Chadema yataka JK alaani uporaji wa madaraka Ivory Coast | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yataka JK alaani uporaji wa madaraka Ivory Coast

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 19, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kurugenzi ya mambo ya Nje ma Mahusiuano ya Kimataifa ya Chadema imeitaka serikali kulaani hadharani matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya kidemokrasia ya kimataifa unaofanywa na Laurent Gbagbo na wafuasi wake nchini Ivory Coast.

  Aidha, kurugenzi hiyo inatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kutamka hadharani kumtambua Alassane Ouattara kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais katika nchi hiyo na kulaani vitendo vinavyofanywa na Gbagbo na wafuasi wake.

  Taarifa iliyotolewa na Mkrugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya kimataifa ya Chadema john Mnyika ilisema:

  “Inashangaza kwamba wakati Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na serikali za nchi mbali mbali ndani na nje ya Afrika zimetoa matamko ya wazi, serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya diplomasia ya kimya. Hii ni tofauti kabisa na wakati wa Mwalimu Nyerere ambapo Tanzania ilikuwa mstari wa mbele na kutoa misimamo ya wazi ya kukemea vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.”………………………………………………………………..


  …………..Habari katika Nipashe katika Nipashe Jumapili.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mkuu siyo inafanana na hii
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  JK hawezi kutoa la namna hiyo bila ya kujiuma mdomo, kwani hadi sasa chama chake kinaendeleza unporaji, au tuseme unyang'anyi wa halmashauri mbali mbali hapa nchini. Labda akishamaliza shughuli hiyo ndiyo atatamka.
   
 4. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Thubutuuu!hawezi kulaani anayoyafanya Bagbo coz hata yeye alifanya hayo hayo,nafsi inamsuta.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Chadema sio wa kumtaka JK afanye nini, wao si hawamtambui? Na au hawatambui namma alivyochaguliwa? Sasa leo vipi? Au ndio kujipendekeza kwenyewe huku?

  Au ndio wamesha "rudi"?
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  JK hana moral authority ya kufanya hivyo!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sasa si tume yake aliyoiteua ilimtangaza kuwa Rais hata baada ya CDM kuiandikia isitangaze matokeo? Kwa kuwa ni Rais wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, atoe tamko tu ili mwenzake anayeng'ang'ania madarakani Gbagbo amwambie kuwa "na wewe mbona unang'ang'ania madarakani!"
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kabla hajalaani mporaji mwenzake basi lazima ajiuzulu kwanza. Tofauti ni kwamba JK amelindwa na katiba, lakini wote wawili ni majambazi wa kura
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kutoka wapi?Mecca kutoka kuhija!!!teh teh teh!!
   
 10. D

  DENYO JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli hana uwezo kusema lolote dhidi kwa kuwa kilichotokea ivory cost ni copy and paste, sema kule ivory cost nec ilikuwa huru ila yakafanyika mapinduzi. Tanzania daima ilionesha kuwa hapa pia yalikuwa mapinduzi kwahiyo jk mutamwonea hana moral authority ya kulaani manake akisema tuu gbabo naye atasema mjomba hata wewe???
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  mmh yaani nanii amkemee nanii mwenzake? sijui kama itawezekana yangu masikio.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  JK mwenyewe mwizi wa kura sasa anapata wapi nguvu za kumkemea mwizi mwenzie
   
 13. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nyoooo !
   
 14. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Yeye mwenyewe kapora ushindi wa uchaguzi mkuu na anaendelea kupora ushindi kwenye umeya, sasa huo ubavu wa kutoa tamko ataupata wapi?
   
 15. d

  dicaprio Member

  #15
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Our internal matters need to be worked upon first, so he is worth not to react to other sovereigns in the prematurity of the Ivorian troubles
  If tho people can't solve a simple riddle then one man shall never entertain it at all, due to vividity of failure
   
 16. k

  kijukuu kindo Member

  #16
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini hatatvibaka wa simu wanaochomwa moto pale kariakoo huchomwa na vibaka wenzao, hivyo naye JK asione aibu, aseme tu tutamsikiza.
   
 17. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu, umetoa point kama yangu. Ukweli Jk hawezi kutoa kauli juu ya hilo maana yatamgeuka baadaye. kama ile tume inayodaiwa na CHADEMA ikiundwa, atakuwa kikaangoni. paka hawezi kumtidhia paka mwenzake. yeye anajua njia zake zilizomweka madarakani.
   
Loading...