anauringia sio?
 
Source yako ni reliable?
Tehe tehe tehe

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimetangaza kutomtambua msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa na kusema wao walishamfuta kabla ya yeye hajakifuta chama hicho.

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr. Willbroad Slaa amesema wao hawatishwi na kauli ya msajili John Tendwa ya kukifuta chama hicho maana wao wanaitambua ofisi ya msajili wa vyama vya siasa tu na si John Tendwa.

Amezungumza hayo hii leo jijini Dsm wakati wa uzinduzi wa kongamano la kimataifa la vijana kuhusu demokrasia.


Source: Mimi mwenyewe!

For more info: Tazama HotMix ya EATV!



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
slaa anaham chadema ifutwe arudi ccm na sisi hatumtaki mhangaikaji wa maisha mara padr,mara ccm, mara chadema .mara ndoa .mara nyumba ndogo. hatulii huyu mzee anamatatizo gan kichwan
 
Wewe ndio unachanganya mambo, ipo tofauti kati ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na msajili wa vyama vya siasa, tena kubwa tu,
Hivi ni kwamba Dr Slaa ajitambui? au ni hurka tu ndio zinamfanya afanye hayo maamuzi?

Kwa hali tu ya kawaida, huwezi kusema unaitambua ofisi pasipo kumtambua mwenye mamlaka na ofisi husika.

Mbona sheria ipo wazi na imesema kutakuwapo na msajili wa vyama vya siasa, na hili liko wazi kwa sasa ni jaji Tendwa.

Dr Slaa usinifanye niamini kuwa ni ubabu ndio unakupereka puta!
 
acha kupotosha umma pitia katiba uone sifa za mtu kuwa msajiri ili ulinganishe na namba 2 yako

hii adhabu itamtesa sana Tendwa, Tendwa alipuuzwa na sasa amefutwa rasmi. hizi si adhabu ndogo ni sawa na mwanao kukwambia kuanzia leo sikutambui kama baba yangu, unatakiwa ujiangalie mara mbili. Tendwa amejiingiza kwenye siasa badala ya kutenda haki. Tendwa anasema ana uwezo wa kuifuta chadema lakini hawezi kuifuta ccm hata kama itakutwa na kosa linalopeleke kufutwa.

Tendwa amejikuta anafanya kazi za Nape nnauye badala ya kufanya kazi za msajili. ni lini Tendwa ameshawai kutoa wasia hata kwa ccm kufanya siasa safi?
 
slaa anaham chadema ifutwe arudi ccm na sisi hatumtaki mhangaikaji wa maisha mara padr,mara ccm, mara chadema .mara ndoa .mara nyumba ndogo. hatulii huyu mzee anamatatizo gan kichwan

Slaa amesema Tendwa hatambuliki wewe umechanganyikiwa namna hii?
 
Hivi ni kwamba Dr Slaa ajitambui? au ni hurka tu ndio zinamfanya afanye hayo maamuzi?

Kwa hali tu ya kawaida, huwezi kusema unaitambua ofisi pasipo kumtambua mwenye mamlaka na ofisi husika.

Mbona sheria ipo wazi na imesema kutakuwapo na msajili wa vyama vya siasa, na hili liko wazi kwa sasa ni jaji Tendwa.

Dr Slaa usinifanye niamini kuwa ni ubabu ndio unakupereka puta!
Dr.W.Slaa ana kila sababu ya kuendelea kukubalika miongoni mwa watanzania! Anasimamia kwa vitendo mambo yote ambayo chama chake kinaamini ni sahihi.
 
Last edited by a moderator:
punguzen jazba siasa sio vita.tz sio kivu.slaa anahulka ya fujo tangu zaman

We m23 umemfahamu DR.SLAA tangu mwaka gani maana wengine(e.g HAMY-D,paulss n.k) mnajivik unazi wa kikada kumbe ni chura mjifunza kuogelea!
 
Chadema waonyesha picha za video alivyouawa Mwangosi;Picha zinaonyesha jinsi RPC Iringa alivyoshuhud
JUMATATU, SEPTEMBA 10, 2012 05:45 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

*Picha zinaonyesha jinsi RPC Iringa alivyoshuhudia tukio
*Zinaonyesha baada ya Mwangosi kuuawa, polisi walilaumiana
*Waandishi wa habari, viongozi wa Chadema waangua vilio
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeonyesha picha za mnato na video zinazoonyesha jinsi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Television cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, alivyouawa.

Picha hizo zilionyeshwa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa pia na waandishi wa habari. Kikao hicho cha Kamati Kuu kilikuwa ni cha dharura na kilifunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Wakati picha hizo zikionyeshwa wazi wazi, viongozi wa CHADEMA na waandishi wa habari, walishindwa kujizuia kwani baadhi yao walijikuta wakiangua vilio wakionyesha kusikitishwa na jinsi Mwangosi alivyouawa.

Katika tukio hilo, Mbowe ni kati ya waliolia na ilifika wakati akanyanyuka kutoka meza kuu na kwenda nje ya ukumbi, ili asiendelee kushuhudia Mwangosi alivyouawa.

