Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Kurugenzi ya mambo ya Nje ma Mahusiuano ya Kimataifa ya Chadema imeitaka serikali kulaani hadharani matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya kidemokrasia ya kimataifa unaofanywa na Laurent Gbagbo na wafuasi wake nchini Ivory Coast.
Aidha, kurugenzi hiyo inatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kutamka hadharani kumtambua Alassane Ouattara kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais katika nchi hiyo na kulaani vitendo vinavyofanywa na Gbagbo na wafuasi wake.
Taarifa iliyotolewa na Mkrugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya kimataifa ya Chadema john Mnyika ilisema:
Inashangaza kwamba wakati Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na serikali za nchi mbali mbali ndani na nje ya Afrika zimetoa matamko ya wazi, serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya diplomasia ya kimya. Hii ni tofauti kabisa na wakati wa Mwalimu Nyerere ambapo Tanzania ilikuwa mstari wa mbele na kutoa misimamo ya wazi ya kukemea vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora. ..
..Habari katika Nipashe katika Nipashe Jumapili.