Wakati picha hizo zikionyeshwa kwa zaidi ya masaa mawili, askari polisi walioshiriki kumuua Mwangosi walionekana wazi wazi na pia Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alionekana pia eneo la tukio akishuhudia Mwangosi akiuawa.

Kwa mujibu wa picha hizo, mwandishi wa habari aliyeanza kukamatwa na askari polisi na kupata kipigo ni Godfrey Mushi wa Gazeti la Nipashe.

Picha hizo za video zilionyesha kuwa, baada ya Mushi kukamatwa, Mwangosi alikwenda kumuokoa mwenzake huyo na alipofika eneo la tukio, askari hao walianza kumpiga na hatimaye kumuua mbele ya Kamanda Kamuhanda.

Picha hizo zinaonyesha kuwa, kabla Mwangosi hajauawa, polisi mmoja alipitisha bunduki yake miguuni kwa polisi mwenzake kisha Mwangosi akauawa.

Baada ya tukio hilo, picha hizo zinaonyesha kuwa, baadhi ya askari polisi waliokuwa wakimpa kipigo Marehemu Mwangosi, walikimbia na kuacha mwili wa marehemu ukiwa vipande vipande.

Kwa mujibu wa picha hizo, polisi hao walipokuwa pembeni, wenyewe kwa wenyewe walianza kulaumiana huku baadhi yao wakimlaumu muuaji na kusema umefanya nini hicho?.

Baada ya hapo, mmoja wa polisi hao alisikika akisema twende tukamchukue mwenzetu na walipofika mahali alipokuwa mwenzao ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa bomu lililomuua Mwangosi, gari ya Kamanda Kamuhanda ilisogea karibu na kumpakia askari polisi aliyejeruhiwa.

Picha hizo za video ambazo zinaonekana zilirekodiwa kwa umakini wa hali ya juu, zinaonyesha baada ya mauaji hayo, askari walishikwa na butwaa huku baadhi yao wakionekana kushika pua.

Wakati hayo yakiendelea baadhi ya askari ambao ni wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walionekana katika mkanda huo wa video, wakifungua kofia zao zilizokuwa zimefunika uso na macho yao, ili waone vizuri maiti ya Mwangosi iliyokuwa vipande vipande.

Wakati wakivua kofia hizo, baadhi yao walikuwa wakinawa nyuso zao kutokana na moshi uliokuwa umesambaa eneo la tukio wakati walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA.

Pia picha hizo, zilionyesha askari polisi mmoja akiwa amevaa kiraia, huku shingoni akiwa na skafu ya CHADEMA lakini baada ya vurugu kuanza, askari huyo alionekana akiivua skafu hiyo na kuiweka mfukoni.

Alipoivua na kuiweka katika mfuko wa nyuma wa kaptula aliyokuwa amevaa, mwenzake mmoja akampa kofia ya kujikinga na moshi kisha askari huyo akachomoa bastola kwa ajili ya mapambano.

Pamoja na picha hizo kuwaonyesha askari polisi walivyotekeleza tukio hilo, Kamanda wa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) wa CHADEMA, Benson Kigaila, alionekana pia akijibizana na ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Iringa kuhusu wafuasi wa CHADEMA kuwepo katika Kijiji cha Nyololo kilichopo Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.

Vile vile, picha hizo za video, awali zilionyesha marehemu Mwangosi alivyokuwa akimuuliza Kamanda Kamuhanda kuhusu sheria ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na maswali hayo yalionyesha jinsi kamanda huyo wa polisi alivyokuwa amechukizwa nayo.

Kutokana na picha hizo, Mbowe alisema huo ni ushahidi wa kutosha kuonyesha jinsi Jeshi la Polisi lilivyokuwa limedhamiria kuua.

Kwa mujibu wa Mbowe, CHADEMA itatoa tamko zito leo kuonyesha ni hatua gani zitachukuliwa baada ya kifo cha Mwangosi.



KABLA YA PICHA
Awali, akifungua kikao hicho, Mbowe alisema ajenda zitakazojadiliwa na kutolewa tamko ni za kitaifa, kijamii na kiusalama kwa manufaa ya wananchi wote.

Mbowe alianza kutoa pole kwa waandishi wa habari nchini kutokana na kifo cha Mwangosi na kuwataka wawe wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kamati imeundwa kuchunguza tukio hilo.

"Kifo cha mwenzenu marehemu Mwangosi kimetugusa sote, ninachoweza kusema ni kwamba, kimesababishwa na Jeshi la Polisi kwa lengo wanalolijua wenyewe, lakini najua wanataka kuwadhoofisha.

"Jambo jingine ambalo napenda kuwaeleza waandishi, ni kwamba sote tunafahamu Rais Jakaya Kikwete alivyo mwepesi kutoa pole na kuhudhuria pale panapotokea msiba, lakini hadi sasa kitu hicho hakijafanyika.

"CHADEMA tunalaani sana kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kutoa pole hata ya kauli, huku akijua tukio hilo limegusa watu wote duniani, tunashangaa kuendelea kutatua migogoro ya nchi nyingine, huku ya kwetu yakitushinda.

"Hakuna asiyefahamu kuna migogoro ya walimu, madaktari, wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakulima, wafugaji na wananchi kwa ujumla, lakini hakuna jitihada zozote zinazofanyika kutatua badala yake tunaendelea kuongeza matatizo mengine," alisema Mbowe.


KAULI YA TENDWA
Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, aliyesema wiki iliyopita, kwamba atakifuta CHADEMA kama mauaji yataendelea kutokea kwenye mikutano yao, Mbowe alisema haitawezekana chama hicho kufutwa vinginevyo ni kuhatarisha amani ya nchi.

Mbowe alisema, mpango wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia vyombo vya dola kama polisi na viongozi kutaka kuzuia mikutano ya M4C inayoendelea nchi nzima, hautafanikiwa.

"Tendwa asijaribu kutoa kauli za kuhatarisha amani ya nchi, kama ni kufuta vyama aanzie CCM, CHADEMA sio chama cha mfukoni, kama amelewa na usajili wa vyama na kuwa kibaraka wa CCM sasa amekanyaga pabaya.

"Napenda kutangaza rasmi kwamba, mikutano ya M4C itaendelea nchi nzima na hakuna mtu anayeweza kuizuia, tunataka kuleta demokrasia na mabadiliko ya kweli.

"Serikali ya CCM isijaribu kuleta machafuko nchini, itambue kwamba, CHADEMA ina mamilioni ya wafuasi na kila siku wanaendelea kuongezeka na kama Serikali hii itaendelea kulea ufisadi, wizi, ubabaishaji, mauaji na kushindwa kuwajibika kwa wananchi, ijue mwisho wake umefika, hakuna cha kulindana," alisema.



TUZO KWA WAANDISHI
Akizungumzia picha zilizopigwa na waandishi wa habari siku ya tukio la mauaji ya marehemu Mwangosi, alisema wanastahili kupatiwa tuzo.

Mbowe alisema kuwa, CHADEMA kinaandaa tuzo kwa waandishi wa habari waliopiga picha za video na mnato katika tukio la mauji ya marehemu Mwangosi.

"Waandishi wa habari wameonyesha uhodari mkubwa sana licha ya kuwa katika msukosuko wa mabomu ya polisi, picha zilizopigwa zimeondoa dhamira chafu ya polisi na Serikali ya CCM, kutaka kutumia mwanya huo kukichafua CHADEMA, picha zote za mnato na video zimeonyesha ukweli wa jambo na wahusika.

"Sisi kama CHADEMA tunathamini mchango wa vyombo vya habari na umuhimu wake na ni mtaji mkubwa sana kwetu, tumesikia waandishi wanatafutwa hatutasita kuwasaidia na mpaka sasa tupo sambamba katika hili," alisema.


AISHUKIA TBC
Katika hali nyingine, Mbowe alionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kwa kusema kuwa limekuwa likifanya kazi ya kuibomoa CHADEMA badala ya kueleza ukweli ulivyo.


DK. SLAA
Naye Katibu Mkuu CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa alikiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Said Mwema na kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa.

Alisema alituma ujumbe huo baada ya kuzuiwa barabarani na polisi wakati wakiwa katika mikutano ya M4C.

Alisema baada ya kuzuiwa na kushushwa kwenye magari yao wakiwa mkoani Iringa na kulazimishwa kutembea kwa miguu hadi hotelini, aliamua kumpigia simu IGP Mwema na kumuelezea jambo hilo, lakini hakumjibu na ndipo alipoamua kumtumia ujumbe huo mfupi.

Hata hivyo alimtaka IGP Mwema na Tendwa kueleza chanzo cha kutuma ujumbe huo na kuachana na tabia ya kupotosha jamii.

Alisema kama kweli sms hiyo aliituma kwa uchochezi ni vema wamkamate na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

​
Tendwa, Polisi na TBC.......ni matawi ya CCM
 
bichwa la tendwa limejaa ugoro tu kwanza muda wake umekwisha sijui anasubiri nini
 
Msajiri alopoki,anafanya kazi kulingana na sheria na procedures zilizopo, haina haja ya tendwa kupiga mkwara jukwaani, kama kweli chadema kinaenda kinyume na procedures au Sheria atumie sheria zilizopo kukiadhibu chadema ,Siyo kuropoka majukwaani. Inaonekana Tendwa yupo kipropaganda za ccm. kama kweli yupo kwa maslai ya wananchi ,basi atumie procedures na sheria zilizopo kuiadhibu Chadema. Siyo kulopoka lopoka tu. DR. Slaa yupo sawa, big up

Hiyo ndio shida ya mtu kuendelea kukaa ofisi ya umma wakati umli umemtupa huyu NDWATE/TENDWA alitakiwa kupumzika. VIVA CDM
 
Back
Top Bottom